JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
LISANDRO MARTINEZ MBIONI KUTUA MANCHESTER UNITED

Man. Utd inakaribia kumsajili beki wa Ajax ya Uholanzi, Lisandro Martinez (23) kwa ada ya Pauni Milioni 46 (Tsh. 126,960,000,000)

Ajax imemuainisha Mykola Matvienko kutoka Shakhtar Donetsk kuwa mbadala wa Lisandro

#JFSports
👍14🔥2
GAMBIA: Mahakama Kuu imemhukumu kifo Mkuu wa zamani wa Shirika la Ujasusi la Taifa, Yankuba Badjie na Maafisa wengine wanne wa zamani wa Shirika hilo kwa mauaji ya Mwanachama wa Chama cha Upinzani cha United Democratic Party mnamo mwaka 2016

Soma - https://jamii.app/GambiaExSpies

#Governance
👍10🤔1
MWANZA: Waziri wa Ardhi ameagiza uchunguzi wa manunuzi ya eneo la Isamilo linalolalamikiwa na Wananchi wakidai lilichukuliwa bila wao kulipwa fidia na sasa limeuzwa kwa 'Vigogo wa Serikali' licha ya wao pia kujaza fomu za ununuzi

Soma - https://jamii.app/MgogoroArdhiMwanza

#JFUwajibikaji
🤯7👍3👏2😁1
Rais wa Sri Lanka, Gotabaya Rajapaksa anatarajiwa kusafiri kutoka Maldives alikokimbilia kuelekea Singapore anakotarajiwa kuwasili jioni ya leo Julai 14, 2022

> Bado hajakabidhi barua ya kujiuzulu Nafasi ya Urais

Soma https://jamii.app/SriLankaPresident

#Governance
😁12🤔6👍3
RAIS SAMIA: SEKTA BINAFSI ZINAKATISHWA TAMAA KUFANYA KAZI NA SERIKALI

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa Serikali kushirikiana na Sekta Binafsi akisema kutofanya hivyo ni kuchelewesha maendeleo ya Nchi

Soma https://jamii.app/SektaBinafsiUshirikiano

#JFUwajibikaji #Governance
👍20
UKRAINE: Makombora ya Urusi yaliyorushwa yameripotiwa kuua takriban Watu 20 wakiwemo watoto watatu huku wengine 90 wakijeruhiwa

> Imeelezwa kuwa, makombora hayo yalirushwa kutoka katika Nyambizi ya Urusi

Soma https://jamii.app/20KilledInUkraine

#RussiaUkraineWar
😁13👍6😢3👎1
#JFAFYA: Shirika la Afya Duniani limeonya kuwa Afrika inakabiliwa na ongezeko la 60% la Magonjwa ambayo huenea kutoka kwa Wanyama hadi kwa Binadamu

> Miongoni mwa magonjwa hayo ni #Ebola, Magonjwa ya Kuvuja Damu, #Dengue, Kimeta na #MonkeyPox

Soma https://jamii.app/MagonjwaWHO

#PublicHealth
👍5👎1
RAIS WA SRI LANKA AJIUZULU KWA BARUA PEPE

Rais Gotabaya Rajapaksa amewasilisha barua ya kujiuzulu Urais wa Nchi hiyo kwa Spika wa Bunge kupitia Barua pepe

Inadaiwa ametuma Barua hiyo baada ya kuwasili Nchini Singapore

Soma - https://jamii.app/GotabayaOut

#Democracy
👍14😁10
CHELSEA YASITISHA MPANGO WA KUMSAJILI CRISTIANO RONALDO

Ni baada ya Kocha Thomas Tuchel kusema anataka mchezaji anayecheza kitimu na si kuangalia kipaji cha mmoja

Kufuatia kauli hiyo, itabidi Ronaldo abaki Man. Utd au atafute timu nyingine

Soma https://jamii.app/ChelseaCR7

#JFSports
👍42😁8🤩3👎2😱21🤔1🤮1
RIPOTI: Takriban Watoto Milioni 25 duniani walishindwa kupatiwa kwa wakati Chanjo muhimu zinazowalinda dhidi ya Magonjwa mbalimbali mwaka 2021

Ripoti ya Shirika la Afya Duniani (WHO) na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Watoto (UNICEF) inasema hali hiyo ilitokana na utoaji wa huduma za Afya kuathiriwa na COVID-19

Soma - https://jamii.app/WatotoChanjo

#JFAfya
👍4🤔2
JULAI 15: SIKU YA UJUZI KWA VIJANA DUNIANI

Inakadiriwa kuwa, nafasi za kazi Milioni 600 zitahitajika kuundwa katika kipindi cha miaka 15 ijayo ili kukidhi mahitaji ya Ajira kwa Vijana

Idadi ya Vijana inatarajiwa kuongezeka kwa zaidi ya Milioni 78 kati ya 2021 - 2030, ikielezwa takriban nusu ya ongezeko hilo itakuwa katika Nchi masikini

Soma - https://jamii.app/UjuziVijana

#WYSD2022
👍6
Kwa mujibu wa Shirika la UNICEF, Vijana watatu kati ya wanne hawana Ujuzi unaohitajika kwenye Ajira

Waliopo Nchi masikini wana uwezekano mdogo zaidi wa kuwa na Ujuzi muhimu kwa fursa za Ajira/Ujasiriamali

Mifumo ya Elimu inatajwa kukwamisha Vijana na Watoto wengi, ikiwaacha bila Maarifa, Ujuzi na hamasa yoyote

Soma - https://jamii.app/UjuziVijana

#WYSD2022
👍5😁3😢1
LUGHA: NINI KINASABABISHA WATU KUCHANGANYA MATUMIZI YA "R" NA "L"?

Mdau wa Jukwaa la Lugha anahoji ni nini kinapelekea makosa kwenye matumizi ya herufi "R" na "L" kuanzia kuyaandika mpaka kutamka?

Anatolea mfano maneno "Rakini" badala ya "Lakini", "Kalili" badala ya "Kariri"

Je, unapata changamoto kwenye matumizi ya herufi hizo?

Mjadala - https://jamii.app/MdauLughaRL

#JFLugha
👍11
MAHAKAMA: ZUIO LA TWITTER NIGERIA LILIKIUKA SHERIA

Mahakama ya Haki ya ECOWAS imesema zuio hilo la mwaka 2021 lilikiuka Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na kunyima Wananchi Haki ya #UhuruWaKujieleza na kupata taarifa

Nigeria imetakiwa kuhakikisha marufuku kama hiyo haijirudii

Soma - https://jamii.app/TwitterBanNGR

#DigitalRights #FreedomOfExpression
👍6
Taasisi ya WAJIBU imezindua Ripoti za Uwajibikaji, Mapato na matumizi ya Fedha za Umma 2020/21 iliyotokana na ripoti za Ukaguzi za Mamlaka ya Serikali za Mitaa, Miradi ya Maendeleo, Mashirika ya Umma na Serikali Kuu zilizotolewa na CAG

Dhumuni ni kuwapatia Wananchi taarifa ya namna Serikali ilivyotekeleza Bajeti ya Taifa katika ukusanyaji wa Mapato na Matumizi ya fedha za Umma kwa mwaka

#JFUwajibikaji
👍8
10% PUNGUFU KWENYE MAKUSANYO: Mwaka 2020/21 Serikali ilipanga kukusanya Tsh. trilioni 34.8, hata hivyo ilikusanya Tsh. trilioni 31.3 (90% ya makadirio)

> Hili ni ongezeko la 5% ikilinganishwa na 2019/20 ambapo Serikali ilishindwa kukusanya Mapato iliyokadirikia kwa 5%

#JFUwajibikaji
👍6🤔2🔥1
UPUNGUFU WA MAJENGO YA MAHABUSU NA WAFUNGWA

Gereza la Keko lilikuwa na msongamano mkubwa zaidi ambapo lilikuwa na Wafungwa 1,075 zaidi ya uwezo wake sawa na 194%

Magereza 8 kati ya 15 yaliyokaguliwa hayakuwa na huduma ya Maji Safi na Salama kutokana na kutolipia Huduma ya Maji kwa Mamlaka husika

#JFUwajibikaji
😢7🤔3👍2
KUCHELEWA KWA RIPOTI ZA CAG

Mwenyekiti wa Kamati ya PAC, Japhet Hasunga amesema CAG anatumia mifumo kuandaa ripoti yake hivyo ripoti hizo zitoke mapema ili Bunge pia liweze kuzijadili mapema

Hasunga amesema hiyo itatoa fursa ya Uwajibikaji kabla fedha nyingine hazijaombwa Bungeni

#JFUwajibikaji
👍14🤔2
SOMALIA: WAANDISHI WAHIMIZA SHERIA ZA VYOMBO VYA HABARI KUREKEBISHWA

Wamesema Kanuni za Adhabu na Sheria ya Vyombo vya Habari zimekuwa tishio kwa usalama wao

Wameeleza kuwa Sheria mpya hailindi usiri wa Vyanzo vya Habari, na inaruhusu Waandishi kuhukumiwa bila kupewa nafasi ya kukata rufaa

Soma - https://jamii.app/SomaliaJounalists

#PressFreedom
👍7
RAIS WA MPITO AAPISHWA SRI LANKA

Ranil Wickremesinghe aliyekuwa Waziri Mkuu ameapishwa kuwa Rais wa Mpito, akimrithi Gotabaya Rajapaksa aliyejiuzulu kufuatia maandamano

Atahudumu kwa muda uliosalia katika Muhula wa Rajapaksa unaokamilika 2024

Soma - https://jamii.app/RaisMpyaSriLanka

#Governance
👍11🔥1