JamiiForums
βœ”
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MBEYA: Jeshi la Polisi linamshikilia Daniel William (Diwani wa Kata ya Iganzo) kwa tuhuma za kumshambulia kwa kumpiga sehemu mbalimbali za mwili Shadrack Zacharia ambaye ni Mpigapicha, akimtuhumu kumpiga picha bila idhini yake

Soma - https://jamii.app/DiwaniPolisi

#JamiiForums
MDAU: UELEWA WA JAMII NI KIKWAZO KWA WATANZANIA KUCHEZA SOKA LA KULIPWA

Anasema Jamii haielewi umuhimu wa Michezo na kupeleka kutokuwa na Mazingira wezeshi

Kuna uhaba wa vituo vya kulea vipaji na kusababisha kuwa na Wachezaji wachache Kimataifa

Soma - https://jamii.app/SokaChangamoto
Kutotayarisha Hesabu na kuziwasilisha kwa CAG kwa Ukaguzi ni uvunjifu wa Kifungu cha 25 cha Sheria ya Fedha za Umma No. 21 ya Mwaka 2001

Mwaka 2019/20 Mashirika ya Umma 11 hayakuwasilisha Hesabu kwa CAG kwa ajili ya Ukaguzi

#JamiiForums #WAJIBU #Accountability #JFUwajibikaji
UKRAINE: WATU WAZIKWA KWENYE KABURI LA PAMOJA

Jiji la Mariupol limechimba mfereji wa mita 22 na kuzika maiti zikiwa ktk mifuko ya plastik. Idadi kamili ya waliouawa haijafahamika

> Tangu Jumanne raia hawana huduma ya maji wala umeme.

Soma https://jamii.app/KaburiMoja
ABRAMOVICH AWEKEWA VIKWAZO NA UINGEREZA

Serikali ya #Uingereza imezuia mali na kumuwekea marufuku ya kusafiri Mmiliki wa #Chelsea, Roman Abramovich na matajiri wengine saba

> Uingereza imesema haiwezi kuwa kimbilio kwa wanaounga uvamizi wa Urusi

Soma https://jamii.app/AbramovichVikwazo
USHIRIKISHWAJI WANANCHI NI MSINGI WA #UTAWALABORA

Ushirikishwaji wa Umma unalenga kuhakikisha Wananchi wanatoa michango yenye maana katika mchakato wa kufanya maamuzi ambayo wanayategemea katika maisha yao

Pia, unatoa fursa ya Mawasiliano kati ya Taasisi zinazofanya maamuzi na Umma

Soma - https://jamii.app/UshirikiRaia
MDAU: UMUHIMU WA MAZOEZI KWA WATOTO WENYE ULEMAVU WA AKILI

Anasema ni muhimu kwa Watoto wenye Ulemavu huo kufanya Mazoezi ambayo hutolewa na '#Physiotherapists'

Mazoezi ndio tiba pekee inayobaki na sio Imani potofu za kupeleka Watoto kwa Waganga

Soma - https://jamii.app/UlemavuWaAkili
Wanajeshi 250 wa #Ukraine waliokuwa wakilinda amani DR-Congo wanatarajia kurejea #Ukraine na vifaa vyao

> Hivi karibuni Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy aliwataka walinda amani warejee ili kuitetea nchi yao

Soma https://jamii.app/UkraineDRC
Magonjwa ya Figo yanaweza kuwa na dalili kadhaa ikiwemo kupungua/kukosa mkojo

Mambo yanayochochea uwezekano wa kupata Magonjwa ya Figo ni pamoja na Ulaji usiofaa, unene uliokithiri, kutofanya mazoezi, uvutaji sigara na unywaji pombe uliopitiliza

Soma - https://jamii.app/WKD22

#WorldKidneyDay
KAMATI YAUNDWA KUCHUNGUZA MADAI YA SAMAKI KUFA KWA SUMU MTO MARA

Ni baada ya picha zinazodaiwa kuwa ni za Mto Mara zikionesha Samaki waliokufa kusambaa Mitandaoni, huku ikielezwa hali hiyo ni kutokana na kemikali za sumu zinazotoka Migodini

Soma - https://jamii.app/SumuMara
#JFLeo
KOREA KUSINI: MPINZANI ACHAGULIWA KUWA RAIS

Yoon Suk-yeol amemshinda mpinzani wake, Lee Jae-myung wa Chama cha Demokrasia kwa chini ya 1%

Waliojitokeza kupiga kura ni 77% ya wanaostahili. Wagombea wote walionekana kutopendwa muda wa kampeni

Soma - https://jamii.app/RaisKoreaKusini
KAYA 86 ZILIZO TAYARI KUHAMA NGORONGORO ZAJITOKEZA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amepokea majina 453 toka Kaya 86 zilizokubali kuondoka hifadhini

> Amesema Serikali imetenga Kilometa za Mraba 400,000 Wilayani Handeni kwaajili ya zoezi hilo

Soma https://jamii.app/NgorongoroHiari
NDUGULILE: KUTOZA KODI BIASHARA ZA MTANDAONI MAPEMA KUTAUA AJIRA NYINGI

Mbunge wa Kigamboni, amesema Tanzania iko nyuma ktk biashara mtandao hivyo ni muhimu kuzilea

> Amesema hayo baada ya mbunge wa Viti Maalum, Neema Lugangira kusema biashara zenye mauzo zaidi ya Tsh. Milioni 4 zitozwe kodi

Soma https://jamii.app/ecommerceTax
πŸ‘1
UPDATES: Serikali ya #Ukraine imesema Raia wa Mji wa #Mariupol wameshindwa kuondoka baada ya Makubaliano ya kusitisha mapigano kwa muda kushindwa kutekelezwa

Jitihada za kupelekea Chakula, Maji na Dawa kwenye Mji huo zimeshindikana

Soma - https://jamii.app/RaiaMariupol

#JFLeo
Kampuni ya Meta inayomiliki Mtandao wa Kijamii wa #Facebook na #Instagram imelegeza sera yake ili kuruhusu maneno ya chuki dhidi ya Urusi

Wataruhusu sentensi za chuki kama β€˜Death to Russian Invaders’ lakini hawataruhusu chuki dhidi ya raia

Soma - https://jamii.app/FacebookPolicy
#JFLeo
Kumekuwa na mapungufu mbalimbali katika Utekelezaji wa Bajeti. Taasisi mbalimbali za Serikali zilifanya matumizi nje ya Bajeti Mwaka 2019/20

Matumizi ya Fedha za Umma nje ya Bajeti yanapelekea uwezekano wa kuwepo Ubadhirifu na vitendo vya Rushwa

#JamiiForums #WAJIBU #JFUwajibikaji #Accountability
TRA: TUNAWAFUATILIA WATEJA WA WANAOFANYA BIASHARA MTANDAONI

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewataka wanaofanya Biashara Kidigitali wafike Ofisini kujisajili

Yasema kuna wenye Maghala makubwa ya bidhaa ila hawana Maduka na TIN

Soma - https://jamii.app/DigitalBusiness
#DigitalRights
MAREKANI YAOMBWA KUTOWEKA VIKWAZO KWA WATOA HUDUMA YA INTANETI URUSI

Asasi za Kiraia zimesema hatua ya Kampuni zinazotoa huduma ya Intaneti kuondoka Nchini Urusi kutokana na vikwazo inaweza kuathiri wenye Mawazo na Misimamo tofauti

Soma - https://jamii.app/InternetRussia
#DigitalRights
Wizara ya Afya Nchini #Kenya imelegeza masharti ya kupambana na #COVID19 ikiwemo kuondoa ulazima wa kuvaa Barakoa kwenye maeneo ya umma

Pia, Wagonjwa wasio na dalili hawatatengwa na hakutakuwa na ulazima wa kukaa Karantini kwa wenye virusi

Soma - https://jamii.app/COVID19Mask
#UVIKO3
JE, WAJUA? - KUTUMIA UGONJWA KUOMBA FEDHA BILA KIBALI NI KOSA KISHERIA

Wakili wa Kujitegemea, Justine Kaleb anasema Mgonjwa akitaka kuombaomba Mtaani lazima apate kibali maalum cha Serikali au Taasisi zinazotambua Ugonjwa wake

Kufanya tofauti na hivyo adhabu yake ni kifungo cha miaka mitatu jela au faini ya Tsh. milioni tano au vyote kwa pamoja

Soma - https://jamii.app/Ombaomba
#JFLeo