JamiiForums
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
UKATILI WA KIUCHUMI: Ni aina ya unyanyasaji katika mahusiano ambao humfanya mtu kuwa tegemezi kwani anakosa sauti kwenye masuala ya Fedha

Kuzuiwa kufanya kazi na kutokuwa na maoni ktk maamuzi ya kifedha ni viashiria vya Ukatili huu

Soma - https://jamii.app/DomesticAbuse

#DomesticViolence
CAG: Kuanzia 2018/2019 hadi 2020/21 Ngorongoro ilipanga ndege ya CESSNA 182P yenye namba za usajili 5H-MPZ ifanye doria za ulinzi kwa saa 900, lakini ilifanya kwa saa 18 tu, huku Tsh. 278,420,000 zilitumika kwa matengenezo yake

Soma: https://jamii.app/CAGReport2022

#CAGReport2022
JE, WAJUA ZANZIBAR ILIWAHI KUWA CHINI YA MALKIA?

Mwaka 1696-1698 utawala wa Unguja uligawanyika na Mtawala wa Zanzibar Kaskazini alikuwa ni Malkia Fatuma binti Yusuf al-Alawi

> Wakati huo Wareno waliitaka Afrika Mashariki na Fatuma aliwasaidia

Soma https://jamii.app/ZnzFatuma
KAMALA HARRIS NA MARK ZUCKERBERG WAPIGWA MARUFUKU KUINGIA URUSI

Serikali ya Urusi imesema Makamu wa Rais wa Marekani, Mwanzilishi wa Facebook (Meta) pamoja na wengine 27 wamezuiwa kwa muda usiojulikana, ikiwa hatua ya kujibu vikwazo dhidi ya Urusi

Soma - https://jamii.app/USVPBanned
👍1
BENKI YA DUNIA: UVAMIZI NCHINI #UKRAINE UMESABABISHA HASARA YA DOLA BILIONI 60

Ni kutokana na uharibifu wa majengo na Miundombinu uliosababishwa na uvamizi uliofanywa na Urusi

Hasara hiyo inaweza kuongezeka kwani vita bado inaendelea

Soma - https://jamii.app/HasaraUkraine

#JFLeo
Rais Samia Suluhu akiwa na Ronald Fenty (Baba wa Rihanna) aliyefika Ukumbi wa Paramount Pictures kuangalia Filamu ya #RoyalTour

> Filamu hii inazinduliwa Los Angeles Aprili 21, 2022 baada ya uzinduzi wa New York uliofanyika Aprili 18, 2022

Soma https://jamii.app/SamiaNaBabaRihanna
CAG: Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa TANESCO unataka uunganishaji wa Mteja kwenye Laini ya Huduma ufanyike ndani ya siku 7 - 14 za kazi kulingana na umbali kutoka kwenye miundombinu iliyopo

> Kushindwa kufanya hivi, TANESCO inatakiwa kumlipa Mteja

Soma https://jamii.app/CAGReport2022
SIKU YA SAYARI DUNIA: Aprili 22 ni #EarthDay, Siku hii inaangazia umuhimu wa kutunza Sayari yetu na kuchukua hatua za kuiokoa

Kila mmoja anapaswa kuwajibika ili kupunguza changamoto zinazotokana na kupuuza athari za uharibifu wa mazingira

Soma zaidi > https://jamii.app/WorldEarthDay
Vikosi vya Israel leo Aprili 22, 2022 vimevamia Msikiti wa Al-Aqsa, Jerusalemu Mashariki na kuwajeruhi takriban Wapalestina 40, wakiwemo Waandishi wa Habari watatu

Soma - https://jamii.app/Uvamizimsikitini

#IsraelPalestineConflict
RAIS WA ZAMANI WA KENYA, MWAI KIBAKI AFARIKI DUNIA

Aliyekuwa Rais wa Kenya kuanzia Mwaka 2002 hadi 2013, Mwai Kibaki amefariki dunia akiwa na miaka 90

Kifo chake kimetangazwa na Rais Uhuru Kenyatta leo Aprili 22, 2022 Ikulu Jijini Nairobi

Soma - https://jamii.app/MwaiKibakiDead

#RIPKibaki
GABON: WATOTO WA RAIS OMAR BONGO WAFUNGULIWA MASHTAKA UFARANSA

Grace Bongo, Betty Bongo, Arthur Bongo na Hermine Bongo wanakabiliwa na tuhuma za ubadhirifu wa Fedha za Umma na Rushwa

Wamekana tuhuma hizo wakisema walipewa mali na Baba yao kama zawadi

Soma - https://jamii.app/FamiliaYaBongo
UKATILI WA KINGONO: Aina hii ya unyanyasaji katika Mahusiano inahusisha Mtu kulazimishwa kushiriki tendo hilo au masuala mengine yanayohusiana nalo

Wakati mwingine anayefanyiwa ukatili huu hutishiwa kuachwa anapokataa

Soma zaidi - https://jamii.app/DomesticAbuse

#DomesticViolence
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu akiwa Bungeni leo Aprili 22, 2022, amekanusha Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kutokuwa himilivu hata baada ya ripoti ya CAG kuonesha vinginevyo

> Adai ripoti hiyo iliishia Juni 2021

Soma - https://jamii.app/HifadhiyaJamii
TALIBAN YAPIGA MARUFUKU TIKTOK KWA KUPOTOSHA VIJANA

Serikali ya Taliban imeweka marufuku hiyo kwa madai kuwa 'App' maarufu ya #TikTok inasababisha Vijana Nchini #Afghanistan kupotea

Mchezo uitwao PUBG nao umepigwa marufuku

Soma - https://jamii.app/TikTokBan

#DigitalRights
TUNISIA: RAIS KAIS SAIED AINGILIA TUME YA UCHAGUZI, ATEUA WAJUMBE WAPYA

Kiongozi huyo ameendelea kujiimarishia Mamlaka baada ya kutoa amri ya kubadilisha Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi

Hatua hiyo inatarajiwa kuchochea upinzani zaidi dhidi yake

Soma - https://jamii.app/TumeUchaguziTun
MDAU: ELIMU NI SILAHA MUHIMU, LAKINI MAISHA HUANZA KWA KUTHUBUTU

Anasema Wasomi wamekuwa wengi hivyo Elimu isifanye Mtu abweteke na kukaa kusubiri Ajira rasmi

Anaongeza kuwa, ni muhimu kuangalia fursa zilizopo katika mazingira yanayotuzunguka

Msome - https://jamii.app/MdauElimuMaisha
MICHEZO: HARRY MAGUIRE ATISHIWA KIFO, APEWA SAA 72 KUONDOKA MAN. UNITED

Beki huyo ametishiwa na watu wasiojulikana baada ya Manchester United kufungwa 4-0 na #Liverpool

Watu hao walimwambia wametegesha mabomu matatu nyumbani kwake

Soma - https://jamii.app/MaguireVitisho

#JFSports
SOMALIA: MLIPUKO WAUA WATU 6 JIJINI MOGADISHU

Mlipuko ulitokea katika Mgahawa uliokuwa ukitumiwa na Askari Polisi na Wabunge. Hata hivyo, hakuna Mbunge aliyepoteza maisha

Mbali na vifo, Watu wengine saba wamejeruhiwa

Soma - https://jamii.app/MlipukoSomalia

#JFLeo
AFYA: 50% YA WANAOTOA MIMBA HAWATOI KATIKA NJIA SALAMA

Daktari Bingwa wa Masuala ya Mama na Mtoto, Dkt.Peter Kibacha anasema kuna wastani wa Mimba Milioni 1 zisizotarajiwa zinatungwa kwa mwaka Nchini, na kati ya hizo 39% huharibiwa kwa makusudi

Soma - https://jamii.app/UtoajiMimba
MTEJA ANA HAKI YA KUONA CHETI CHA MUUZA DUKA LA DAWA

Ukaguzi wa Wizara ya #Afya umebaini Wamiliki na watoa huduma wengi katika maduka ya dawa sio waaminifu

Vilevile, wapo wengine wanaohudumia wateja lakini hawana Elimu hiyo

Soma - https://jamii.app/DukaLaDawa

#JamiiForums