JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
GEITA: Mkuu wa Wilaya ya Geita, Wilson Shimo amethibitisha vifo vya Wachimbaji 3 wa dhahabu na majeruhi wawili baada ya kuangukiwa na kifusi katika machimbo ya Nyamatagata

> Shughuli kwenye machimbo hayo zimesimamishwa kwa muda

Soma - https://jamii.app/VifoGeita

#JFMatukio
👍8😢3👎2
MANCHESTER UNITED YAMSAJILI ERIKSEN

Christian Eriksen (30) amesaini mkataba wa miaka mitatu kufuatia kufanyiwa uchunguzi mkali wa afya

Mchezaji huyo anaimarisha safu ya kiungo ya Erik ten Hag baada ya kuchagua kutosalia Brentford, alikokuwa msimu uliopita kwa mkopo

#JFSports
👍16👏1
JOTO KALI: UINGEREZA YATANGAZA HALI YA DHARURA

Mamlaka imetangaza hali ya dharura ya Kitaifa na kutoa onyo la joto kali katika baadhi ya maeneo

Wataalamu wamesema joto linaweza kufikia viwango vya juu vinavyoweza kuathiri watu na miundombinu

Soma - https://jamii.app/UKHeatRise
👍8🤔4👎21🔥1😁1
UGANDA: Zaidi ya watu 500,000 katika Mkoa wa Karamoja wanakabiliwa na njaa iliyosababishwa na ukame uliodumu kwa muda mrefu

Aidha, watu kadhaa wameripotiwa kufariki dunia maeneo ya Kaskazini Mashariki ya Nchi hiyo kutokana na njaa

Soma - https://jamii.app/UgandaNjaa
😢11👍4😱1
MISRI KUONDOA VIKOSI VYAKE VYA KULINDA AMANI NCHINI MALI

UN imesema Misri itaondoa Wanajeshi wake ifikapo Agosti 15. Kujitoa kwao ni pigo jingine baada ya doria za Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa nchini Mali kusitishwa kwa muda

Wanajeshi 7 wa Misri wameuawa mwaka 2022

Soma https://jamii.app/VikosiMali

#Diplomacy
👍11👏1
AFRIKA KUSINI: Mamia waandamana kushinikiza kuondolewa kwa Rais Ramaphosa kutokana na kupanda kwa gharama za maisha na kukatika kwa umeme mara kwa mara

> Sababu nyingine ni kukithiri kwa rushwa ktk Taasisi za Umma na ukosefu wa ajira

Soma https://jamii.app/MaandamanoAfrikaKusini

#Democracy
👍14🔥4😁2
BARCELONA YAKUBALIWA KUMSAJILI LEWANDOWSKI

Mshambuliaji wa Bayern Munich, Robert #Lewandowski atasajiliwa kwa takriban Tsh. Bilioni 117

> Anasafiri leo kwenda Hispania kukamilisha usajili huo, anatarajiwa kusaini miaka mitatu

Soma https://jamii.app/LewandowskiBarca

#JFSports
👍21
TMA: NJOMBE KUNA SAKITU SIYO THELUJI

Mamlaka Hali ya Hewa (TMA) imefafanua kuwa kinachotokea Njombe hivi karibuni ni Sakitu inayosababishwa na umande kuganda na siyo Theluji

> Pia, Upepo wa Kusi unasababisha baridi kali maeneo mengine Nchini

Soma https://jamii.app/BaridiLaNjombe
👍11😁2🎉1
UTAFITI: KANDA YA ZIWA YAONGOZA UKATILI WA WENZA

Wataalamu wa Afya wamesema Mikoa inayoongoza ni Mara, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Geita

> Mikoa ambayo ina kiwango cha chini cha ukatili kwa wenza ni Pemba, Ukanda wa Pwani na Tanga

Soma https://jamii.app/UkatiliRipoti

#JFSaikolojia
👍14🤔1
KOCHA WA BARCELONA AZUIWA MAREKANI

Kocha Xavi Hernandez amezuiwa kwenda Marekani kutokana na rekodi ya kuingia Nchini Iran zaidi ya mara tatu

Ili kuingia Marekani, yeyote mwenye rekodi kama hiyo anatakiwa kupata kibali maalum

Soma > https://jamii.app/XaviMarekani

#JFSports
😱12👍7😁7💩7🤔5🎉1
KENYA: MTENGENEZA MAUDHUI YA 'TIKTOK' ALAZWA BAADA YA KULA BUIBUI

Inadaiwa Aq9ine alianza kuumwa kifua huku joto la mwili likifika 48℃ baada ya kula buibui

Baada ya kushambuliwa Mitandaoni amesema akipona, atapika na kula chura na nyoka

Soma - https://jamii.app/TiktokerHospitalized
😁10🤔6👍1
MEXICO: Helikopta iliyokuwa ikitumika kusaka wahalifu wakiwemo wa dawa za kulevya imeanguka na kuua watu 14, huku mmoja akijeruhiwa vibaya

Chanzo cha ajali ya ndege hiyo hakijawekwa wazi

Soma - https://jamii.app/HelikoptaMexico
👍8😁4🤔4👎2🤮1
Huduma ya Intaneti imetoa usaidizi mkubwa katika kutafuta kazi, lakini bado ina safari ndefu kuwa namna ya kutegemewa katika kutafuta kazi kwenye jamii masikini kwani ufikiaji wake ni changamoto

Kwa mujibu wa Takwimu za Benki ya Dunia, ongezeko la 10% la upenyaji wa Intaneti Afrika linaweza kuongeza Pato la mtu mmoja mmoja kwa karibu 2.5%

Soma - https://jamii.app/HudumaIntaneti

#JFData #DigitalRights
👍7
WAMAREKANI 61 MARUFUKU KUINGIA IRAN

Iran imetoa orodha ya majina 61 ya Wamarekani ambao hawaruhusiwi kuingi Iran. Sababu kubwa ni kuunga mkono kikundi cha MEK ambacho wanakishutumu kwa ugaidi

Wengi wao ni Maofisa wa Serikali

Soma - https://jamii.app/IranUSA

#JFDiplomasia
👍14👎1
MDAU: JINSI YA KUTIBU/KUZUIA KISUKARI KWA KUTUMIA LISHE

Saga Karoti, Tango, Kitunguu Maji, Hoho, Nyanya na Limau likiwa na maganda na mbegu zake

> Kunywa mchanganyiko huo kila asubuhi dakika 45 au 60 kabla ya kula kitu kingine

Je, unafahamu lishe gani nyingine?

Soma https://jamii.app/TibaYaKisukari

#PublicHealth #JFAfya
👍293🤮3😁2
MANCHESTER UNITED KUMSAJILI LISANDRO

Imefikia makubaliano na Ajax kumsajili Lisandro Martinez (24) kwa £55.3m (Tsh. 151,522,000,000)

Atakuwa beki wa 2 ghali zaidi ktk klabu hiyo baada ya Harry Maguire

Atasaini mkataba wa miaka 5 na kulipwa £120,000 (Tsh. 328,800,000) kwa wiki

#JFSports
👍23😁9🔥3💩2
#UKRAINE: Rais Volodymyr Zelensky amewafuta kazi Mkuu wa Idara ya Usalama, Ivan Bakanov na Mwendesha Mashtaka Mkuu, Iryna Venediktova

Amesema hatua hiyo ni kufuatia tuhuma za maafisa wao kushirikiana na #Russia

Soma https://jamii.app/MaafisaUkaine
👍11😢1
CHELSEA YATAKA KUWASAJILI KIMPEMBE NA KOUNDE

Chelsea imetoa ofa ya Paundi Milioni 40 (Tsh. 109,600,000,000) ili kumnasa Beki wa PSG, Presnel Kimpembe (26)

Aidha, imerejea kwenye mazungumzo ya kumsajili Beki wa Sevilla, Jules Kounde (23) anayewaniwa pia na Barcelona

#JFSports
👍8🥰1
ARSENAL MBIONI KUMSAJILI ZINCHENKO

Arsenal ina tumaini la kumsajili Beki wa Manchester City, Oleksandr Zinchenko (25) wiki hii, baada ya kutoa ofa ya Paundi Milioni 35 (Tsh. 95,900,000,000)

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta anathamini sana uwezo wa Beki huyo wa Kushoto

#JFSports
👍9🔥1
Kila Julai 18, Siku ya Mandela au Siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela inasherehekewa duniani kote kuenzi mafanikio ya Kiongozi huyo

Kwa mwaka 2022, Maadhimisho haya yanaangazia Usalama wa Chakula na Mabadiliko ya TabiaNchi

Mandela alizaliwa Julai 18, 1918 na kufariki dunia Desemba 5, 2013. Alikuwa Rais wa Afrika Kusini kati ya 1994 - 1999

Soma zaidi - https://jamii.app/Mandela2022

#MandelaDay
👍9👏1