JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Kauli za Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu #Katiba na Tume Huru ya Uchaguzi

#Demokrasia #Democracy #JamiiForums
Bunge la #Pakistan kukutana ili kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu, Imran Khan aliyeingia madarakani 2018

Mapema mwezi huu Muungano wa Vyama vya Upinzani uliwasilisha hoja ukisema Khan amepoteza idadi kubwa ya uungwaji mkono #Bungeni

Soma https://jamii.app/KuraImanPakistan
#JFLeo
Ili kuweza kutuma Maombi ya nafasi hizi tembelea - https://jamii.app/NafasiAjira

#JamiiForums
TANAPA YATANGAZA KIFO CHA FARU RAJABU (MTOTO WA FARU JOHN)

Imetangazwa kifo cha Faru Rajabu (43) leo Machi 21, 2022 katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti chanzo kikitajwa ni uzee

Rajabu alikuwa Mtoto wa Faru John aliyekufa Mwaka 2015

Soma > https://jamii.app/FaruRajabu

#JamiiForums
Chombo cha Habari cha #China (CCTV) kimeripoti kuanguka kwa Ndege ya #Boeing737 ktk Milima ya #Guangxi na kuwaka Moto

Ndege hiyo ilikuwa na Abiria wapatao 133. Bado haijajulikana madhara yaliyotokana na ajali hiyo

Soma - https://jamii.app/Boeing737Crash
#JFLeo
CAG alibaini Mamlaka za Maji 21 kati ya 23 zina kiwango kikubwa cha upotevu wa Maji ikilinganishwa na kiwango kinachokubalika kisichozidi 20% kutokana na Miundombinu chakavu

Mwaka 2019/20, upotevu wa Maji ulikuwa wa Tsh. Bilioni 74.29 sawa na 47% ikilinganishwa na Mwaka 2018/19 ambapo ulikuwa Tsh. Bilioni 65.45 sawa na 42%

#JamiiForums #Accountability #JFUwajibikaji #WAJIBU
IRINGA: Mtoto (miaka 15) anayetuhumiwa kuwalawiti watoto (miaka 4-14) anatarajiwa kufikishwa Mahakamani wiki hii

> Mtuhumiwa anadaiwa kuwarubuni watoto wenzake kwa kuwapa pipi na pesa, kisha kuwaruhusu kuangalia Televisheni na ndipo alitimiza azma yake

Soma > https://jamii.app/Iringa
UTAFITI: Shirika la Utafiti wa Jiolojia la Uingereza (BGS) limebaini Afrika ina maji chini ya ardhi yanayoweza tumika hadi miaka 50 ijayo

> Hayo yamesemwa katika mkesha wa kuamkia Machi 22 ambayo ni Siku ya Maji Duniani

Soma https://jamii.app/UndergroundWater
UINGEREZA YAPONGEZA UHURU WA HABARI TANZANIA

Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania asema Uingereza imeridhishwa na uimarikaji wa hali ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Tanzania

Pia, asema ushirikishwaji wa demokrasia ya Vyama vya Upinzani ni matumaini mema

Soma > https://jamii.app/UKTZ
MACHI 22: SIKU YA MAJI DUNIANI

Takwimu zinaonesha Mtu 1 kati ya 3 anaishi bila Maji salama ya kunywa huku Watu bilioni 2.2 wanaishi bila kupata Maji salama

Ifikapo 2025, nusu ya Watu Duniani wataishi ktk maeneo yenye uhaba wa Maji

Soma https://jamii.app/WaterDay22
#WoldWaterDay2022
Idara ya Taifa ya kusimamia Maafa haikuweza kutumia Tsh. Bilioni 4.31 ambazo zilichangwa na Wadau mbalimbali ili kukabiliana na janga la #CoronaVirus kwa kuwa haikupata maelekezo kutoka Mamlaka zinazohusika

#JamiiForums #Accountability #JFUwajibikaji #WAJIBU
Ili kuweza kutuma Maombi ya nafasi hizi tembelea - https://jamii.app/NafasiAjira

#JamiiForums
URUSI: MAHAKAMA YASITISHA SHUGHULI ZA FACEBOOK NA INSTAGRAM

Ofisi ya Mwendesha Mashtaka imesema kumekuwa na machapisho makali kwenye Mitandao hiyo ya Kijamii, yakitoa wito wa vurugu dhidi ya raia wa Urusi na Wanajeshi wake walioko #Ukraine

Soma https://jamii.app/FBIGBanRussia
#DigitalRights
Waziri wa Utamaduni, #Sanaa na #Michezo, Mohamed Mchengerwa amelitaka BASATA kuwaita Viongozi wa Shirikisho la Muziki kushughulikia mgogoro unaoendelea baada ya Steven Mengele (Steve Nyerere) kuteuliwa kuwa Msemaji

Aidha, Steve amesema hawezi kujiuzulu nafasi hiyo bila utaratibu au kutokana na mashinikizo kutoka kwa Wasanii

Soma - https://jamii.app/BasataVsSteve