JamiiForums
βœ”
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Saratani ni moja kati ya visababishi vikubwa vya vifo japokuwa inaweza kutibiwa. Kuchelewa kugundua Saratani inatajwa kuwa sababu kubwa inayochangia vifo

Kwa Tanzania, Saratani zinazoongoza ni pamoja na Saratani ya Mlango wa Kizazi kwa Wanawake, Saratani ya Matiti na Saratani ya Tezi Dume

Soma - https://jamii.app/CancerTZ

#Afya
SHINYANGA: Mkazi wa Ndala, Manispaa ya Shinyanga anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumnajisi mtoto wake wa kambo mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi 11 wakati Mama wa mtoto akiwa dukani

> Tukio hilo limetokea Aprili 9, 2022

Soma: https://jamii.app/AnajisiMtoto

#JFMatukio
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema idadi ya Watanzania wanaojisaidia vichakani imepungua kutoka 5.7% Mwaka 2017 hadi kufikia 1.4% Desemba 2021

> Amesema hayo leo, Aprili 11, 2022 kwenye Kilele cha Kampeni ya #NyumbaNiChoo

Soma: https://jamii.app/KujisaidiaVichakani

#Afya
ZITTO : WATU WAPO HURU, HAWAOGOPI KUZUNGUMZA

Kiongozi wa ACT-WAZALENDO, Zitto Kabwe amesema mazingira ya kisiasa Nchini Tanzania yamebadilika na sasa kuna Uhuru

> Asema kwa sasa, Watu wapo Huru kuzungumza, hawaogopi kutekwa wala kushtakiwa

Soma - https://jamii.app/ZittoUhuruUpo

#FreeSpeech
UPANDAJI BEI ZA BIDHAA: Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji amesema dunia imekumbwa na tatizo la mfumuko mkubwa wa bei

Kuhusu athari za vita kati ya Ukraine na Urusi hapa Nchini amesema, "Tanzania ilikuwa na mahusiano ya Kibiashara ya moja kwa moja kwenye Ngano, Mafuta ya Kula, Mbolea na Mafuta (Dizeli, Petroli na Mafuta ya Taa)"

Soma - https://jamii.app/UchumiBeiBidhaa
MWIGULU: TUTAPUNGUZA MAKALI YA MAISHA, LAKINI YAPO AMBAYO WATANZANIA WATALAZIMIKA KUYABEBA

Waziri wa Fedha asema "Tukisema tunataka tuchukue hatua za kumaliza tatizo ambalo sio la hapa kwetu, tunaweza tukaumaliza Uchumi wetu na kuingia ktk matatizo"

Soma https://jamii.app/UchumiBeiBidhaa
KILIMANJARO: Bazara la Madiwani Manispaa ya Moshi Mjini Aprili 11, 2022 limemng’oa Meya wa Manispaa hiyo, Juma Raibu kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo kuunga mkono ushoga

> Inadaiwa mwezi Februari alikuwa Mgeni Rasmi kwny sherehe ya kuzaliwa ya mmoja wao

Soma https://jamii.app/MeyaMoshi
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Deogratius Ndejembi amesema Watumishi wa Umma 1,477 wamesimamishwa kazi 2015-2022 kwa kukiuka Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo

> Amesema hayo leo Aprili 11, 2022 Bungeni, Dodoma

Soma - https://jamii.app/WasimamishwaKazi
UFARANSA: Rais Emmanuel Macron ameongoza kwenye duru la kwanza la Uchaguzi Mkuu wa Rais nchini humo kwa kumshinda Mpinzani wake Mkuu, Marine Le Pen na wawili hao watakutana katika duru ya pili ambayo ni ya mwisho Aprili 24, 2022

Soma - https://jamii.app/UchaguziUfaransa
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza kushushwa kwa Kodi ya Sukari inayoingizwa Nchini kwa kiwango kisichopungua 10% kwa muda huu ambapo kuna ongezeko la bei za bidhaa

Soma https://jamii.app/UchumiBeiBidhaa

#JamiiForums
PAKISTAN: Bunge limemchagua #ShahbazSharif kuwa Waziri Mkuu mpya wa nchi hiyo, baada ya #ImranKhan kuondolewa madarakani kwa Kura ya Kutokuwa na Imani naye jana, Aprili 10, 2022

> Shahbaz Sharif anakuwa Waziri Mkuu wa 23 wa Nchi hiyo

Soma: https://jamii.app/PakistanWaziriMkuu
TMA imetoa tahadhali ya uwepo wa mvua kubwa ktk Mwambao wa Bahari ya Hindi kuanzia Aprili 12-14, 2022 kwa Zanzibar na Mikoa ya Dar, Pwani, Mtwara, Lindi

> Madhara yanayoweza tokea ni makazi kujaa maji na kuathirika kwa shughuli za Uchumi

Soma - https://jamii.app/PwaniMvuaKubwa
MWIGULU: BEI ZA MAFUTA YA GARI NA YA KUPIKIA ZITAPUNGUZWA

Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Timu ya Wataalamu itakaa ndani ya wiki moja kisha itakuja na majibu kujua jinsi ya kuchukua hatua za kupunguza bei ya Mafuta ya Gari

Soma - https://jamii.app/UchumiBeiBidhaa
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) imepitisha kuwa Mkutano Mkuu wa 44 wa Kawaida wa CAF utafanyika Agosti 10, 2022 Jijini Arusha, Tanzania

> Katibu Mkuu wa CAF, Veron Mosengo-Omba ametoa taarifa hiyo

Soma - https://jamii.app/CAFArusha

#JamiiForums #JFSports
UFILIPINO: MVUA YAUA TAKRIBAN WATU 25

Mvua kubwa imesababisha maporomoko ya ardhi Katikati na Kusini mwa Nchi hiyo

> Takriban matukio 200 ya mafuriko yaliripotiwa katika maeneo tofauti ya Majimbo ya Kati na Kusini mwishoni mwa wiki iliyopita

Soma - https://jamii.app/MvuaVifo25

#JFLeo
URUSI YAZIONYA FINLAND NA SWEDEN KUJIUNGA NATO

Msemaji wa Kremlin amesema muungano huo unabaki kuwa kama 'chombo kinacholenga makabiliano'

> Ikulu ya Marekani inaunga mkono mpango huo huku ikiamini nchi hizo zitaomba Uanachama Juni, 2022

Soma - https://jamii.app/FinlandSwedenNato
UTAFITI: MTU 1 KATI YA 6 DUNIANI HUUMWA KICHWA

Inaelezwa, maumivu ya kichwa huweza kusababishwa na vitu mbalimbali ikiwemo matatizo ya kulala na Msongo wa Mawazo

Je, wewe ni miongoni mwa watu wanaoumwa kichwa mara kwa mara?

Soma - https://jamii.app/AfyaKichwa

#Afya
Kesi inayomkabili aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini #JacobZuma imeahirishwa kusubiri matokeo ya rufaa ya kutaka Mwendesha Mashtaka wa Serikali aondolewe kwenye kesi hiyo

> Zuma anakabiliwa na mashtaka 18 ikiwemo Ufisadi na Utakatishaji fedha

Soma: https://jamii.app/KesiYaZuma
WAKAGUZI WA MAGARI WALIOZUIWA KENYA WAOMBA TENDA TANZANIA

Ni Kampuni za Auto Terminal Japan Limited na EAA Automobiles Services

> Mwaka 2021, zilifungiwa kufanya kazi hiyo Kenya na Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma Kenya kwa Kughushi Nyaraka

Soma - https://jamii.app/TendaYaMagari
Baada ya Mkuu wa Mkoa wa zamani wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuandika mtandaoni kuwa kuna Makundi Matano yanamuwinda ili kumuua, Jeshi la Polisi limesema kama kweli ana hofu anatakiwa aende kutoa taarifa Kituo cha Polisi

Soma - https://jamii.app/PolisiMakonda

#JamiiForums