JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Katika Mjadala wa Demokrasia, Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza, Aidan Eyakuze amesema ni muhimu kuzungumza kwa namna gani Serikali inaongeza Demokrasia kupitia uwanja wa kidigitali

Amesisitiza kuwa Serikali ya Kidigitali sio Demokrasia ya Kidigitali, na Ushiriki wa Watu Kidigitali nao haumaanishi Demokrasia

Soma > https://jamii.app/DemocracyTalk

#DemocracyTalkTz
MWIGULU: MFUMUKO WA BEI HAUTOKANI NA UZEMBE WA SERIKALI

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kupanda kwa gharama za maisha na mfumuko wa bei kunatokana na majanga yanayoendelea kuikumba Dunia na sio matatizo ya Sera

Soma https://jamii.app/MfumkoWaBei
#JFUchumi
TAKUKURU YAINGILIA KATI SAKATA LA MAKONDA NA GHALIB SAID MOHAMED KUGOMBEA KIWANJA

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Salum Hamduni athibitisha wanafanyia kazi suala hilo

Kamishna wa Ardhi Mkoa wa Dar, Idrisa Kayera amesema Mamlaka zinafanya Uchunguzi

Soma - https://jamii.app/MakondaGSM
PUTIN: OPERESHENI YA URUSI NCHINI UKRAINE IMEFANIKIWA

Rais wa #Urusi, Vladimir Putin amesema Operesheni ya Kijeshi Nchini #Ukraine imefanikiwa

> Amesema Benki Kuu ya Urusi haina haja ya kuchapisha pesa mpya

Soma > https://jamii.app/UkraineRussia

#JamiiForums #RussianUkraineWar
RAIS SAMIA: NAPENDA KUIONA TANZANIA YENYE #DEMOKRASIA YA KISTAARABU

Katika mahojiano na Mwananchi Digital, amesema anapenda kuiona #Tanzania yenye Raia wanaojielewa ktk kuitetea Nchi, sio wanaoambiwa waingie barabarani na kuharibu mali za watu

Soma - https://jamii.app/Wanaojielewa
MWANZA: Diana Bundala 'Mfalme Zumaridi' na wenzake 84 wamefikishwa Mahakamani kusomewa Maelezo ya awali katika mashtaka matatu yakiwemo usafirishaji haramu wa binadamu na kuzuia Maofisa wa Serikali kutimiza wajibu wao

Soma - https://jamii.app/Zumaridi

#JamiiForums #JFLeo
NJOMBE: JELA MIAKA 30 KWA KUMBAKA MPWA WAKE WA MIAKA 15

Mahakama imemhukumu Furaha Samweli Ligate miaka 30 jela kwa kumbaka Mpwa wake aliyekuwa amehitimu Darasa la Saba mwaka 2021

Mshtakiwa alitishia endapo angesema anafanyiwa ukatili huo

Soma - https://jamii.app/UbakajiNjombe

#JFLeo
NIGER: WATU 21 WAUAWA KATIKA SHAMBULIO LA KIGAIDI

Watu waliokuwa na silaha nzito wanaodhaniwa kuwa ni magaidi wameshambulia basi na lori eneo la Tillaberi

Maafisa wa Polisi wawili wameuawa na mmoja kujeruhiwa katika shambulio hilo

Soma - https://jamii.app/Niger21
#JFLeo
DAR: 14 MBARONI KWA TUHUMA ZA KUSAMBAZA VIDEO YA MGONJWA AKIWA ICU

Allen Samwel Mhina na wenzake 13 wanashikiliwa kwa tuhuma za kusambaza video Mitandaoni kinyume na Sheria

Video hiyo imemuonyesha Mgonjwa aliyekuwa amelazwa Hospitali ya Muhimbili

Soma - https://jamii.app/PoliceDar
DAR: WANANCHI WAHIMIZWA KUCHANGAMKIA CHANJO YA #COVID19

Mkuu wa Mkoa, Amos Makalla ametoa wito huo akisema mdau wa kwanza wa #Afya yako ni wewe mwenyewe

Aidha, ametaka Wananchi wahamasishwe kwa kupewa maarifa muhimu ili wawe na hiari ya kuchanja

Soma - https://jamii.app/DSMChanjo
UN imesema zaidi ya Raia 700 wakiwemo Watoto 52 wameuawa Nchini #Ukraine tangu Urusi ilipoivamia wiki tatu zilizopita

WHO imethibitisha mashambulizi 43 dhidi ya Hospitali na Vituo vya Afya huku Watu 12 wakiuawa na 34 kujeruhiwa

Soma - https://jamii.app/700DeadUkraine
#RussiaUkraineWar
#UKRAINE YARUHUSU MATUMIZI YA CRYPTOCURRENCY

Rais Volodymyr Zelensky ameruhusu matumizi ya Cryptocurrency baada ya utendaji wa Benki kuzorota kutokana na mzozo unaoendelea

> Kampuni za Cryptocurrency zitaruhusiwa kuwa na akaunti ktk Benki

Soma https://jamii.app/UkraineCryptocurrency
👍1
TMDA YAPIGA MARUFUKU KUVUTA SIGARA HADHARANI

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imekataza matumizi ya bidhaa za tumbaku maeneo yasiyo rasmi ili kulinda Afya ya Jamii

Watumiaji watatakiwa kutengewa maeneo yenye vibao ili kulinda Afya za wasiotumia

Soma https://jamii.app/SigaraTMDA
DAR: Jeshi la Polisi limewakamata watu 11 kwa kuwatapeli Masista wa Kanisa Katoliki Tabora Tsh. milioni 100 kwa kujifanya wanamiliki na kuuza viwanja vya makazi ambavyo sio vyao

> Matukio hayo yametokea kati ya Januari na Februari 2022

Soma > https://jamii.app/Utapeli
#JFMatukio
USWISI: BENKI ZATANGAZA KUZUIA ZAIDI YA TSH. TRILIONI 350 ZA WARUSI

Uswisi imetangaza kuwa na zaidi ya Dola Bilioni 160 (Takriban Tsh. Trilioni 372) zilizowekwa na Warusi. Fedha hizo zinazuiwa kutokana na vikwazo vilivyowekwa na EU dhidi ya Urusi

Soma - https://jamii.app/UswiziFedha
Pamoja na Serikali kukusanya mapato kwa asilimia 95, bado kumekuwa na changamoto katika usimamizi wa Mfuko Mkuu wa Serikali

Kwa Mwaka 2019/20, kiasi cha Tsh. bilioni 132.08 kutoka Mapato ya ndani ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa kilitumika bila kuripotiwa kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali

Kiasi hiki kimepungua kwa asilimia 76 kutoka kiasi cha Tsh. bilioni 553.38 kwa Mwaka 2018/19.

#JamiiForums #Accountability #JFUwajibikaji #WAJIBU
MBOWE: SISI SIO MAGAIDI, KOSA LETU NI KUSEMA UKWELI

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe amesema nafasi ya Chama hicho katika #Siasa na kuwa Chama Kikuu cha Upinzani imejengwa kwa Imani na Wananchi na kwa kuwa Watu wamefanya kazi

Soma - https://jamii.app/MbowePress
#JFLeo
MBOWE: KAULI YA CCM KWA POLISI, IGP SIRRO ALITAKIWA KUJIUZULU

Amesema CHADEMA wamekuwa wakihubiri sana kuhusu Jeshi la Polisi

"Tumeshasema sana kwamba Jeshi la Polisi linaonea Watu. Hata huko Magereza kumejaa sababu ya Uonevu wa Jeshi la Polisi"

Soma - https://jamii.app/MbowePress
ROBO FAINALI - UEFA: CHELSEA YAPEWA R. MADRID

- Michezo ya kwanza ya robo fainali itachezwa Aprili 5 & 6, 2022 huku ile ya marudiano ikichezwa Aprili 12 & 13, 2022

- Michezo ya kwanza ya nusu fainali itachezwa Aprili 26 & 27, 2022 huku ile ya marudiano ikichezwa Mei 3 & 4, 2022
Balozi wa Marekani Umoja wa Mataifa (UN), Linda Thomas-Greenfield amesema mzozo kati ya Urusi na #Ukraine sio Vita Baridi hivyo Nchi za Afrika haziwezi kubaki kati kwa kutounga mkono upande wowote

Asema hakuna Msingi wa kutoegemea upande wowote

Soma - https://jamii.app/UpandeAfrika