JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
VIONGOZI WA DINI: BUSARA ITUMIKE KUMALIZA KESI YA MBOWE

Wakiwa Ikulu, Dar wameomba Mamlaka husika kutumia busara na kuangalia namna ya kumaliza kesi hiyo

Pia, wamependekeza kuwe na Mjadala kuhusu Mfumo mpya wa Elimu utakaokidhi mahitaji ya sasa

Soma - https://jamii.app/ViongoziDiniIkulu
UKRAINE - UPDATES: Jeshi la Urusi linadaiwa kushambulia Shule 3 Mjini #Kharkiv. Pia inaripotiwa kuwa Majengo kadhaa ya Makazi ya Watu huko #Okhtyrka nayo yameharibiwa kutokana na mashambulizi yanayoendelea

Watu zaidi ya Milioni 1 wamekimbia #Ukraine

Soma https://jamii.app/UkraineUrusi
MSUMBIJI: MAWAZIRI SITA WAONDOLEWA KAZINI

Rais Filipe Nyusi amewatoa kwenye nafasi zao Mawaziri sita wakiwemo Waziri wa Fedha na Waziri wa Madini na Nishati

Ni Mabadiliko makubwa ya pili kufanyika kwenye Baraza la Mawaziri miezi ya hivi karibuni

Soma - https://jamii.app/MinisterSackMoz
URUSI: Waziri wa Ulinzi, Meja Jenerali Igor Konashenkov amesema Wanajeshi wa #Urusi 498 wameuawa na 1,597 wamejeruhiwa ktk mapigano na #Ukraine

> Aidha, Rais wa Ukraine amesema Wanajeshi wa Urusi 7,000 wameuawa ktk mapigano hayo

Soma https://jamii.app/UrusiWapiganaji

#RussiaUkraineConflict
Machi 03, 2022 ni Siku ya Usikivu Duniani ambapo inaelezwa takriban Watu Bilioni 1.5 Duniani kote wanaishi na tatizo la usikivu. Wataalamu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) wanasema idadi hii inaweza kuongezeka hadi Bilioni 2.5 kufikia Mwaka 2030

Kaulimbiu ya Mwaka 2022 inasema, "Ili kusikia maisha yote, sikiliza kwa uangalifu!"

Soma - https://jamii.app/TatizoUsikivu

#WorldHearingDay2022
DAR: Daniel Muga, mkazi wa Bombambili anasakwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumuua mtoto wake wa miaka mitatu kwa kumpiga na kitu kizito kichwani

> Kamanda wa Polisi Dar, ACP Muliro Jumanne Muliro amesema tukio hilo lilitokea Februari 28, 2022

Soma - https://jamii.app/Mauaji
AFYA: MAMBO UNAYOTAKIWA KUYAFAHAMU
KUHUSU KUCHANGIA DAMU


Huwezi kupata Maambukizi ya Magonjwa kwa kuchangia Damu kwasababu zoezi la kuchangia Damu ni salama na huendeshwa na Watumishi wenye ujuzi na vifaa vinavyotumika ni salama

Mtu mwenye #Afya ana wastani wa Lita 6 - 7 za Damu na anaweza kuchangia mara kwa mara, chupa moja ya Damu ina ujazo usiozidi Mililita 450. Pia, Mtu mwenye uzito wa Kilo 50 na kuendelea ana Damu ya kutosha kuweza kuchangia.

#JamiiForums #HealthCare #BloodDonation
Ripoti ya ukaguzi ya Mwaka 2019/20 inaonesha kati ya mapendekezo 15 yaliyotolewa na CAG Mwaka 2018/19, OR – TAMISEMI haikutekeleza pendekezo lolote kikamilifu

Ripoti hiyo pia inaonesha kati ya mapendekezo 3,126 yaliyotolewa Mwaka 2018/19, ni mapendekezo 1,071 sawa na 34% ndiyo yametekelezwa kikamilifu.

#JamiiForums #JFUwajibikaji #Accountability #WAJIBU #JFPartnership
MDAU: VIJANA WASHIRIKISHWE ZAIDI KWENYE SHUGHULI ZA MAENDELEO

Asema nyenzo ya uhusishwaji/ushikishwaji Vijana ktk Mipango na Utekelezaji wa shughuli za Maendeleo isipotumika vizuri, inaweza kuchangia Vijana na Serikali kulaumiana

Soma https://jamii.app/VijanaSerikaliSOC

#StoriesOfChange
LIBYA HATARINI KUTUMBUKIA ZAIDI KWENYE MGOGORO WA KISIASA

Bunge linajiandaa kuapisha Serikali ya Fathi Bashagha huko Tobruk, Mashariki mwa #Libya lakini Waziri Mkuu aliye Madarakani, Abdulhamid al-Dbeibah ameapa kutoachia madaraka

Soma - https://jamii.app/SiasaLibya

#JFLeo
WANACHAMA WA UN WAPIGA KURA YA MZOZO WA URUSI NA UKRAINE

Nchi 141 zimelaani #Russia na kuridhia kuwekewa vikwazo mbalimbali vya Kimaendeleo

Nchi 4 zimekubaliana na Urusi. Nchi 35 hazijafungamana na upande wowote ikiwemo #Tanzania, China na Uganda

Soma - https://jamii.app/UNVoteUkraine
ZANZIBAR: Rais Hussein Mwinyi atengua Uteuzi wa;

- Mkurugenzi Mkuu (Afya) Wizara ya Afya, Dkt. Abdulla Ali

- Mkurugenzi Mkuu wa Sekretarieti ya Tume ya Ushindani, Mohammed Jumanne

- Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uhifadhi Mji Mkongwe, Madina Khamis

Soma https://jamii.app/Utenguzi3Znz
UFARANSA: Serikali imewaambia Raia wake waondoke Nchini #Urusi kutokana na mashambulizi ya kijeshi ya Taifa hilo yanayoendelea Nchini #Ukraine

> Uingereza na Marekani zimeshatoa tangazo la kuwaondoa Raia wake nchini humo

Soma - https://jamii.app/RussiaFrance

#RussiaUkraineCrisis
MDAU: NI HATARI UMMA KUPOTEZA MAMLAKA YAKE KWA MUDA MREFU MPAKA UCHAGUZI

Anasema Demokrasia inakamilishwa na nguzo kuu nne; Kwanza ni lazima kuwe na mfumo wa kuchagua na kubadilisha Serikali kupitia Chaguzi Huru na za Haki

Pili, kuwe na ushiriki hai wa Watu (active participation of the people) katika michakato ya Kisiasa, Michakato ya Maamuzi na mwelekeo wa Nchi katika Maisha ya kila siku mbali na wakati wa Uchaguzi

Soma zaidi - https://jamii.app/MamlakaWananchi

#Democracy #HumanRights
SINGIDA: Polisi inawashikilia Wanafunzi sita wa Shule ya Sekondari Mwenge kwa kuchoma moto pikipiki ya Mwalimu yenye Namba 'MC 653 BFS' na kufyeka mahindi shambani mwake baada ya kupewa adhabu kwa kukutwa na simu shuleni kinyume na Taratibu

Soma - https://jamii.app/Shule
TABORA: AMUUA BABA YAKE KWA SHOKA AKIMSHUTUMU KWA USHIRIKINA

Maiko Jacobo (25) mkazi wa Kijiji cha Upungu, Nzega anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumuua baba yake mzazi, Jacobo Lubela (88) kwa kumkata kichwani, shingoni na mikono yote miwili

Soma - https://jamii.app/TaboraMauaji
MDAU: WATOTO WA NJE YA NDOA HUATHIRIKA KISAIKOLOJIA KWA KUKATALIWA

Anasema Watoto wa nje wanapata shida sana na kuathirika Kisakolojia hasa pale wanapohisi kukataliwa au kutokutambulika. Wengi huonekana kama Maadui na wezi wa Mali zilizotafutwa ndani ya Ndoa

Ameongeza, zipo sababu nyingi zinazopelekea kupatikana kwa Watoto wa nje ya Ndoa, ila Hisia zisitumike sana kwani huweza kuzalisha Uadui baina ya Watoto

Msome zaidi - https://jamii.app/WattNjeNdoa
#JamiiForums #Malezi
UKRAINE: KITUO CHA MITAMBO YA NYUKLIA CHASHAMBULIWA NA URUSI

Kituo cha Mtambo mkubwa wa Nishati ya Nyuklia Barani Ulaya, #Zaporizhia kimeshambuliwa usiku wa kuamkia leo

Ukraine yataka kusitishwa kwa mapigano ktk eneo hilo ili kuepusha Maafa

Soma - https://jamii.app/ZaporizhiaAttack

#JFLeo
UPDATES: Ukraine na #Russia zimekubaliana kutengeneza na kuweka maeneo salama ya kibinadamu ili kuruhusu Raia kuondolewa

Pande zote zimethibitisha Makubaliano hayo, lakini #Ukraine imesema bado haijapata matokeo inayohitaji

Soma - https://jamii.app/RussUkrAgree

#RussiaUkraineCrisis
Katika Ukaguzi wa Mapato ya Ndani ya Mamlaka za Serikali za Mitaa (MSM) 43 kwa kipindi cha 2017/18 - 2019/20, CAG alibaini kutokusanywa kwa Tsh. Bilioni 60.81 ambazo ni Mapato ya Ndani

Ukaguzi wa 2019/20 umeonesha kuongezeka kwa kutokusanywa kwa Mapato ya Ndani kwa kipindi cha 2016/17 - 2019/20.

#JamiiForums #JFUwajibikaji #Accountability #WAJIBU