JamiiForums
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
CAG: Kati ya Juni 2020 hadi Juni 30, 2021 Bohari Kuu ya Dawa haikupeleka Dawa na Vifaa Tiba vyenye thamani ya Tsh. Bilioni 1.17 kwa Mamlaka 9 za Serikali za Mitaa

Kutopeleka bidhaa hizo kunaathiri ubora wa huduma za #Afya

Soma zaidi > https://jamii.app/CAGReport2022

#CAGReport2022
Ili kuweza kuona fursa hizi na nyingine nyingi za Ajira, tembelea > https://jamii.app/NafasiAjira

#JamiiForums
ELIMU BILA MALIPO: CAG ABAINI MAMLAKA 25 ZILIPATA FEDHA PUNGUFU

Ripoti ya 2020/21 inasema Ukaguzi umebaini Fedha za Ruzuku kwa Shule za Msingi na Sekondari zilitolewa pungufu kwa Tsh. 4,252,600,723 katika Mamlaka 25 za Serikali za Mitaa

Soma - https://jamii.app/CAGReport2022

#RipotiCAG
Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema Filamu ya #RoyalTour ambayo itazinduliwa Aprili 18, 2022 haijatumia fedha za Watanzania

> Pia, Rais Samia alisema gharama za kutengeneza filamu hiyo ni Tsh. bilioni 7

Soma - https://jamii.app/MsigwaUtalii

#JamiiForums
#CAGReport2022: Manispaa ya Temeke ililipa Bilioni 18.79 kama Malipo ya Fidia. Kati ya hizo, Tsh. Bilioni 2.16 zililipwa kwa Watu 94 Wasiotambuliwa na Serikali za Mitaa

Fidia hiyo ni ya ujenzi wa Miradi inayofadhiliwa kwa Fedha za Benki ya Dunia

Soma - https://jamii.app/CAGReport2022
WHO: MAAMBUKIZI NA VIFO VYA UVIKO-19 VIMEPUNGUA SANA AFRIKA

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema maambukizi ya #COVID19 yametoka 308,000 hadi chini ya 20,000 kwa wiki iliyopita huku vifo vikishuka kwa 29% na 37% ktk wiki za hivi karibuni

Soma - https://jamii.app/Covid-19Africa
#CAGReport2022: Kati ya Mei 2016 hadi Septemba 2021 ajali 1,107 zilitokea katika Miundombinu ya BRT

> Ajali hizo zilisababisha vifo vya Watu 50, Majeruhi 211 na uharibifu mkubwa wa mali

Soma: https://jamii.app/CAGReport2022
Tunawatakia wote Ijumaa Kuu njema na yenye Amani

#GoodFriday #Easter2022
Sanaa katika aina zake mbalimbali inaruhusu watu kujieleza. Pia, ina nafasi muhimu katika kutoa maarifa

Siku ya #Sanaa huadhimishwa ili kukuza ufahamu juu ya umuhimu wake katika maisha yetu ya kila siku

Je, Sanaa ina mchango gani kwako?

Soma - https://jamii.app/SikuYaSanaa

#WorldArtDay
CAG: MAJENGO MENGI YA SERIKALI NI HATARI KWA MAISHA YA WATU

#CAGReport2022 imebainisha majengo mengi ya #Serikali yamejengwa bila usanifu wa uokozi wa majanga ya moto

Kuna hatari ya kupoteza mali au maisha ya watu likitokea janga

Soma - https://jamii.app/CAGReport2022

#JamiiForums
#CAGReport2022: Serikali haijaanza uchimbaji wa Madini ya Tanzanite tangu ilipolitwaa eneo la Uchimbaji la Kitalu C, huko Mererani Mei 13, 2020

> Aidha, kuna njia haramu za uchimbaji katika eneo hilo bila ufahamu wa JWTZ

Soma - https://jamii.app/CAGReport2022
UNYANYASAJI/UKATILI KATIKA MAHUSIANO: Hii inaweza kuwa kwa vitendo vya kimwili, kingono, kihisia, kiuchumi au kisaikolojia

Unyanyasaji unaweza kutokea kwenye Ndoa, kwa watu ambao wanaishi pamoja au walio kwenye hatua za awali za uhusiano

Nini maoni yako kuhusu Unyanyasaji kwenye Mahusiano?

Soma - https://jamii.app/DomesticAbuse

#DomesticViolence
URUSI YATISHIA KUTUMIA NYUKLIA

Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Usalama, Dmitry Medvedev ambaye ni Mshirika wa karibu wa Putin ameonya #Russia itapeleka silaha za nyuklia na makombora ya masafa marefu Ulaya ikiwa Sweden na Finland zitajiunga na NATO

Soma - https://jamii.app/RussiaNuklia
CAG: WAFANYAKAZI 6 WAHUSIKA NA UBADHIRIFU WA TSH. BILIONI 3.9 BENKI KUU

Ubadhirifu huo ulitokana na mchakato wa kubadili Noti Chakavu ambapo Wafanyakazi 6 walihusika na mchezo huo uliofanyika Januari 2017 hadi Desemba 2019

Soma - https://jamii.app/CAGReport2022

#CAGReport2022
MDAU: ACHA KUTAMANI MAFANIKIO, ANZA HATUA ZA KUFIKIA MALENGO

Anasisitiza kuwa mwaminifu na kufanya kazi zako kwa ubora katika fursa unayoitumikia

Anasema, ongeza ujuzi na epuka mambo yanayokupotezea muda na kukukwamisha kufikia malengo uliyonayo

Msome - https://jamii.app/MalengoSOC
RAIS SAMIA AZUNGUMZA NA MAKAMU RAIS WA MAREKANI

Rais Samia Suluhu Hassan na Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris wamefanya mazungumzo hayo Ikulu ya Marekani - Washington DC

Rais Samia amesema Serikali ya Tanzania inathamini mchango mkubwa wa Marekani, akitoa wito kwa Serikali ya Nchi hiyo kuhimiza Sekta Binafsi kufanya kazi na Tanzania

Soma - https://jamii.app/SamiaKamalaIkulu

#JFLeo
Masuala kadhaa aliyozungumza Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa Ikulu ya Marekani - Washington DC

Soma zaidi > https://jamii.app/SamiaKamalaIkulu

#JFLeo
1
DAR: Polisi imewakamata Watuhumiwa 1,251 wa Makosa ya Usalama Barabarani na baadhi yao wamefikishwa Mahakamani huku wengine wakitozwa faini

> Makosa wanayokutwa nayo ni Mwendokasi, Kuendesha magari mabovu na Kutojali alama za barabarani

Soma https://jamii.app/MagariMabovuYakamatwa
1