JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
TUNISIA: RASIMU YA KATIBA ILIYOANDALIWA NA RAIS YADAIWA ITAFUTA UTAMBULISHO WA NCHI

Imedaiwa baadhi ya vifungu ktk Rasimu hiyo vinaweza kufungua njia kwa Utawala wa Kidikteta na ni tofauti na rasimu iliyopendekezwa na Kamati ya kuandaa Rasimu

Soma - https://jamii.app/KatibaTunisia
👍5
RONALDO AKWAMA KUFIKA MAZOEZINI MAN UNITED

Mshambuliaji Cristiano Ronaldo hajaripoti mazoezini Manchester United, sababu ametaja ni matatizo ya kifamilia

Alitakiwa kurejea leo Julai 4, 2022 kuanza kazi

Soma > https://jamii.app/RonaldoUtd

#JFSports
👍15🤔1
SRI LANKA YAISHIWA PETROLI

Serikali imesema Taifa hilo lina Petroli ya kutosha siku isiyozidi moja kwa mahitaji ya kawaida

Petroli nyingine inatarajiwa kati ya Julai 22 - 23, lakini Nchi hiyo haina Fedha za kutosha kulipia Mafuta hayo

Soma - https://jamii.app/PetroliSriLanka
👍8🤔4🎉1
ERIKSEN AKUBALI KUJIUNGA NA MAN. UNITED

Kiungo Christian Eriksen anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka mitatu Man. United

> Eriksen (30) anajiunga akiwa mchezaji huru baada ya kuichezea Brentford msimu uliopita

Soma - https://jamii.app/EriksenManU

#JFSports
👍14
MAANDAMANO YAENDELEA LIBYA, VIJANA WAINGIA MTAANI

Kuongezeka kwa bei ya bidhaa na kuendelea kwa migogoro ya kisiasa ni baadhi ya sababu za maandamano

Kundi la Vijana la "Beltress" limesema litaendeleza maandamano Mjini #Tripoli

Soma > https://jamii.app/LibyaChaos

#JamiiForums
👍9
DAR: Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA, Madeni Kipande (66) amesomewa mashtaka ya kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Tsh. Bilioni 4.2 akiwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, leo Julai 4, 2022

Soma - https://jamii.app/BossTPA

#JamiiForums
🤔16👍8🔥1
CHELSEA YAANGALIA UWEZEKANO WA KUMSAJILI RONALDO

Inadaiwa Chelsea inafikiria kumnunua Cristiano Ronaldo wakati kukiwa na sintofahamu ya mustakabali wake katika klabu ya Man. Utd

Inaelezwa Ronaldo aliiambia klabu hiyo anataka kuondoka iwapo itapatikana ofa inayofaa

#JFSports
👍16🤮3
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Jifunze, kuwa bora kuliko jana na weka bidii zaidi kutimiza malengo yako!

#JamiiForums
👍23👏4🙏2
SUDAN: Kiongozi wa Mapinduzi, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan amesema Jeshi litajiondoa katika mazungumzo ya Siasa yanayoendelea, na kuyaachia Makundi ya Kisiasa na Kimapinduzi mchakato wa kuunda Serikali ya Mpito

Tangu Mapinduzi ya Oktoba 2021, kumekuwa na maandamano ya kupinga Utawala wa Kijeshi

Soma - https://jamii.app/JeshiSDN
👍13
INDIA: 'SERVICE CHARGE' ZAPIGWA MARUFUKU HOTELINI

Kufuatia malalamiko ya kulazimishwa kulipa, Hoteli na Migahawa zimezuiwa kuwatoza Wateja Gharama za Huduma (Service Charge)

Aidha, Migahawa imezuiwa kuwanyima Huduma wateja wanaokataa kutoa 'Tip'

Soma - https://jamii.app/SCHotelsIndia
👍13
Kiongozi Mkuu wa M23, Sultani Makenga amedaiwa kurejea toka mafichoni na kuungana na Wanamgambo wake huko Mashariki mwa DR Congo

> Inadaiwa kurejea kwake ni kutokana uwezekano wa Jeshi la Afrika Mashariki kuungana na Jeshi la DRC ktk kupambana na M23

Soma - https://jamii.app/KamandaM23
😁13👍2🤔2
CAMEROON: Shirikisho la Soka Nchini humo linachunguza Wachezaji 44 kutoka katika Klabu 8 kwa tuhuma za kudanganya umri au utambulisho wao

> Iwapo watapatikana na hatia watakabiliwa na adhabu ya kufungiwa kwa miezi 6 kushiriki mechi

Soma - https://jamii.app/WachezajiWachunguzwa

#JFSports
👍10
RUTO: NILIMFANYA KENYATTA KUWA RAIS WA KENYA

Naibu Rais wa Kenya, William Ruto amesema kuwa Mahakama ilipoamuru Uchaguzi wa Marudio mwaka 2017, Kenyatta hakutaka kurudia ila yeye ndiye alimlazimisha kurudia uchaguzi huo na kumfanya kuwa Rais

Soma - https://jamii.app/RuttoVsKenyatta
👍16🤮5
MATOKEO KIDATO CHA 6: Watahiniwa 93,136 (98.97%) wamefaulu Mitihani, ikielezwa Wasichana ni 40,907 na Wavulana ni 52,229. Watahiniwa 83,877 (99.24%) wamefaulu katika Daraja 1 - 3

Ufaulu wa Masomo ya General Studies, Geography na Basic Applied Mathematics (BAM) umeshuka

Soma - https://jamii.app/MatokeoKidato6
👍16
WAZIRI UMMY MWALIMU: NAPATA KIGUGUMIZI KUSEMA TUSIVAE BARAKOA

Amesema Nchi nyingine zimeondoa uvaaji barakoa kwasababu wamechanja watu zaidi ya 70%

Ameeleza, "Napata kigugumizi ninapoulizwa, tungekuwa tumechanja angalau 50% ningesema tuache"

Soma - https://jamii.app/UvaajiBarakoaTZ
👍17👎3
DAR: Rais Samia Suluhu amefurahishwa na mpango wa Hospitali ya CCBRT kuwa na vyumba binafsi kwa ajili ya kujifungulia vinavyoruhusu Mwenza kuwepo wakati wa kujifungua

> Amesema "Hii itasaidia Waume zetu kuona kishindo tunachopambana nacho kule ndani"

Soma - https://jamii.app/CCBRTSamia
😁26👍6👏32👎1
DAR: Rais Samia Suluhu Hassan amesema vifo vingi vya kina Mama na Watoto wakati wa kujifungua vinatokana na Watoa Huduma kutozingatia weledi, kuwa na dharau au uzembe

> Ameagiza Wizara ya Afya kufuatilia huduma katika Vituo vya Afya

Soma - https://jamii.app/CCBRTSamia
👍8
DAR: Rais Samia amesema inakadiriwa Wanawake 12,000 hadi 18,000 wana tatizo la fistula nchini. Watoto wa miaka 4-12 wana tatizo hilo huku sababu mojawapo ya tatizo hilo ikiwa ni Ubakaji

> Amesisitiza Jamii kutofumbia macho tatizo la Ubakaji

Soma - https://jamii.app/WagonjwaFistula
👍11
Uganda imegundua tani milioni 31 za dhahabu zenye thamani ya dola trilioni 12 katika Wilaya ya Busia na imeipa leseni Kampuni ya Uchimbaji Dhahabu ya Kichina kuanza kuchimba bidhaa za dhahabu kwa miaka 21

Soma - https://jamii.app/UgandaGoldDeposit

#JamiiForums
👎20😁10🤔6👍3
RAIS SAMIA: TANGANYIKA PACKERS PAJENGWE KITUO CHA MICHEZO

Rais amesema, "Licha ya tatizo la umiliki wa eneo hilo lakini Wizara ya Michezo angalieni uwezekano wa kujenga Kituo cha Michezo eneo hilo la Kawe, Dar es Salaam"

Mbali na kuwa na Kituo cha Mabasi yaendayo maeneo mbalimbali Dar es Salaam, eneo hilo kwa sasa pia hutumika kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo maombi

Soma - https://jamii.app/SamiaUwanja

#JFSports
👍3