JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
SIMIYU: Watu wanne wamepoteza maisha baada ya magari waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso eneo la Nyaumata-Bariadi Julai 12, 2022

> Kamanda wa Polisi-Simiyu amesema chanzo cha ajali ni mwendo kasi na Madereva wanashikiliwa na Polisi

Soma https://jamii.app/AjaliBariadi

#JFMatukio
😢9👍3👎1
KAIMOSI, KENYA: ATUHUMIWA KUMUUA BINAMU KATIKA UGOMVI WA KUCHAJI SIMU

Inadaiwa alimuua kwa kumchoma mshale kifuani wakati kila mmoja alipokuwa akitaka kuwa wa kwanza kuanza kuchaji simu

Mtuhumiwa alikimbia baada ya tukio na anatafutwa na Polisi

Soma > https://jamii.app/AmuuaBinamuKE

#JFMatukio
😢14👍11👎1
Fuatilia Mkutano na Waandishi wa Habari kuhusu Uzinduzi wa Awamu ya Pili ya Shindano la Stories Of Change Mwaka 2022 litakaloanza Julai 15

Bonyeza > https://fb.watch/eecsLXntHU/

#StoriesOfChange #SOC2022
👍5
AWAMU YA PILI YA SHINDANO LA "STORIES OF CHANGE" YAZINDULIWA

Shindano linakusudia kuongeza maudhui bora Mtandaoni na kuhamasisha ushiriki wa raia

Andiko linatakiwa kuchochea mabadiliko kwenye nyanja mbalimbali zikiwemo za Elimu, Uchumi, Kilimo, Utawala, Afya, Sayansi na Teknolojia

Kwa taarifa zaidi - https://jamii.app/Shindano2

#StoriesOfChange #SOC2022
👍11
STORIES OF CHANGE: Maandiko yawasilishwe kuanzia Julai 15 hadi Septemba 14, 2022 kwenye Jukwaa la “JF Stories Of Change"

Mtanzania yeyote mwenye umri wa miaka 18 na zaidi anaweza kushiriki

Maelezo zaidi > https://jamii.app/Shindano2

#StoriesOfChange #SOC2022
👍11
UPDATE: Waziri Mkuu wa Sri Lanka, Ranil Wickremesinghe ambaye anakaimu nafasi ya Urais kwa sasa baada ya Rais Gotabaya Rajapaksa kukimbia, ametangaza Hali ya Hatari

Inaripotiwa kuwa, Ofisi yake imezingirwa na mamia ya Waandamanaji

Soma - https://jamii.app/SOESriLanka

#Democracy
👍12🔥2
UGONJWA USIOFAHAMIKA LINDI: Wizara ya Afya imesema kufikia Julai 12, 2022 kulikuwa na Wagonjwa 13, na 3 kati yao wamefariki dunia

Sampuli za awali zimeonesha Majibu Hasi kwa Magonjwa ya Ebola, Marburg na UVIKO-19, vipimo zaidi vinasubiriwa

Wenye dalili za Homa, Kuvuja Damu puani, kuumwa kichwa na mwili kuchoka wanaendelea kutafutwa

Soma - https://jamii.app/UgonjwaLindiWA

#JFAfya
🤔9👍7
RWANDA: AFISA WA ZAMANI WA SERIKALI AHUKUMIWA MIAKA 20 JELA KWA MAUAJI YA HALAIKI

Laurent Bucyibaruta aliyekuwa Gavana wa Gikongoro Kusini amekutwa na hatia ya mauaji ya mwaka 1994, akidaiwa kutumia ushawishi wa nafasi yake kuhimiza maelfu ya Watutsi kukimbilia Shule ya Ufundi ya Murambi kwa hifadhi ambapo waliuawa

Soma - https://jamii.app/RwandaGenocide
👍8🤔1
MALI: Takriban Wanajeshi 50 wa Ivory Coast wanashikiliwa ikidaiwa ni Mamluki waliowasili Nchini humo kwa mgongo wa Umoja wa Mataifa (UN)

> UN imesema Wanajeshi hao waliingia Mali kwa kazi maalum ktk Mradi wa Sahelian Aviation Services

Soma https://jamii.app/WanajeshiWazuiwaMali

#Governance
👍6😁1
KENYA: Baraza la Habari limetoa wito kwa Polisi kuchunguza kwa haraka mashambulizi dhidi ya Wanahabari siku chache baada ya kushambuliwa kwa Mwanahabari Ian Byron

> Anadaiwa kushambuliwa kufuatia kuandika habari kumhusu Mbunge, Junet Mohamed

Soma https://jamii.app/PressFreedom

#PressFreedom
👍8
TERAT, ARUSHA: Watu watatu wa familia moja wamefariki Dunia papo hapo kwa kugongwa na gari wakati wakitoka hospitalini wakiwa wamepanda pikipiki

> Waliofariki ni Ebenezer Mollel (1), Neema Mollel (27) na Agustino Mollel (24)

Soma https://jamii.app/AjaliArushaJulai

#JFMatukio
😢12👍1👎1
MDAU: NAPITIA WAKATI MGUMU, NAANZIA WAPI KUTAFUTA PESA?

Anasema baada ya harakati zilizomleta Mjini kufeli, Kaka yake amemwambia atamsaidia malazi na kumtaka kujisimamia katika mahitaji mengine

Ndugu yake amemwambia, "Umeshakuwa mtu mzima, Mji umeujua hivyo uanze kujitafutia kipato badala ya kukaa tu nyumbani"

Ni ushauri/wazo gani unaweza kumpa kumsaidia?

Mjadala - https://jamii.app/UshauriMdau
👍24
CHELSEA KUTANGAZA USAJILI WA KOULIBALY

Usajili wa Kalidou #Koulibaly kutoka Napoli kwenda Chelsea unatarajiwa kukamilika leo Julai 14, 2022

> Beki huyo anaweza kutangazwa baada ya kukamilisha Vipimo vya Afya

Soma https://jamii.app/KoulibalyChelsea

#JFSports
👍15👏2
SRI LANKA: Watu 84 wamejeruhiwa na mmoja amefariki dunia kufuatia mvutano kati ya Maafisa wa Polisi na Waandamanaji karibu na jengo la Bunge na katika Ofisi ya Waziri Mkuu

Wananchi wanasubiri Rais Gotabaya Rajapaksa ajiuzulu rasmi, lakini bado barua yake haijawasilishwa

Soma - https://jamii.app/84InjuredSL

#Democracy
👍8😢8👎1
Watanzania wengi wanaendelea kujiunga Mtandaoni, lakini kasi ya ukuaji wa Watumiaji hailingani na uelewa uliopo kuhusu Uhalifu wa Mitandaoni

Ripoti ya CIPESA inasema Watumiaji wengi wa Intaneti hawafahamu kuhusu uhalifu mtandaoni, au kwanini wanahitaji kulinda Faragha zao

Soma - https://jamii.app/CyberCrimesCPS

#DataPrivacy #DigitalRights
👍7
LISANDRO MARTINEZ MBIONI KUTUA MANCHESTER UNITED

Man. Utd inakaribia kumsajili beki wa Ajax ya Uholanzi, Lisandro Martinez (23) kwa ada ya Pauni Milioni 46 (Tsh. 126,960,000,000)

Ajax imemuainisha Mykola Matvienko kutoka Shakhtar Donetsk kuwa mbadala wa Lisandro

#JFSports
👍14🔥2
GAMBIA: Mahakama Kuu imemhukumu kifo Mkuu wa zamani wa Shirika la Ujasusi la Taifa, Yankuba Badjie na Maafisa wengine wanne wa zamani wa Shirika hilo kwa mauaji ya Mwanachama wa Chama cha Upinzani cha United Democratic Party mnamo mwaka 2016

Soma - https://jamii.app/GambiaExSpies

#Governance
👍10🤔1
MWANZA: Waziri wa Ardhi ameagiza uchunguzi wa manunuzi ya eneo la Isamilo linalolalamikiwa na Wananchi wakidai lilichukuliwa bila wao kulipwa fidia na sasa limeuzwa kwa 'Vigogo wa Serikali' licha ya wao pia kujaza fomu za ununuzi

Soma - https://jamii.app/MgogoroArdhiMwanza

#JFUwajibikaji
🤯7👍3👏2😁1
Rais wa Sri Lanka, Gotabaya Rajapaksa anatarajiwa kusafiri kutoka Maldives alikokimbilia kuelekea Singapore anakotarajiwa kuwasili jioni ya leo Julai 14, 2022

> Bado hajakabidhi barua ya kujiuzulu Nafasi ya Urais

Soma https://jamii.app/SriLankaPresident

#Governance
😁12🤔6👍3
RAIS SAMIA: SEKTA BINAFSI ZINAKATISHWA TAMAA KUFANYA KAZI NA SERIKALI

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa Serikali kushirikiana na Sekta Binafsi akisema kutofanya hivyo ni kuchelewesha maendeleo ya Nchi

Soma https://jamii.app/SektaBinafsiUshirikiano

#JFUwajibikaji #Governance
👍20