JamiiForums
52.9K subscribers
34.3K photos
2.43K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
SIMIYU: WATENDAJI WA SERIKALI WAKAMATWA KWA WIZI WA CHUPA ZA DAWA

Watu 12 wakiwamo Watendaji wa Serikali za Mtaa wamekamatwa wakidaiwa kuiba Chupa 434 za Dawa za kuua wadudu wa Pamba zilizotolewa na Serikali kwa Wakulima Wilayani Bariadi

Soma - https://jamii.app/WiziSimiyu

#JFLeo
URUSI YATOA MASHARTI YA KUACHA KUISHAMBULIA UKRAINE

Imeitaka Ukraine kuitambua #Crimea kama sehemu ya #Russia, na Donetsk and Luhansk kama Mataifa huru

Aidha, #Ukraine imetakiwa kubadili Katiba na kukataa kuingia katika kambi yoyote kama NATO

Soma - https://jamii.app/UrusiMasharti
WANAFUNZI WA KITANZANIA WATOKA SALAMA UKRAINE

Waziri wa Mambo ya Nje, Balozi Liberata Mulamula amesema Wanafunzi wapatao 150 wamevuka salama na kukimbilia nchi za Poland, #Hungary, Romania na #Denmark. 23 wamefanikiwa kurejea Tanzania

Soma - https://jamii.app/WatanzaniaSalama

#JFLeo
#BURUDANI: Watu wengi hasa Vijana wanapenda kuangalia Filamu (#Movies). Filamu hizi huburudisha, huchangamsha na kutoa mafunzo kwa Jamii

Je, ni Filamu gani uliyowahi kuangalia zaidi ya mara moja na bado huichoki?

Mjadala - https://jamii.app/FilamuBurudani

#Entertainment #JamiiForums
SERIKALI: WATU 8 WAFARIKI DUNIA KWA #COVID19 NDANI YA MWEZI MMOJA

Visa vipya 290 viliripotiwa kuanzia Februari 5 - Machi 4, 2022. Wagonjwa 136 walilazwa na 128 kati yao hawakupata chanjo

Idadi ya waliopata dozi kamili ya chanjo Nchini ni 2,664,373

Soma https://jamii.app/8COVID19
#UKRAINE YATAKA ZELENSKY NA PUTIN KUFANYA MKUTANO

Taifa hilo linataka mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Rais Volodymyr Zelensky na Rais wa #Russia, Vladimir Putin likisema linatambua maagizo yote yanatoka kwa Kiongozi huyo

Soma - https://jamii.app/ZelenskyPutin

#RussiaUkraineWar
Machi 8 ni Siku ya Wanawake Duniani

> Tunaungana na Watu wote kuadhimisha Siku hii, na tunawatakia Maadhimisho mema ya Siku ya Wanawake Duniani

#JamiiForums #IWD2022 #InternationalWomensDay
👍1
Takwimu zilizotolewa na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins zimeonesha idadi ya Vifo vilivyotokana na #COVID19 vimefikia 5,999,158

Nchi nyingi zimelegeza masharti huku Safari na #Biashara zikianza kurejea. Aidha, kupata chanjo bado kunasisitizwa

Soma - https://jamii.app/COVID19Duniani

#UVIKO3
#UGANDA: Gabriel Rwotomiya amefariki kwa kupigwa risasi wakati Polisi wakituliza vurugu za Wanafunzi wa Sekondari Gulu baada ya kuzuiwa kutazama Mechi ya Man City na Man U, Machi 6

Wanafunzi wamerejeshwa Nyumbani na Shule kufungwa kwa muda

Soma - https://jamii.app/Uganda

#JFLeo
Katika Mwaka wa Fedha 2019/20, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) alipata taarifa za makusanyo ya Mapato katika Halmashauri 135

Alibaini Bilioni 18.77 zilikusanywa kutoka vyanzo mbalimbali, lakini hakuna ushahidi Mapato hayo yaliwasilishwa Benki

#JamiiForums #WAJIBU #JFUwajibikaji #Accountability
Katika kuadhimisha #InternationalWomensDay ni muhimu kuangazia changamoto mbalimbali zinazowakabili na kuhamasisha jitihada za kukomesha ukosefu wa #UsawaWaKijinsia

Leo, tunasherehekea na kutambua Uongozi, nguvu, uwezo, ujasiri na mchango walionao Wanawake wote katika Jamii

Maadhimisho ya Mwaka 2022 yanabeba Kaulimbiu isemayo, "Kizazi cha Haki na Usawa kwa Maendeleo Endelevu"

#JamiiForums #BreakTheBias #IWD2022
MDAU: WATUMISHI WAFUNDISHWE NAMNA BORA YA KUTUMIA MIKOPO WANAYOCHUKUA

Anasema Watumishi wa Serikali huvutiwa huchukua Mikopo wakiamini ni ya gharama nafuu hali inayowafanya wawe na madeni hadi wanastaafu

Ameshauri kiundwe chombo maalum cha kudhibiti usimamizi na uendeshaji wa Taasisi zote za Kifedha. Sheria ya Mafao iboreshwe ili kuwezesha Watumishi wanapostaafu wawe wanajengewe Nyumba za Makazi

Soma - https://jamii.app/WatumishiMadeni

#StoriesOfChange
Rushwa ya Ngono inatajwa kuwa tatizo linalowatafuna Wanawake ndani kwa ndani hasa maeneo ya Kazi

Utafiti wa Asasi ya Wanawake katika Habari Afrika (WIN) ulibaini 41% ya Wanawake wanahabari waliwahi kufanyiwa Unyanyasaji wa Kingono kazini

Soma - https://jamii.app/Womenday

#IWD2022
Rais Samia ametoa wito kwa Wananchi kujitokeza ktk zoezi la Sensa huku akisema suala jipya lililoongezwa ni swali kuhusu Anuani za Makazi

Asema hakutakuwa na swali kuhusu Dini kwa kuwa suala hilo lilishakataliwa tangu enzi za Mwl. Nyerere

Soma - https://jamii.app/DiniSensa
#JFLeo
MDAU: JAMII HAIWEZI KUCHOCHEA USTAWI BILA MAWAZO HURU

Anasema kukabiliana na changamoto kutahitaji sauti, uwazi na ukweli hivyo walio Madarakani wanahitaji kukosolewa

Jamii ikifungwa, watu wake wanakuwa kama Watumishi waoga badala ya Raia huru

Soma - https://jamii.app/UhuruKujieleza
Rais Samia Suluhu Hassan amesema kupanda kwa bei ya Mafuta kwa kiasi inasababishwa na Mgogoro kati ya Urusi na #Ukraine

Amesema “#Tanzania hatutanusurika, bidhaa zote zitapanda bei, nauli zitapanda bei, thamani ya kila kitu itapanda juu"

Soma - https://jamii.app/WomanDay

#IWD2022
Balozi wa #Urusi katika Umoja wa Mataifa (UN), Vassily Nebenzia, amesema Nchi yake itasitisha mapigano ili kuruhusu raia waliopo Kiev, Cher-nigov, Sumy na Mariupol kuondoka bila masharti kwa raia wanaopitia Urusi

Soma - https://jamii.app/RaiaWapite
#JamiiForums #RussiaUkraineConflict
KILIMANJARO: Grace Pima anashikiliwa na Polisi akidaiwa kumchoma Moto Mtoto wake wa Miaka Mitano Mdomoni na Puani kwa kosa la kutukana

Alifanya unyama huo Februari 28 na kumfungia Mtoto ndani kwa Saa 48 akimtibu kwa Dawa za Asili.

Soma - https://jamii.app/MotoMtoto
#UkatiliMtoto
#ZANZIBAR: Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati (ZURA) imetangaza kuanzia Machi 9, Petroli itauzwa Tsh. 2,459, Dizeli Tsh. 2,500 na Mafuta ya Taa Tsh. 1,811 kwa Lita

Ongezeko limetokana na kupungua thamani ya Shilingi na tozo za Serikali

Soma https://jamii.app/MafutaZanzibar
UPDATE: Ofisi ya #HakiZaBinadamu ya Umoja wa Mataifa inasema Raia wa #Ukraine wapatao 474 wameuawa tangu uvamizi wa Urusi kuanza, lakini inahofiwa idadi halisi inaweza kuwa kubwa zaidi

Ukraine imesema Vikosi vya Urusi vimeharibu takriban Hospitali 61

Soma - https://jamii.app/VifoUkraine