JamiiForums
βœ”
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
WABUNGE WALIOFUKUZWA WAPO BUNGENI

Wabunge wa Viti Maalum, Salome Makamba na Grace Tendega ambao walifukuzwa Uanachama CHADEMA, wameshiriki katika shughuli za Bunge, leo Juni 23, 2022 na wamepata nafasi ya kuuliza Maswali ya Nyongeza

> Juni 22, 2022 Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ilitupilia mbali maombi ya Wabunge 19 waliopinga kufukuzwa Uanachama na CHADEMA

Soma https://jamii.app/MdeeWenzake

#JamiiForums
πŸ‘Ž13πŸ€”7😁5😱4πŸ‘2
AJALI YA TRENI TABORA: Rais Samia Suluhu Hassan ametuma Salamu za Rambirambi na kutaka hatua stahiki zichukuliwe

> TRC ilisema chanzo cha ajali kilikuwa ni hujuma kwani kipande cha reli kiliondolewa na kurudishwa kwa kuegeshwa ktk eneo la ajali

Soma https://jamii.app/AjaliYaTreni
πŸ‘12😱2😒2
#JFSPORTS: Kiungo Rally Bwalya sasa ni Mchezaji halali wa Amazulu ya Afrika Kusini iliyomsajili akitokea Simba

> Timu ya Amazulu imemaliza Msimu wa 2021/22 ikiwa nafasi ya 7 katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini kati ya timu 16

Soma https://jamii.app/RallyBwalya

#JamiiForums
πŸ‘14πŸ‘6
AFGHANISTAN: Mvua zinazoendelea kunyesha na uharibifu wa majengo na miundombinu ni kikwazo kwa jopo la uokoaji ktk eneo ambalo tetemeko la ardhi liliua zaidi ya Watu 1,000 na kujeruhi takriban 1,500

> Taliban imetoa wito wa msaada wa Kimataifa

Soma:https://jamii.app/AfghanRescue
😒6πŸ‘4πŸ€”3
MDAU: Nakerwa na tabia ya Watumia Kiswahili kurudia maneno bila kuwa na maana wanapozungumza

> Mfano sentensi kama β€˜Mimi kama mimi niko makini’ inakuwa sawa ukisema 'Mimi niko makini’

Je, unakerwa na tabia gani toka kwa Watumiaji wa Kiswahili?

Soma https://jamii.app/Kiswahili
πŸ‘13😁9πŸ’©2
Mbunge wa Iringa Mjini, Jesca Msambatavangu amesema kuwa Sheria iliyoundwa kudhibiti Maduka ya Kubadilisha Fedha za Kigeni ziondolewe ili kuimarisha Sekta Binafsi

> Amesema Sheria hizo zinakandamiza juhudi za kukuza utalii na kutoa ajira

Soma: https://jamii.app/SheriaBureauDeChange
πŸ‘4
RUTO: NITAWAFUKUZA WACHINA NIKISHINDA URAIS

William Ruto (55) ameahidi kuwafukuza Wachina wote wanaofanya kazi au biashara zinazoweza kufanywa na Wakenya iwapo atashinda uchaguzi Agosti 9, 2022

> Ubalozi wa China Nchini humo haujatoa tamko lolote

Soma https://jamii.app/RutoNaWachina
πŸ‘Ž26😁11πŸ‘7πŸ€”3πŸ”₯2
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo amesema anatamani Jeshi la Tanzania liwe la kisasa zaidi, kuchangia uchumi wa Nchi na liwe la kujitegemea

> Asema anapenda Wanajeshi wawe na Afya ya Akili na wafikirie Maendeleo ya Jeshi

Soma https://jamii.app/GeneraliMabeyo
πŸ‘39😁13❀1πŸ”₯1
UINGEREZA: Serikali imetangaza awamu mpya ya Vikwazo vya kibiashara dhidi ya #Russia ikiwemo marufuku ya kusafirisha bidhaa na teknolojia mbalimbali nchini humo, usafirishaji wa mafuta ya ndege na usafirishaji wa Noti za Umoja wa Ulaya

Soma: https://jamii.app/NewEconomicSactions
πŸ‘9πŸ‘Ž3
TETESI: CHELSEA YAANGALIA UWEZEKANO WA KUMSAJILI DE LIGT

Baada ya Antonio Rudiger na Andreas Christensen kuondoka, Chelsea inataka kumsajili beki wa kati wa Juventus, Matthijs de Ligt (22)

Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Uholanzi ana mkataba na Juventus hadi mwaka 2024

#JFSports
πŸ‘14πŸ‘3πŸ₯°2😁2
GHANA: Bunge laidhinisha uchunguzi wa matumizi ya Tsh. Trilioni 3.5 za kupambana na athari za #COVID19 kufuatia madai ya kutofautiana kwa stakabadhi za malipo zilizowasilishwa na Waziri wa Fedha, Ken Ofori-Atta na za Rais Nana Akufo-Addo

Soma - https://jamii.app/BungeUchunguzi

#JamiiForums
πŸ‘12
SIMBA 2-0 MTIBWA SUGAR

Beki wa Simba, Pascal Wawa ameagwa vizuri na timu yake ambayo imeshinda Mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Mtibwa Sugar katika Uwanja wa Mkapa, Juni 23, 2022

> Magoli yamefungwa na Pape Sakho na Peter Banda

Soma: https://jamii.app/Simba2Mtibwa0
#JFSports
πŸ‘15
MONKEYPOX YAINGIA AFRIKA KUSINI

Mwanaume wa miaka 30 Mkazi wa Jiji la Johannesburg ametangazwa kuwa na Virusi vya #Monkeypox

> Serikali imesema mgonjwa huyo hana historia ya kusafiri hivyo inafuatilia kujua alikoupata ugonjwa huo

Soma https://jamii.app/MonkeypoxSA
#JamiiForums
πŸ€”6πŸ‘5πŸ‘Ž3😒2
UMOJA WA MATAIFA: Ghasia zinazoendelea Magharibi mwa Sudan kwa mwezi Juni 2022 zimesababisha raia 84,000 kukimbia makazi yao

> Hizo ni takwimu za juu zaidi kwa Watu kukimbia makazi ndani ya mwezi mmoja tangu Januari 2021

Soma https://jamii.app/ChaosInSudan

#JamiiForums
πŸ‘6😒3πŸ₯°1
#JFSPORTS: FIFA yapitisha mpango wa kuruhusu kikosi cha Wachezaji 26 kwenye Michuano ya Kombe la Dunia Qatar 2022

> Hapo awali kila timu ilitakiwa kuthibitisha majina ya Wachezaji 23 yaani 11 wa uwanjani na 12 wa akiba kwenye kikosi chake

Soma: https://jamii.app/FIFAWachezaji
#JamiiForums
πŸ‘11πŸ‘9
BENKI KUU YA TANZANIA: Benki na Taasisi za Fedha zipunguze masharti ya mikopo na riba ili malengo ya kuwawezesha Wananchi Kiuchumi yaweze kutimia

> Benki ambazo hazitashusha gharama za uendeshaji hazitaruhusiwa kutoa gawio

Soma https://jamii.app/GavanaBOT

#JamiiForums
πŸ‘21
#Netflix kwa awamu ya pili imeachisha kazi takriban Wafanyakazi 300 kama namna ya kudhibiti gharama za uendeshaji. Mnamo mwezi Mei ilipunguza Wafanyakazi takriban 150

> Kampuni hiyo imedaiwa kupoteza Watazamaji 200,000 mwaka huu

Soma: https://jamii.app/NetflixWafanyakazi
#JFEntertainment
πŸ‘11πŸ‘Ž1
MDAU: Mafundi wengi wa Simu Mitaani hawana uwezo mzuri kwenye teknolojia na wamekuwa wagumu kukiri hivyo wamekuwa wakiharibu vifaaa vya wateja wao

> Je, imewahi kukutokea Fundi wa Mtaani akaharibu zaidi kifaa chako badala ya kukirekebisha?

Soma https://jamii.app/FundiSimu
πŸ‘18πŸ‘3
Mwigulu Nchemba (Waziri wa Fedha): Duniani kote nchi zinazotekeleza Miradi mikubwa ya Maendeleo na zenye Uchumi mkubwa, zina madeni makubwa. Ipo hivyo, nendeni mkaangalie

> Huwezi linganisha Uchumi wa Tanzania na Marekani

#JamiiForums #Bajeti2022
πŸ‘Ž11πŸ‘6
Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama ameagiza Sekretarieti ya Ajira kutangaza Vijana waliofaulu usaili wa ajira za Utumishi wa Umma na ajira zote mpya zianze kufanya kazi Julai 1, 2022

Soma: https://jamii.app/AjiraMpyaJulai1
πŸ‘19