JamiiForums
βœ”
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
#KENYA: Wizara ya Afya imetangaza ongezeko kubwa la maambukizi ya #UKIMWI ambapo Watoto wa Kike 98 wenye Miaka 10 hadi 19 huambukizwa VVU kila wiki

Januari - Februari, Wasichana 45,724 wamekutwa na Mimba huku 2,196 wakikumbana na Unyanyasaji

Soma - https://jamii.app/VVUWatotoKE

#Afya
πŸ‘1
ALIYESHIRIKISHWA β€˜EKWUEME’ AFARIKI DUNIA

Mwanamuziki wa Nyimbo za Injili wa Nigeria, Osinachi Nwachukwu aliyepata umaarufu kupitia wimbo wa #Ekwueme amefariki dunia

> Amefariki Aprili 8, 2022 baada ya kupambana na ugonjwa kwa muda mrefu

Soma - https://jamii.app/EkwuemeDeath
ELIMU: Imebainika zaidi ya asilimia 90 ya Watoto walio Mitaani Jijini Mwanza wana umri wa kwenda Shuleni

Kuanzia Januari - Aprili 2022 kuna Wanafunzi watoro 19,133 ktk Shule za Msingi huku za Sekondari Wanafunzi watoro wakiwa ni 7,594

Soma - https://jamii.app/UtoroShuleni

#HakiMtoto
MBUNGE: TUME ILIYOKWENDA MTO MARA ICHUNGUZWE

Kasalali Mageni amesema Wataalamu wengi wana mazingira ya rushwa akisisitiza, "Nchi hii haiwezi kula Ripoti ya kupikwa"

Asema Uchunguzi unahitajika kufahamu chanzo cha Magonjwa ya Saratani Kanda ya Ziwa

Soma - https://jamii.app/TumeMtoMara

#JFLeo
πŸ‘1
MWANZA: Walimu 250 wa Wilaya ya Nyamagana wadaiwa kuandamana kudai posho za kazi ya kuweka Alama za Anwani za Makazi waliyoifanya kwa siku tano

> Inaelezwa kuwa, kila Mtumishi anadai Tsh. 100,000 ambayo ndio malipo ya siku tano

Soma - https://jamii.app/MwanzaWalimu

#JamiiForums
Rais Samia Suluhu Hassan amechaguliwa kuwa mshindi wa Tuzo ya Africa Road Builders–Babacar Ndiaye Trophy Mwaka 2022

Tuzo hiyo hutolewa kwa Watu mashuhuri Afrika ambao wameonesha dhamira ya kuendeleza Sekta ya Miundombinu ya usafiri Barani

Soma - https://jamii.app/SamiaNdiayeTuzo
#JFLeo
#PAKISTAN: WAZIRI MKUU, IMRAN KHAN AONDOLEWA MADARAKANI

Ni baada ya Bunge kupiga Kura ya kutokuwa na Imani naye

Khan anakuwa Waziri Mkuu wa kwanza kuondolewa kwa Kura ya kutokuwa na imani naye

Waziri Mkuu mpya kuchaguliwa Aprili 11, 2022

Soma - https://jamii.app/ImranKhanOut

#JFLeo
Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imesema ni kosa kisheria kuvuta sigara hadharani au kwenye maeneo ya mikusanyiko

> Faini yake ni Tsh. 200,000 au kifungo miezi 6 jela

Soma > https://jamii.app/FainiSigara

#JamiiForums
UGANDA: Rais Yoweri #Museveni amewataka Polisi kuwakamata wanaoandika kuwa Spika Jacob #Oulanyah amefariki kwa kupewa sumu

> Aidha, Naibu M/Kiti wa Chama cha NRM amesema Jacob alimjulisha kuwa alipewa sumu baada ya kushinda Uspika

Soma - https://jamii.app/SpikaSumuUganda
RONALDO AOMBA RADHI BAADA YA KUVUNJA SIMU YA SHABIKI WA EVERTON

Imetokea Aprili 9, 2022 baada ya Man. United kufungwa bao 1-0 na Everton ktk Uwanja wa Goodison Park

> Shabiki alimpiga Ronaldo picha wakati akirejea vyumbani baada ya mchezo

Soma - https://jamii.app/CR7AvunjaSimu

#JFSports
BEN AFFLECK AMCHUMBIA TENA JENNIFER LOPEZ

Mwanamuziki, Jennifer #Lopez na Muigizaji, Ben Affleck wametangaza kuwa wachumba baada ya Ben kumvalisha pete Jennifer

Wawili hao walirudiana 2021 baada ya uchumba wao wa awali kuvunjika 2004

Soma - https://jamii.app/JloBenPete
Shirika la Afya Duniani limesema mbili ya tatu ya watu waliopo Afrika wameambukizwa COVID-19 ndani ya miaka miwili, ikiwa ni mara 97 ya takwimu zilizoripotiwa na Mamlaka husika

> Nchi iliyoripoti maambukizi mengi Afrika ni Afrika Kusini

Soma - https://jamii.app/Uviko-19Afrika
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema magari yaliyotengenezwa chini ya mwaka 2010 yasiingizwe nchini

> Aidha, Waziri Mkuu ameiambia #TBS kuwa ina wajibu wa kujiridhisha na kuelimisha wanaoagiza magari

Soma - https://jamii.app/MagariBandarini

#JamiiForums
LIGI KUU: SIMBA SC YAAMBULIA POINTI MOJA KWA POLISI TANZANIA

Simba imepata pointi moja kwa matokeo ya 0-0 dhidi ya Polisi Tanzania, katika Uwanja wa Ushirika Moshi

Kocha wa Simba, Pablo Franco amesema uwanja haukuwa mzuri

Soma - https://jamii.app/PolisiSimba

#JamiiForums #Sports
#UKRAINE: UCHUMI KUPOROMOKA KWA 45.1% KUTOKANA NA VITA

Benki ya Dunia inasema uvamizi wa Urusi umelazimisha biashara kufungwa na kupunguza mauzo ya nje

Pato la Taifa la #Russia Mwaka 2022 linatarajiwa kushuka kwa 11.2% kutokana na vikwazo

Soma - https://jamii.app/VitaUchumiUkr

#JFLeo
JE, UNAJUA NINI KINACHELEWESHA UPATIKANAJI WA VITAMBULISHO VYA TAIFA?

Ripoti ya Ukaguzi wa CAG Mwaka 2019/20, ilionesha zoezi la usajili na utoaji Vitambulisho vya Taifa linaathiriwa na uchapaji mdogo wa vitambulisho ikilinganishwa na wingi wa Wananchi walioandikishwa

#JFUwajibikaji #WAJIBU #Accountability
GWAJIMA: DIRA YA TAIFA INAHITAJIKA KUEPUSHA KILA RAIS KUANZA NA LAKE

Mbunge wa Kawe amesema Dira ni muhimu ili Rais anayeingia Madarakani asimamie maono ya Nchi na si yake binafsi

Asema hakuna Nchi inayoweza kuendelea ndani ya Utawala mmoja

Soma - https://jamii.app/TZDiraTaifa
BONDIA MWAKINYO AVULIWA MKANDA WA ABU

Baada ya Bondia Hassan Mwakinyo kuvuliwa Mkanda wa Ubingwa wa Mabara wa WBF, sasa amevuliwa Mkanda wa Ubingwa wa Afika (ABU)

> Sababu ni kwa kuwa hajapigana kuitetea ndani ya miezi sita

Soma > https://jamii.app/MwakinyoMikanda

#JamiiForums #JFSports
Balozi wa Marekani Nchini Tanzania, Donald J. Wright amesema Upinzani wa Kisiasa ukiwa imara ni jambo jema kwenye Afya ya Demokrasia

> Amesema hayo leo Aprili 11, 2022 alipokutana na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe

Soma - https://jamii.app/MboweUSA

#JamiiForums #Demokrasia
πŸ‘1
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Saratani ni moja kati ya visababishi vikubwa vya vifo japokuwa inaweza kutibiwa. Kuchelewa kugundua Saratani inatajwa kuwa sababu kubwa inayochangia vifo

Kwa Tanzania, Saratani zinazoongoza ni pamoja na Saratani ya Mlango wa Kizazi kwa Wanawake, Saratani ya Matiti na Saratani ya Tezi Dume

Soma - https://jamii.app/CancerTZ

#Afya