JamiiForums
βœ”
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Balozi wa Marekani Umoja wa Mataifa (UN), Linda Thomas-Greenfield amesema mzozo kati ya Urusi na #Ukraine sio Vita Baridi hivyo Nchi za Afrika haziwezi kubaki kati kwa kutounga mkono upande wowote

Asema hakuna Msingi wa kutoegemea upande wowote

Soma - https://jamii.app/UpandeAfrika
MBOWE: HAKI HAITAWALI, VINAVYOTAWALA NI SHERIA NA KATIBA

M/kiti wa CHADEMA Taifa amesema Haki ni mkusanyiko wa vitu vingi vinavyowekewa utaratibu ktk Nchi

Ameongeza "Tutapambana kuhakikisha tunaipata #Katiba, hii ni ajenda ya CHADEMA”

Soma - https://jamii.app/MbowePress
#Democracy
RAIS SAMIA: KAULI YANGU HAIATHIRI MAAMUZI YA MAHAKAMA

Akihojiwa na BBC Swahili, amesema kauli aliyowahi kuitoa kuhusu Kesi iliyokuwa inakabili Freeman Mbowe haikuathiri maamuzi ya Mahakama

Amesema kesi hiyo haijatia doa Utawala wake

Soma - https://jamii.app/AthariKauli
#JFLeo
MDAU: JAMII KUTOWAJALI WANAUME HUSABABISHA KUNDI HILI KUFARIKI MAPEMA

Anasema licha ya uchache wa Wanaume kiidadi katika Sensa, bado wanatangulia kufariki zaidi na kuacha Wake zao wakihangaika na Watoto

Anasema inachangiwa na Jamii kutowajali sana Wanaume. Asasi nyingi huhangaika na masuala ya Wanawake. Kesi za Wanaume kunyanyaswa hazisikilizwi kwa kutiliwa maanani kama za Wanawake na Watoto

Soma - https://jamii.app/WanaumeIssues
#GenderEquity
VITA YA URUSI NA #UKRAINE: Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) inapanga kuchangisha Dola Bilioni 1 (sawa na Tsh. Trilioni 2.3) ili kupambana na uhaba wa chakula unaotokana na vita hiyo

Nchi nyingi Afrika zinategemea Urusi na Ukraine kupata chakula

Soma - https://jamii.app/AfrikaChakula
MDAU: NGUZO YA KWANZA KWENYE MTAJI WA MAFANIKIO NI AFYA NJEMA

Anasema neno #Afya njema si tu kutokuwepo kwa Magonjwa au udhaifu wa Mwili, bali pia kuwa na Jamii safi, salama na inayostawi

Afya njema ni uhusiano mwema na Mwili wako kwa kuupa unachostahili. Mtu asiyeona umuhimu wa Afya yake ni sawa na asiyejali Gari lake

Msome - https://jamii.app/AfyaMafanikio
#HealthCare
πŸ‘1
Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, David Cameron anaendesha lori kuelekea Nchini Poland ili kutoa msaada kwa wakimbizi wa #Ukraine

Miongoni mwa misaada inayotarajiwa kutolewa ni pamoja na nguo, nepi na mahitaji ya huduma ya kwanza

Soma > https://jamii.app/UKUkraine

#JamiiForums
RAIS SAMIA: TUTAFANYA MABADILIKO POLISI

Amesema mapendekezo yaliyotolewa na Tume zilizoundwa kuchunguza matukio ya Jeshi la Polisi yataleta mabadiliko kidogo ndani ya Jeshi hilo

Rais Samia ameeleza hayo wakati akihojiwa na MCL

Soma > https://jamii.app/SamiaPolice

#JamiiForums
Wizara ya Mambo ya Nje ya #Bulgaria imesema Wanadiplomasia 10 wa Urusi hawahitajiki tena na kuwapa Saa 72 kuondoka

Hii ni mara ya pili kwa Wanadiplomasia wa Urusi kuamriwa kuondoka Bulgaria. Wengine wawili walifukuzwa Machi 2

Soma - https://jamii.app/BulgariaBanRussia
#RussiaUkraineWar
KIGOMA: MAJAMBAZI WAUA MFANYABIASHARA NA KUPORA FEDHA

Daglas Kinungunyi, Mfanyabiashara na Mkazi wa Nyamidaho Wilayani Kasulu ameuawa kwa kupigwa risasi Mkono wa kulia na kwenye Nyonga kisha kuporwa Fedha ambazo hazijajulikana kiasi chake

Soma - https://jamii.app/MajambaziKasulu
#JFLeo
BIDEN AIONYA CHINA KUHUSU KUISAIDIA URUSI

Rais wa #Marekani, Joe Biden amemuonya Rais wa #China, Xi Jinping ikiwa wataisaidia vifaa vya kivita #Urusi

> Aidha, Rais Xi ametoa wito kwa NATO kuzungumza na Urusi ili kuondoa mzizi wa mgogoro uliopo

Soma https://jamii.app/ChinaUrusi
BRAZIL: TELEGRAM YAZUILIWA KWA KUTOFUATA SHERIA

Mahakama Kuu imezuia matumizi ya Telegram baada ya kutofuata Sheria inayotaka udhibiti wa taarifa zisizo sahihi

#Telegram inatumiwa sana na Rais Jair Bolsonaro na wafuasi wake

Soma - https://jamii.app/TelegramBrazil

#DigitalRights
KAMATI: KINYESI NA MIKOJO YA MIFUGO VILISABABISHA VIFO VYA SAMAKI MTO MARA

Kamati imebaini uwepo wa kinyesi cha ng'ombe tani milioni 1.8 na mkojo lita bilioni 1.5

> Hali hiyo imebadilisha rangi ya maji, harufu na samaki kufa kwa kukosa Oksijeni

Soma https://jamii.app/MtoKinyesi
UKRAINE: Wanajeshi wa Urusi wameripotiwa kuingia katika Mji wa #Mariupol na kupelekea kufungwa kwa Kampuni kuu ya chuma cha Pua

Afisa wa Polisi wa Mariupol amesema Watoto na Wazee wanafariki zaidi kutokana na mashambulizi

Soma - https://jamii.app/RussiaMauripol
#RussiaUkraineWar
UNICEF: 4% YA WATOTO WALIO MTANDAONI WALIFANYIWA UNYANYASAJI MWAKA 2021

Utafiti umeonesha Watoto wa miaka 12 - 17 wamekuwa wakitumiwa ujumbe wa vitisho au kutakiwa kushiriki ngono kwa malipo

Picha zao za utupu zilisambazwa mitandaoni bila ruhusa

Soma - https://jamii.app/OnlineChildren
VIFO VYA SAMAKI MTO MARA: MDAU ACHAMBUA RIPOTI ZINAZOKINZANA

Anasema, "Ikitokea Samaki wengi wamekufa ndani ya muda mfupi kuna tatizo. Kuhusu Maji kubadilika rangi hoja ya wingi wa Mafuta ingeeleweka, kinyesi na mkojo ni ngumu kubadilisha rangi"

Msome - https://jamii.app/Mara
RAIS ZELENSKY: KUSHINDWA KWA MAZUNGUMZO KUTAMAANISHA VITA YA 3 YA DUNIA

Rais wa #Ukraine, Volodymyr Zelensky amesema yuko tayari kwa mazungumzo ila hatokubali kutambua maeneo yanayojitenga

Amesema wangekuwa Wanachama wa NATO vita isingeanza

Soma https://jamii.app/MazungumzoUkraine
#JFLeo
#UKRAINE: Shirika la wakimbizi Duniani (UNHCR) limesema Watu milioni 10 wamekimbia kutokana na vita

90% ya waliokimbia ni Wanawake na Watoto. Watoto milioni 1.5 wako hatarini kukabiliwa na biashara haramu ya usafirishaji Binadamu

Soma - https://jamii.app/Refugees10MUkraine
#RussiaUkraineWar
JE, WAJUA? - Nyoka aina ya Koboko (Black Mamba) wana uwezo wa kurefuka hadi kufikia futi 14. Ndiyo Nyoka mrefu kuliko Nyoka wote wenye sumu Barani Afrika

Anakimbia kwa kasi kuliko Nyoka wote Duniani (20km/h). Akiwa na hasira ana uwezo wa kuinua moja ya tatu (1/3) ya Mwili wake

Soma zaidi - https://jamii.app/BlackMamba
#WildLife #Animals
Mtaalamu wa Afya ya Umma, Dkt. Katanta Simwanza amewashauriwa Wanawake kuacha kuweka ktk sehemu za siri dawa za kuongeza hamu ya ngono ambazo hazijapimwa na Wataalamu, kwani kufanya hivyo kunawaweka hatarini kupata Saratani ya Shingo ya Kizazi

Soma > https://jamii.app/AfyaSaratani