JamiiForums
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
UKRAINE: Rais Volodymyr Zelensky ameonya kuwa uvamizi wa Urusi dhidi ya Nchi yake ulikuwa mwanzo tu, na malengo ya Moscow yanavuka Mipaka ya #Ukraine

Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa UN anatarajiwa kukutana na Marais wa Ukraine na Urusi wiki ijayo

Soma - https://jamii.app/ZelenskyUrusi
JAPANI: Askari wa Ulinzi wa Pwani ya Japani wanatafuta Boti ya Watalii iliyokuwa na Watu 26 iliyopotea katika Kisiwa cha Kaskazini cha Hokkaido

> Mamlaka imesema ilipoteza mawasiliano na boti hiyo iliyokuwa ikizunguka Rasi ya Shiretoko

Soma: https://jamii.app/BotiyapoteaJapani
YANGA YAIFUNGA NAMUNGO 2-1

Ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Namungo umeifanya #Yanga kuongoza Ligi Kuu kwa tofauti ya pointi 13

Mayele na Fei Toto wameifungia Yanga, bao la Namungo limefungwa na Kichuya

Soma - https://jamii.app/Yanga2Namungo1

#JFSports
DR CONGO: KISA KIPYA CHA EBOLA CHAREKODIWA

Ikiwa ni miezi minne tangu mlipuko wa mwisho kumalizika, Mwanaume mmoja (31) Mkazi wa Mbandaka, Kaskazini Magharibi mwa Nchi hiyo amethibitishwa kuugua #Ebola

Taifa hilo limeshuhudia milipuko 13 ya Ebola

Soma - https://jamii.app/mlipukowaebola
NIGERIA: MLIPUKO KWENYE KIWANDA HARAMU WAUA ZAIDI YA WATU 100

Vyombo vya Habari Nchini #Nigeria vimeripoti kuwa zaidi ya watu 100 wamefariki dunia baada ya kuteketea kwa moto kufuatia mlipuko katika Kiwanda kinachochakata Mafuta kinyume na Sheria

Soma - https://jamii.app/100DeadNigeria
👍1
UINGEREZA: Bondia Tyson Fury ametetea Mkanda wa WBC The Ring baada ya kumpiga Dillian Whyte kwa TKO ktk Pambano la Uzito wa Juu, usiku wa kuamkia Aprili 24, 2022

> Pia, Uwanja wa Wembley uliweka rekodi ya kujaza mashabiki wengi kwenye ndondi

Soma - https://jamii.app/FuryAshinda
MGOGORO WA #URUSI NA #UKRAINE: Rais Volodymyr Zelensky kwa mara nyingine ameomba kukutana na Rais Vladimir Putin katika juhudi za kumaliza vita baina ya nchi hizo

> Hii ni mara ya pili Zelensky anaomba kukutana na Putin kwa mazungumzo

Soma - https://jamii.app/UrusiUkraineVita
WATANZANIA WAANDAMANA UBALOZINI NCHINI MAREKANI

Baadhi ya Watanzania wameonekana wakiandamana Ubalozi wa Tanzania Nchini Marekani

Wameshika mabango yenye madai mbalimbali na kuyaonesha kwa Viongozi waliowakuta nje ya Ubalozi

Soma - https://jamii.app/MaandamanoMarekani

#JamiiForums
KILIMANJARO: Salah Jackson (5) mwenye ulemavu wa viungo amefariki dunia kutokana na njaa kisha mama yake mzazi, Rebecca Siowi (30) kumzika kimya kimya usiku wa manane kuamkia Aprili 22, 2022

> Polisi wameufukua mwili kujiridhisha sababu ya kifo

Soma https://jamii.app/AfaKwaNjaa
TANZIA: MBUNGE WA VITI MAALUM (CCM) AFARIKI DUNIA

Bunge la Tanzania limetangaza kuondokewa na Mbunge wa Viti Maalum, Irene Ndyamkama aliyefariki leo Aprili 24, 2022 akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Tumbi Mkoani Pwani

Soma - https://jamii.app/IreneMbunge
TUCHEL ATHIBITISHA RUDIGER KUONDOKA CHELSEA

- Kocha wa Chelsea, Thomas Tuchel amethibitisha beki wa timu hiyo, Antonio Rudiger ataondoka klabuni hapo baada ya mkataba wake kuisha mwisho wa msimu huu

- Inadaiwa Rudiger ameanza mazungumzo na Real Madrid ili kujiunga nayo

#JFSports
URUSI YAPELELEZA JESHI LA UINGEREZA KUISAIDIA UKRAINE

Inadaiwa Wanajeshi 20 wa Jeshi la Anga la Uingereza (SAS) walipelekwa Ukraine kwa Kazi Maalum

> Msemaji wa Jeshi la Uingereza alipoulizwa alisema "Hatuwezi kuzungumzia kuhusu SAS"

Soma - https://jamii.app/UingerezaUkraine
UCHAFUZI WA MAZINGIRA: Mgodi wa Barrick North Mara uliopo Mkoani Mara umetozwa faini ya Tsh. Bilioni 1 kwa uchafu wa mazingira

Ni baada ya bomba linalopitisha majitaka kupasuka na kutiririsha maji katika Mto Tigite unaomwaga maji yake Mto Mara

Soma - https://jamii.app/FainiMgodiMara
SIMBA YATOLEWA CAF KWA PENATI 4-3

Simba imekwama kuingia nusu fainali ya Kombe la Shirikisho baada ya kufungwa kwa penati 4-3 dhidi ya Orlando Pirates

Dakika 90 ziliisha kwa Orlando kushinda goli 1-0 hivyo matokeo ya jumla kuwa goli 1-1

Soma - https://jamii.app/SimbaYatolewaCAF

#JFSports #CAFCC
UCHAGUZI UFARANSA: MACRON AMSHINDA LE PEN

Ripoti zinaonesha Emmanuel Macron (44) ameongoza kwa kupata 58.6% ya Kura huku Mpinzani wake, Marine Le Pen (53) akipata Kura 41.4%

Anatarajiwa kutangazwa kuwa mshindi wa Urais leo Aprili 25, 2022

Soma - https://jamii.app/MarconUfaransa

#JFLeo
#SUDAN: Takribani watu 168 wameuawa na 98 kujeruhiwa Aprili 24, 2022 ktk mapigano kati ya Waarabu na wasio Waarabu Mjini #Darfur

> Kundi la Wanamgambo linaoungwa mkono na Serikali, maarufu kama #JanjaWeed linashutumiwa kwa mashambulizi hayo

Soma - https://jamii.app/mapiganoDarfur
Rais wa Uturuki, Recep Erdogan amesema Nchi yake tayari kusuluhisha mgogoro baina ya Ukraine na Urusi

> Amesema watatoa usaidizi unaohitajika katika mchakato wa majadiliano ya kumaliza vita ambayo imefikisha miezi mitatu

Soma - https://jamii.app/UturukiUkraine

#JamiiForums
UMUHIMU WA KUPIMA AFYA MARA KWA MARA

1) Huwezesha kujua hali yako kiafya: Mtu anakuwa na taarifa muhimu zitakazomsaidia kufanya maamuzi sahihi kuhakikisha ustawi wa Afya yake

2) Husaidia kubaini Magonjwa mapema: Utaratibu huu unaruhusu Madaktari kubaini viashiria vya Ugonjwa na kuchukua hatua haraka

Soma > https://jamii.app/KupimaAfya

#Afya
👍1
SIKU YA MALARIA DUNIANI

Ugonjwa wa #Malaria unaendelea kuathiri vibaya Afya na maisha ya watu duniani kote licha ya kuwa unazuilika na kutibika. Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Mtoto 1 hufariki dunia kwa Malaria kila dakika mbili

Wataalamu wanasema matumaini ya kutokomeza Malaria yapo juu zaidi baada ya Chanjo ya kwanza dhidi ya Ugonjwa huo kuidhinishwa

Soma - https://jamii.app/MalariaDay22

#EndMalaria #WorldMalariaDay
DODOMA: Spika wa Bunge la Tanzania, Dkt. Tulia Ackson ameahirisha shughuli za Bunge hadi April 27, 2022 kutokana na kifo cha Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Rukwa (CCM), Irene Alex Ndyamkama kilichotokea jana Aprili 24, 2022

Soma - https://jamii.app/ShughuliBunge

#JFLeo