JamiiForums
βœ”
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
BULGARIA: Waziri Mkuu, Kiril Petkov asema atamfuta kazi Waziri wa Ulinzi, Stefan Yanev baada ya Kiongozi huyo kusita kuelezea uvamizi wa Urusi dhidi ya #Ukraine kama vita akisisitiza "Waziri wangu hawezi kutumia neno operesheni badala ya vita"

Soma - https://jamii.app/BulgariaMD
SERIKALI YAONDOA TOZO YA TSH. 100 KWENYE MAFUTA

Tozo hiyo kwa kila Lita ya Dizeli, Petroli na Mafuta ya Taa yaondolewa kulinda Wananchi na athari za mabadiliko ya Bei za Mafuta

Bei zimepanda kutokana na sababu kadhaa ikiwemo vita ya Urusi & Ukraine

Soma https://jamii.app/TZTozoMafuta
#BELARUS: RAIS LUKASHENKO AJIONGEZEA MUDA WA KUKAA MADARAKANI

Tume ya Uchaguzi imesema 65% ya Watu waliopiga kura wameridhia mabadiliko ya #Katiba

Mabadiliko yanampa Rais Lukashenko aliyeiongoza tangu 1994 muda zaidi Madarakani na kinga ya Maisha

Soma - https://jamii.app/LukashenkoPower
UKRAINE YASAINI MAOMBI YA KUJIUNGA UMOJA WA ULAYA (EU)

Pia, Rais Volodymyr ameomba Umoja huo uiruhusu #Ukraine ipate Uanachama mapema iwezekanavyo, chini ya Utaratibu Maalum wakati ikijilinda dhidi ya mashambulizi ya Urusi

Soma - https://jamii.app/UkraineEU

#RussiaUkraineCrisis
URUSI YAENDELEA KUISHAMBULIA UKRAINE LICHA YA MAZUNGUMZO

Makombora yaua watu kadhaa #Kharkiv, na ving'ora vya mashambulizi ya anga vimesikika tena katika Mji Mkuu, #Kyiv

Rais Volodymyr asema shambulio la Urusi huko Kharkiv ni uhalifu wa kivita

Soma - https://jamii.app/RussiaAttacks
#BURKINAFASO: JESHI LAIDHINISHWA KUONGOZA KWA MIAKA MITATU

Mkutano wa Kitaifa umepitisha Mkataba utakaoruhusu Utawala wa Kijeshi kuongoza kipindi hicho

Mkutano huo uliidhinisha Hati ambayo baadaye ilisainiwa na Luteni Kanali Henri-Paul Damiba

Soma - https://jamii.app/Jeshi3BurFaso
AFGHANISTAN: Marufuku ya kusafiri nje ya Nchi imetolewa na Serikali ya #Taliban ikilenga kuwakinga Waafghanistan na ugumu wa Maisha nje ya Taifa hilo

Familia ambazo zinahitaji kuondoka zinahitaji kuwa na sababu muhimu kwa Mamlaka ya Uhamiaji

Soma - https://jamii.app/TravelBanTaliban
#HumanRights
Nguvu ya #Demokrasia halisi hutegemea Uhuru na Haki fulani za kimsingi. Uhuru na Haki hizi lazima vilindwe ili kuhakikisha Demokrasia inafaulu

Katika Nchi nyingi Haki za Msingi zinapatikana na kulindwa na #Katiba. Katiba huelezea Miundo na kazi za Serikali pamoja na kutoa Miongozo ya kuunda #Sheria nyingine

Kwa kawaida, Katiba inatakiwa kulindwa dhidi ya kufanyiwa marekebisho na Vigogo wa Serikali pasipo kuwasilisha mabadiliko yoyote kwa Wapigakura kupitia Kura ya Maamuzi/Maoni

#JamiiForums #Democracy
MDAU: OFISI ZA SERIKALI ZIWE NA KIBAO CHA KURIPOTI UZEMBE KWENYE UTOAJI HUDUMA

Apendekeza kuwe na kibao kwenye kila Taasisi inayohudumia Wananchi chenye namba za kuripoti kukitokea Ucheleweshwaji wa Huduma bila sababu za Msingi, Urasimu, na Uzembe wowote ule

Anasema hii itasaidia kuwa na Taasisi zinazofanya Kazi kweli na Wafanyakazi watakuwa hawana longo longo kwenye Utoaji huduma.

Msome - https://jamii.app/UzembeHuduma
#StoriesOfChange #Accountability
UPDATES: Mamlaka Nchini #Ukraine zinasema shambulio la Urusi limeua Wanajeshi wapatao 70 kwenye Kitengo cha Kijeshi huko Okhtyrka, Mji ulioko kati ya Kharkiv na Kyiv

Umoja wa Mataifa umesema idadi ya watu waliokimbia Ukraine imefikia 520,000

Soma - https://jamii.app/UrusiUkraine1
UFAHAMU UGONJWA WA POLIO (2)

Ugonjwa huu hauna tiba, na njia kuu ya kuuzuia ni kuwapatia watoto chanjo ya Polio ambayo hutolewa kwa Dozi Nne

Wataalamu wanasema ni muhimu Mtoto akamilishe ratiba ya Chanjo kama inavyotakiwa ili kupata kinga kamili

Soma - https://jamii.app/UgonjwaPolio
LINDI: MGANGA ATUHUMIWA KUMBAKA MWANAFUNZI

Jeshi la Polisi Mkoani humo linamtafuta Mganga wa Kienyeji Juma Salumu maarufu 'Juma Kipanya' anayekabiliwa na tuhuma za kubaka na kumpa ujauzito Mwanafunzi (15) wa Darasa la Saba

Soma - https://jamii.app/LindiMganga
#HumanRightsViolations
URUSI: Kocha wa Klabu ya Lokomotiv Moscow, Markus Gisdol (52), amejiuzulu akipinga uvamizi wa Urusi kwa Ukraine

Asema β€œSiwezi kuwa kwenye uwanja wa mazoezi huko Moscow kufundisha wachezaji wakati umbali wa Kilomita chache yanatolewa maagizo yanayoleta mateso kwa watu”

#JFSports
GENEVA: Zaidi ya Wajumbe 140 wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, leo Machi 1, 2022 walitoka nje ya ukumbi wakikataa kusikiliza hotuba ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergei Lavrov

> Wanapinga uvamizi wa Urusi Nchini Ukraine

Soma - https://jamii.app/UNRussia
ADIDAS YAVUNJA USHIRIKIANO NA URUSI

Adidas imesimamisha ushirikiano na Chama cha Soka cha Urusi baada ya nchi hiyo kuvamia Ukraine

Adidas ambayo ni Kampuni ya 2 kwa ukubwa kwa utengenezaji wa vifaa vya michezo, imesitisha udhamini wa jezi za Urusi ulioanza mwaka 2008

#JFSports
GHANA: Kundi la kwanza la Raia wa Ghana wakiwemo Wanafunzi limewasili Accra Nchini humo toka Ukraine ambapo kuna machafuko ya kushambuliwa na Urusi

> Inaelezwa kuwa, wengi wa Raia hao wanaelekea Slovakia, Hungary, Romania na Poland

Soma - https://jamii.app/GhanaUkraine
UTEUZI: Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi amemteua Yusuph Juma Mwenda kuwa Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB). Uteuzi wake unaanza leo Machi 01, 2022

Kabla ya kuteuliwa na Rais Mwinyi, Mwenda alikuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)

Soma - https://jamii.app/UteuziZRB
MDAU: WAZAZI HUCHANGIA KUHARIBU NDOA ZA WATOTO WAO

Anasema Ndugu/Wazazi wanapokuja kukaa kwa Mtoto wao mwenye Ndoa huwa na Mitazamo tofauti ya namna wanavyotegemea Ndoa iwe na huweza hata kuleta mfarakano na kuharibu Uhusiano uliopo

Ikiwa Ndugu wanakuja kuishi nanyi ni vema kuwe na sababu zinazochangia kukaa na nyie ikiwemo Ugonjwa au Maisha magumu. Lakini kama Mzazi ana nguvu na anaweza kufanya kazi zake za kawaida ni makosa kuishi kwa Mwanao aliyeoa/aliyeolewa

Msome - https://jamii.app/WazaziNdoaMtoto
#Maisha #Mapenzi
πŸ‘1
VISA NA MASTERCARD ZAFUNGIA TAASISI ZA FEDHA ZA URUSI

- Zimezifungia Taasisi hizo kutumia mifumo ya huduma zake ikiwa ni sehemu ya vikwazo kwa Urusi

- Pia, zimeahidi kutoa Dola za Kimarekani Milioni 2 kila moja kwa ajili ya kusaidia Ukraine

Soma https://jamii.app/VisaMastercard-Ur

#JFLeo