JamiiForums
βœ”
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Rais Samia: Tozo ya Tsh. 100 iliyokuwa imeondolewa kwenye mafuta irejeshwe kwa sababu hesabu zake tayari zilikuwa zimepigiwa kwenye bajeti

> Kwa mwenendo wa upandaji wa Bei ya Mafuta Duniani, kuondoa tozo hiyo ni kuikosesha Serikali mapato

Soma - https://jamii.app/Tozo

#JamiiForums
Rais Samia: Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani bado hakiko vizuri, ndio sababu ya CAG kukutana na matatizo mengi

> Baadhi ya Wakaguzi wa Ndani hushirikiana na Watu wa Manunuzi ili kujua mbinu za kuchepusha fedha za Serikali

Soma https://jamii.app/InternalAudits

#JamiiForums #RipotiYaCAG #CAG
DR-CONGO: Waasi wa M23 waiangusha Helkopta ya Umoja wa Mataifa Wilayani Rutshuru-Kivu Kaskazini na kusababisha vifo vya Wanajeshi Walinda Amani 8

> M23 wamelilaumu Jeshi la DRC kwa kuwashambulia ndipo wao walipojibu wakaiangusha helkopta hiyo

Soma https://jamii.app/WalindaAmani
TAKUKURU: Kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka tumetaifisha mali zenye thamani ya Tsh. bilioni 1.2, tumeweka zuio la fedha kiasi cha Tsh. milioni 495.5 na mali zenye thamani ya Tsh. bilioni 2.6

> Pia, tumefanikiwa kuokoa Tsh. bilioni 29.3

Soma https://jamii.app/Takukuru
NAIBU WAZIRI (KATIBA NA SHERIA): Watanzania waipe muda Katiba iliyopo iangaliwe maeneo yanayokera ili iimarishwe, haina tatizo lolote isipokuwa wanaoitafsiri hutoa maana tofauti

> Amesema Katiba hii ni kama Kitabu cha Dini, kila mmoja anatafsiri yake

Soma https://jamii.app/Katiba
MDAU: NAMNA YA KUKUZA TABIA YA KUPENDA KUSOMA KWA MTOTO

1. Panga Ratiba ya kusoma na Mtoto wako kila siku. Endapo mtasoma pamoja, Mtoto ataona kusoma kuna umuhimu

2. Mnapotaka kusoma, shirikiana na Mtoto kuchagua vitabu. Msomee Mtoto kwa sauti huku ukimwonesha unapopasoma. Hii itamsaidia kujifunza maneno mapya kirahisi na kuyakumbuka

Soma - https://jamii.app/KusomaMtoto
#Malezi
TANZIA: Balozi Emmanuel Ole-Naiko amefariki dunia, leo Machi 30, 2022 nyumbani kwake Bahari Beach Dar es Salaam

Ole-Naiko amewahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kituo Cha Uwekezaji (TIC), amefariki akiwa Balozi wa Heshima wa #Botswana nchini #Tanzania

Soma https://jamii.app/BaloziOleNaiko
UKRAINE: Gavana wa Chernihiv, Viacheslav Chaus asema Urusi haijalegeza mashambulizi dhidi ya Ukraine licha ya ahadi ya amani iliyotolewa

> Awali, Naibu Waziri wa Ulinzi wa Urusi alisema nchi hiyo itapunguza kwa kiasi kikubwa mashambulizi

Soma: https://jamii.app/UrusiMashambulizi
TUNISIA: Rais Kais Saied amelivunja Bunge la Nchi hiyo kwa madai ya kulinda Nchi na amesema kuwa Wabunge watafunguliwa mashtaka kwa kujaribu kufanya mapinduzi

> Wabunge walifanya kikao kupitisha Muswada kupinga Rais huyo kujiongzea Mamlaka

Soma https://jamii.app/TunisiaRais
DR-CONGO: Wabunge wamepiga kura za kumuondoa madarakani Waziri wa Uchumi, Jean Marie Kalumba kwa tuhuma za uratibu mbovu wa Sekta ya Uvuvi, Mfumuko wa Bei wa bidhaa muhimu na Uhaba wa Petroli

> Kalumba aliteuliwa kwenye wadhifa huo mwaka 2021

Soma https://jamii.app/WaziriDRC
VAN NISTELROOY AWA KOCHA MPYA PSV

- Ruud Van Nistelrooy (45) ametangazwa kuwa Kocha wa Klabu ya PSV Eindhoven kuanzia msimu wa 2022/23, akisaini mkataba wa miaka 3

- Alistaafu kucheza soka mwaka 2012 baada ya kutumikia Klabu za PSV, Manchester United na Real Madrid

#JFSports
#IRAQ: BUNGE LASHINDWA KUCHAGUA RAIS KWA MARA YA TATU MFULULIZO

Ni Wabunge 178 pekee kati ya 329 waliokuwepo ikiwa ni idadi isiyofika theluthi mbili inayohitajika

Wabunge lazima wamchague Mkuu wa Nchi, na lazima atoke Jamii ya Wakurdi

Soma - https://jamii.app/RaisIraqMkwamo
#Democracy
#Ujerumani ambayo ni mnunuzi mkubwa wa Mafuta na Gesi kutoka #Urusi imetangaza mgao wa bidhaa hizo kwa raia wake na imesema inaweza kuacha kuagiza mafuta kutoka Urusi

> Kuanzia Machi 31, 2022, Urusi itaanza kuuza mafuta kwa fedha yake (Ruble)

Soma https://jamii.app/MgaoWaMafuta
Mapungufu yaliyobainishwa ktk utekelezaji wa Miradi kwa utaratibu wa β€œForce Account” yamepelekea Kukosekana kwa thamani ya Fedha ktk miradi

Mfano; Majengo kupata nyufa muda mfupi baada ya kukamilika ikiwemo Shule za Sekondari Berege na Mazae

#JamiiForums #Accountability #WAJIBU
ARUSHA: Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, imepanga kuwa Mei 31, 2022 itatoa hukumu ya Kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake 6

> Kesi hiyo itatajwa Aprili 13, 2022 kabla ya hukumu

Soma - https://jamii.app/SabayaKesiArusha
PHILIP MANGULA ANG'ATUKA, KINANA ACHUKUA NAFASI

Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Philip Mangula ameachia wadhifa wake alioushika tangu Novemba 13, 2012

> Nafasi yake imechukuliwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulrahman Kinana

Soma https://jamii.app/MangulaAngatuka
BURUNDI: BBC YAREJESHEWA KIBALI CHA UTANGAZAJI MIAKA 3 BAADAYE

Sauti ya America pamoja na BBC zilisimamishwa wiki mbili kabla ya Kura ya Maoni ya Marekebisho #Katiba ili kumruhusu Rais wa zamani, Pierre Nkurunziza kuongoza hadi 2034

Soma - https://jamii.app/BBCBurundi
#MediaFreedom
❀1
MAREKANI NA UINGEREZA: Wanaompotosha Rais wa Urusi, Vladimir Putin ni washauri ambao wanahofu ya kumwambia ukweli jinsi vita na Ukraine itakavyofanya Urusi kuwa dhaifu muda mrefu

Soma - https://jamii.app/RussiaUkraineUS

#JamiiForums #RussiaUkraine
IRINGA: Kitengo cha Usalama Barabarani Mkoani humo kimepiga marufuku Watoto chini ya umri wa Miaka 9 kupanda Bodaboda

Imeelezwa Wazazi na Walezi ndio wanaoongoza kuwapakia Watoto kwenye usafiri huo wakati wa kwenda na kurudi Shuleni

Soma - https://jamii.app/WttPikpikIringa
#ChildSafety
MAHAKAMANI: Diana Bundala 'Mfalme Zumaridi' na wenzake 83 wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mwanza kwaajili ya kusomewa maelezo ya awali ya mashtaka yanayowakabili

> #Zumaridi amekosa dhamana sababu ya aina ya kesi yake huku wenzake 7 wakipata

Soma > https://jamii.app/ZumaidiDhamana