JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
RIPOTI: BELARUS YAENDELEZA UKANDAMIZAJI DHIDI YA WAPINZANI NA VYOMBO VYA HABARI

Ripoti hiyo ya UN inaweka wazi ukiukwaji unaofanywa kwa wanaojaribu kutekeleza Haki zao za Msingi, lakini pia inaonesha namna wahanga wanavyoshindwa kupata Haki zao

Soma - https://jamii.app/UNRipotiBelarus
MANENO GANI YA KIINGEREZA UMEYATAMKA VISIVYO KWA KIPINDI KIREFU?

Wadau wa Jukwaa la Lugha ndani ya JamiiForums.com wametolea Mifano maneno ambayo wameyatamka visivyo kwa muda mrefu yakiwemo; Entrepreneur, Advertisement, Schedule, Determine, Mishandle na Frying Pan

Maneno gani ya Kiingereza yamewahi au yanaendelea kukusumbua hadi sasa?

Mjadala zaidi > https://jamii.app/ManenoEnglish
MBEYA: KIJANA AKAMATWA NA POLISI AKISAFIRISHA VIPODOZI VYENYE SUMU

Polisi wanamshikilia Emmanuel Msigala (42) kwa kusafirisha vipodozi vyenye viambata Sumu vilivyopigwa marufuku

Mtuhumiwa ni mnunuzi, msafirishaji na muuzaji wa bidhaa hizo

Soma - https://jamii.app/Vipodozi
#Afya
LINDI: Mama mmoja Mkazi wa Ruangwa anatuhumiwa kumuua Mwanaye wa Mwaka mmoja kwa kumnywesha sumu ya kuua Magugu

Alifikia hatua hiyo baada ya Mama mkwe wake kukataa kukaa na Mtoto akimwambia bado mdogo, anastahili kuendelea kunyonya

Soma - https://jamii.app/SumuMtoto
#UkatiliWatoto
UKRAINE: Hospitali ya Wajawazito ya Mariupol imeshambuliwa na Wanajeshi wa #Urusi katika shambulio la anga na kusababisha majeruhi 17

> Inaelezwa kuwa, waliojeruhuwa ni Wafanyakazi na Wajawazito huku Watoto wakiwa salama

Soma https://jamii.app/17Wajeruhiwa
#RussiaUkraineCrisis
Leo Machi 10, 2022 ni Maadhimisho ya Siku ya Figo Duniani, inayolenga kuongeza ufahamu kuhusu Afya ya Figo ili kuziba pengo la uelewa wa Ugonjwa wa Figo. Mwaka huu, Kaulimbiu ni "Afya ya Figo kwa Wote"

Zipo njia mbalimbali za kupunguza hatari ya kupata Ugonjwa wa Figo zikiwemo kufanya mazoezi, kuzingatia Lishe na Mitindo bora ya Maisha

Soma - https://jamii.app/WKD22

#WorldKidneyDay2022
MAREKANI: Rais Joe Biden atasaini agizo la Serikali la kutaka utafiti ufanyike dhidi ya Crypto-Currency ili kubaini madhara yake kwny uchumi na usalama kwa wanaowekeza kwenye fedha hizo

> 16% ya Wamarekani wamewekeza katika Crypto-Currency

Soma https://jamii.app/CryptocurrencyMarekani
MBEYA: Jeshi la Polisi linamshikilia Daniel William (Diwani wa Kata ya Iganzo) kwa tuhuma za kumshambulia kwa kumpiga sehemu mbalimbali za mwili Shadrack Zacharia ambaye ni Mpigapicha, akimtuhumu kumpiga picha bila idhini yake

Soma - https://jamii.app/DiwaniPolisi

#JamiiForums
MDAU: UELEWA WA JAMII NI KIKWAZO KWA WATANZANIA KUCHEZA SOKA LA KULIPWA

Anasema Jamii haielewi umuhimu wa Michezo na kupeleka kutokuwa na Mazingira wezeshi

Kuna uhaba wa vituo vya kulea vipaji na kusababisha kuwa na Wachezaji wachache Kimataifa

Soma - https://jamii.app/SokaChangamoto
Kutotayarisha Hesabu na kuziwasilisha kwa CAG kwa Ukaguzi ni uvunjifu wa Kifungu cha 25 cha Sheria ya Fedha za Umma No. 21 ya Mwaka 2001

Mwaka 2019/20 Mashirika ya Umma 11 hayakuwasilisha Hesabu kwa CAG kwa ajili ya Ukaguzi

#JamiiForums #WAJIBU #Accountability #JFUwajibikaji
UKRAINE: WATU WAZIKWA KWENYE KABURI LA PAMOJA

Jiji la Mariupol limechimba mfereji wa mita 22 na kuzika maiti zikiwa ktk mifuko ya plastik. Idadi kamili ya waliouawa haijafahamika

> Tangu Jumanne raia hawana huduma ya maji wala umeme.

Soma https://jamii.app/KaburiMoja
ABRAMOVICH AWEKEWA VIKWAZO NA UINGEREZA

Serikali ya #Uingereza imezuia mali na kumuwekea marufuku ya kusafiri Mmiliki wa #Chelsea, Roman Abramovich na matajiri wengine saba

> Uingereza imesema haiwezi kuwa kimbilio kwa wanaounga uvamizi wa Urusi

Soma https://jamii.app/AbramovichVikwazo
USHIRIKISHWAJI WANANCHI NI MSINGI WA #UTAWALABORA

Ushirikishwaji wa Umma unalenga kuhakikisha Wananchi wanatoa michango yenye maana katika mchakato wa kufanya maamuzi ambayo wanayategemea katika maisha yao

Pia, unatoa fursa ya Mawasiliano kati ya Taasisi zinazofanya maamuzi na Umma

Soma - https://jamii.app/UshirikiRaia
MDAU: UMUHIMU WA MAZOEZI KWA WATOTO WENYE ULEMAVU WA AKILI

Anasema ni muhimu kwa Watoto wenye Ulemavu huo kufanya Mazoezi ambayo hutolewa na '#Physiotherapists'

Mazoezi ndio tiba pekee inayobaki na sio Imani potofu za kupeleka Watoto kwa Waganga

Soma - https://jamii.app/UlemavuWaAkili
Wanajeshi 250 wa #Ukraine waliokuwa wakilinda amani DR-Congo wanatarajia kurejea #Ukraine na vifaa vyao

> Hivi karibuni Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy aliwataka walinda amani warejee ili kuitetea nchi yao

Soma https://jamii.app/UkraineDRC
Magonjwa ya Figo yanaweza kuwa na dalili kadhaa ikiwemo kupungua/kukosa mkojo

Mambo yanayochochea uwezekano wa kupata Magonjwa ya Figo ni pamoja na Ulaji usiofaa, unene uliokithiri, kutofanya mazoezi, uvutaji sigara na unywaji pombe uliopitiliza

Soma - https://jamii.app/WKD22

#WorldKidneyDay
KAMATI YAUNDWA KUCHUNGUZA MADAI YA SAMAKI KUFA KWA SUMU MTO MARA

Ni baada ya picha zinazodaiwa kuwa ni za Mto Mara zikionesha Samaki waliokufa kusambaa Mitandaoni, huku ikielezwa hali hiyo ni kutokana na kemikali za sumu zinazotoka Migodini

Soma - https://jamii.app/SumuMara
#JFLeo
KOREA KUSINI: MPINZANI ACHAGULIWA KUWA RAIS

Yoon Suk-yeol amemshinda mpinzani wake, Lee Jae-myung wa Chama cha Demokrasia kwa chini ya 1%

Waliojitokeza kupiga kura ni 77% ya wanaostahili. Wagombea wote walionekana kutopendwa muda wa kampeni

Soma - https://jamii.app/RaisKoreaKusini
KAYA 86 ZILIZO TAYARI KUHAMA NGORONGORO ZAJITOKEZA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amepokea majina 453 toka Kaya 86 zilizokubali kuondoka hifadhini

> Amesema Serikali imetenga Kilometa za Mraba 400,000 Wilayani Handeni kwaajili ya zoezi hilo

Soma https://jamii.app/NgorongoroHiari
NDUGULILE: KUTOZA KODI BIASHARA ZA MTANDAONI MAPEMA KUTAUA AJIRA NYINGI

Mbunge wa Kigamboni, amesema Tanzania iko nyuma ktk biashara mtandao hivyo ni muhimu kuzilea

> Amesema hayo baada ya mbunge wa Viti Maalum, Neema Lugangira kusema biashara zenye mauzo zaidi ya Tsh. Milioni 4 zitozwe kodi

Soma https://jamii.app/ecommerceTax
👍1