JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
RAIS SAMIA: WANASIASA WA TANZANIA HAKUNA HATA ALIYEUMWA NA SISIMIZI

Akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya DW amesema Wanasiasa wa Upinzani wako wengi Tanzania na hakuna anayeishi kwa mashaka hivyo Tundu Lissu aulizwe mashaka yake ni yapi

Soma - https://jamii.app/SiasaTz

#JFSiasa
INDIA: 13 WAPOTEZA MAISHA BAADA YA KUTUMBUKIA KISIMANI

Wamefariki dunia baada ya kuangukia ndani ya kisima wakiwa Harusini

Mamlaka zasema waliofariki ni Wanawake na Watoto, 11 walipoteza maisha eneo la tukio na wawili wakipatiwa matibabu

Soma - https://jamii.app/13DeadIndia

#JFMatukio
Rais Samia amesema Serikali ipo tayari kupokea Mapendekezo kuhusu Marekebisho ya Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016, ambapo baadhi ya vipengele vimekuwa vikilalamikiwa kuwa kandamizi

Ameeleza hayo kwenye Mahojiano Maalum na DW

Soma - https://jamii.app/SheriaKandamizi

#PressFreedom
BAJETI ZITEKELEZE MIPANGO ILIYOPANGWA

Mdau anashauri kuwepo Mfumo shirikishi utakaosaidia Wananchi kushiriki katika kuonesha vipaumbele vya Maendeleo na Utekelezaji

Itasaidia Wananchi kuwa Wasimamizi wa Miradi katika maeneo yao

Soma - https://jamii.app/MdauSOC1

#StoriesOfChange #Accountability
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema suala la idadi ya Watu ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro ni kubwa, hivyo watakaotaka kuhama kwa hiyari Serikali itawahudumia

Pia, amewataka wakazi wasiwalazimishe Watu kubaki kwa kuwa Mtu anaweza kuishi kokote

Soma - https://jamii.app/NgorongoroPM

#Governance
FREEMAN MBOWE NA WENZAKE WAKUTWA NA KESI YA KUJIBU

Mahakama imemkuta Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe pamoja na Washtakiwa wengine watatu na Kesi ya Kujibu katika Mashtaka matano kati ya 6 kwenye Kesi ya Uhujumu Uchumi yenye Mashtaka ya Ugaidi inayowakabili

Jaji Joachim Tiganga amesema Mahakama imepitia vielelezo vyote vya Upande wa Mashtaka na Utetezi, na imeona upo Ushahidi Washtakiwa Wana Kosa la Kujibu

Soma zaidi - https://jamii.app/MboweKesiJibu

#JFSiasa
ZANZIBAR: Rais wa #Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi amemteua Balozi Mohammed Mwinyi Mzale kuwa Kamishna wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma katika Ofisi ya Rais; Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora

Uteuzi wake umeanza leo Februari 18, 2022

Soma - https://jamii.app/UteuziKamishZnz

#Governance
BRUSSELS, UBELGIJI: Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen leo Februari 18, 2022

Rais Samia yupo Nchini Ubelgiji kwa ziara ya kikazi

#Governance
Dkt. Ahmed Yousef wa Hospitali ya Chuo Kikuu cha Aga Khan amesema 15% hadi 20% ya wenye matatizo ya Nguvu za Kiume huteseka kimyakimya

Dalili ni kushindwa kushiriki Tendo kwa Dakika 15 mfululizo, kushindwa kusimamisha na kuwahi kumaliza

Soma - https://jamii.app/UpandikizajiUume

#JFAfya
Wadau wa Jukwaa la Elimu ndani ya JamiiForums.com wametaja mbinu kadhaa zilizokuwa zinatumika kukariri Sayari ikiwemo, "Mama Veronica Endeleza Mapishi Jikoni Sitaki Ugali Nataka Pilau"

Ulitumia njia gani kufahamu Formula na Mipangilio ukiwa Shuleni?

Mjadala zaidi > https://jamii.app/FormulaShule

#JFMdau
TETEMEKO LATOKEA MPANDA, KATAVI

Tetemeko la Ardhi la kipimo cha Richa 4.6 limeripotiwa kutokea Mpanda, Katavi usiku huu

> Hakuna taarifa ya kifo madhara yoyote yalioripotiwa hadi sasa. JamiiForums inaendelea kufuatilia kwa karibu tukio hilo

Soma https://jamii.app/TetemekoKatavi

#JFMatukio
TANZANIA YAPATA MSAADA WA TSH. TRILIONI 1.15 KUTOKA ULAYA

Fedha hizo zitatumika ktk Miradi mbalimbali ya Maendeleo

Serikali imeainisha kutumia Tsh. Bilioni 480 (Euro Milioni 180) kwenye miradi mitatu ikiwemo kuimarisha Mifumo ya Kidijitali

Soma - https://jamii.app/TZFedhaUlaya

#Governance
MDAU ASHAURI VYA KUFANYA KUEPUKA AJALI ZA MOTO

Mshiriki wa #StoriesOfChange ashauri kuelimisha Jamii. Pia kuwa na Sheria ya kudhibiti mafundi holela

> Kufunga vifaa vya kutaarifu kuhusu moto. Vifaa vya kuzima moto vipatikane kwa bei nafuu

Soma https://jamii.app/MotoAjali

#JFMdau
RADI YAJERUHI WAWILI NGORONGORO

Jeshi la Polisi limesema Uchunguzi umebaini chanzo ni matumizi ya simu wakati mvua kubwa ikinyesha huku ikiambatana na radi kali

Waliojeruhiwa wamepata majeraha sehemu mbalimbali, na wanapatiwa matibabu Zahanati

Soma > https://jamii.app/2MvuaSimu

#JFMatukio
UGAWAJI WA MIRABAHA WAKOSOLEWA

Mtandao wa Sekta ya Ubunifu Tanzania(CINT) umesema mirabaha inapaswa kulipwa kwa kazi zote za ubunifu sio wanamuziki pekee

> COSOTA imekosolewa kukosa uwazi wa kanuni iliyotumika kugawa mirabaha

Soma https://jamii.app/MirabahaCOSOTA

#JFBurudani
NAPE: SHERIA INALENGA KUADHIBU MWANAHABARI SIO CHOMBO

Waziri wa Habari, Nape Nnauye amesema Sheria ya Habari ya 2016 inalenga kutoa leseni kwa wanahabari ili likitokea kosa aadhibiwe mtu sio Chombo cha Habari

> Nia ni kufanya tasnia ya habari kuwa taaluma

Soma https://jamii.app/KufungiaMtu

#PressFreedom
RUKWA: AMCHAPA MKEWE VIBOKO MPAKA KIFO

Kamanda wa Polisi Rukwa, ACP William Mwampaghale amesema Mwanaume huyo alianza kumshambulia Mkewe kwa fimbo maeneo mbalimbali ya Mwili na kusababisha kuvuja Damu nyingi kwa ndani na baadaye kusababisha mauti

Soma - https://jamii.app/KifoViboko

#JFMatukio #UkatiliKijinsia
SIKU YA KIMATAIFA YA HAKI ZA KIJAMII

Siku hii huangazia hitaji la kukuza Haki za Kijamii ambazo zinahusisha jitihada za kushughulikia masuala mbalimbali kama Umasikini, Ukosefu wa Usawa wa Kijinsia, Ajira na #HakiZaBinadamu

Soma - https://jamii.app/SJD2022

#SocialJusticeDay #SocialJustice
KAMATI YA KUCHUNGUZA MAUAJI YA MTWARA NA TANGA YAONGEZEWA SIKU 7

Kamati hiyo iliyoanza kazi Februari 4, 2022 ilipaswa kukamilisha ripoti yake Februari 17, 2022 ila imeomba muda zaidi kutokana na ukubwa wa kazi na kujiridhisha na baadhi ya masuala

Soma - https://jamii.app/KamatiMauaji7

#Accountability