JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
UJASIRIAMALI: #Biashara ya kuoka Mikate, Maandazi na Keki inakua kwa kasi kutokana na ukubwa wa Soko lake

Vifaa vya muhimu ni Jiko la kuokea Mikate (Oven), Prover kwa ajili ya kuumulia Unga wa Ngano, Mixer ya kuchanganyia mahitaji, Slicer ya Mkate, meza pamoja na mikebe ya Oven

Jifunze uzalishaji, masoko na changamoto za Bakery - https://jamii.app/BiasharaMikate

#JFBiashara
BUNGENI: Mbunge wa Kinondoni, Tarimba Abbas amehoji ikiwa Serikali haioni ni muda wa kulifumua Shirika la Umeme (TANESCO) ili kuwe na Kampuni 3 kwa ajili ya Uzalishaji, Usafirishaji na Ugawaji Umeme

Waziri Mkuu asema kutolewa maeneo hayo kwa watu tofauti kunaweza kuleta athari kwenye Usalama wa Nchi

Soma - https://jamii.app/TANESCOBungeni

#JFSiasa
CHAMA KIMOJA PEKEE KIMEWASILISHA JINA LA MGOMBEA UNAIBU SPIKA

Bunge limesema zoezi la uteuzi limekamilika, na hadi kufikia muda huo CCM ndiyo imewasilisha jina

Litawasilishwa mbele ya Wapiga Kura kesho Februari 11, 2022 kwa taratibu za Uchaguzi

Soma - https://jamii.app/NaibuSpikaBunge

#Democracy
KATAVI: MWALIMU WA MAFUNDISHO AKAMATWA KWA KULAWITI WATOTO 4

Jeshi la Polisi limemkamata Mwalimu wa Mafundisho ktk Kanisa la Katoliki Mpanda Mjini, Joseph John(27)

Alikuwa akiwalaghai Watoto wamsindikize kwenye shughuli za Biashara

Soma - https://jamii.app/MwlRCUlawiti

#JFMatukio #GBV
TANZIA: DKT. MWELE MALECELA AFARIKI DUNIA

Aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Tanzania (NIMR), Dkt. Mwele Malecela amefariki Dunia akiwa Geneva - Uswisi

Enzi za Uhai wake, Dkt. Mwele aliwahi kujitangaza kusumbuliwa na Maradhi ya Saratani

#JFLeo
Kati ya Mwaka 2030 hadi 2050 Mabadiliko ya TabiaNchi yanatarajiwa kusababisha takriban vifo 250,000 zaidi kwa mwaka

Shirika la Afya Duniani(WHO) limetaja Mabadiliko hayo kuwa tishio kubwa zaidi la kiafya linalowakabili Binadamu

Soma https://jamii.app/AfyaTabiaNchi

#ClimateChange #JFAfya
#COVID19: Namna Bara la Afrika linavyokabiliana na janga hilo imetajwa kubadilika, lakini kasi zaidi katika Chanjo inahitajika ili kudhibiti maambukizi

Mkurugenzi wa WHO-Afrika asema jitihada inapaswa kuwa kwenye kuhamasisha watu kuchanjwa

Soma https://jamii.app/ChanjoAfrica

#UVIKO3 #JFAfya
Ripoti ya Faharasi ya #Demokrasia imeonesha Demokrasia kushuka Mwaka 2021

45.7% ya Watu Duniani waliishi ktk aina fulani ya Demokrasia pungufu ya 49.4% Mwaka 2020

Ni 6.4% pekee ya Watu ndiyo wanaishi ktk mazingira ya Demokrasia kamili

Soma https://jamii.app/DemocracyFall

#Democracy
ANGOLA YADAI KUREJESHA ZAIDI YA DOLA BILIONI 11.5 ZILIZOIBWA SERIKALINI

Waziri wa Sheria asema ndani ya miaka mitatu iliyopita Serikali imerejesha Mali na Fedha zinazofikia Dola za Marekani Bilioni 11.5 zilizoibwa na kufichwa Mataifa mbalimbali

Soma - https://jamii.app/AssetsAngola

#JFUwajibikaji
SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE NA WASICHANA KATIKA SAYANSI

Ushiriki kamili wa Wanawake na Wasichana kwenye Sayansi na Teknolojia ni muhimu zaidi wakati huu ambapo Dunia inaendelea kukabiliana na COVID-19 na janga la Mabadiliko ya TabiaNchi

Ni wakati wa kupinga Ubaguzi dhidi ya Wanawake na Wasichana katika Sayansi

Soma - https://jamii.app/WomenGirlsScience

#WomenInScience
MAREKANI YAHIMIZA RAIA WAKE KUONDOKA UKRAINE

Ni kutokana na vitisho vya Urusi kuchukua hatua za Kijeshi kuongezeka. Rais Biden asema hatotuma Vikosi kuokoa Wamarekani ikiwa Ukraine itavamiwa

Urusi imekuwa ikikataa kuwa na Mipango ya kuvamia Ukraine

Soma https://jamii.app/USUkraine

#Governance
JE, WAJUA: Utafunaji wa Chingamu (Maarufu Big G/Jojo) ulipigwa Marufuku Nchini #Singapore tangu Mwaka 1992 kwa lengo la kuhifadhi Mazingira na kuyaweka Safi

Mnamo Mwaka 2004, Marufuku hiyo ilifanyiwa marekebisho na kuruhusiwa kwa Chingamu zinazotumika kwa Matibabu ya Kinywa ambazo hununuliwa Hospitalini au Famasi

#JamiiForums #JFMaarifa
MDAU: MZAZI NI KIUMBE WA KIPEKEE SANA

Anasema Siku zote ni ngumu Mzazi kutoa laana kwa Mtoto, lakini hii haimaanishi laana hazitoki. Laana na Baraka hutokana na mapokeo ya Moyo kwa kile anachotendewa na Mtoto wake

Ukiona Mzazi anaomba msaada kwa Mwanaye tambua ana shida kweli kwasababu Wazazi wengi hawapendi kuonekana wasumbufu

Soma, zaidi - https://jamii.app/MzaziMtoto

#JFMdau
VIJANA TUWE WABUNIFU, WAAMINIFU NA TUSAIDIE JAMII ZETU

Mdau anasema wimbi kubwa la Vijana wamekuwa Wavivu wa kubuni, wanatumia muda mwingi katika starehe zisizo za ulazima na hata kukosa muda wa kupumzika. Wanasahau kufikiria kuisaidia Jamii

Kuishi ndani ya matendo na kauli nzuri kutafanya wajenge thamani katika Jamii

Msome - https://jamii.app/UshauriVijanaSOC

#StoriesOfChange #JFMdau
Jamii Forums kwa kushirikiana na Muhimbili University of Health and Allied Science (MUHAS), Muhimbili National Hospital (MNH), Tumaini la Maisha (TLM) na Wadau wengine wameandaa Mjadala utakaofanyika kupitia Clubhouse ya JamiiForums ili kuongeza uelewa juu ya Saratani kwa Watoto Nchini #Tanzania

Mjadala huu unatarajiwa kufanyika Jumanne, Februari 15, 2022 ambapo Wataalamu mbalimbali wa #Afya wataeleza kwa kina kuhusu Saratani ya Watoto na namna ya kukabiliana nayo

Je, una swali gani au ungependa kufahamu nini kuhusu hali ya #Saratani kwa Watoto? Karibu ujiunge nasi katika Mjadala huu.

#JamiiForums #CancerDay2022 #JFAfya
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema Serikali itagharamia matibabu ya aliyekuwa Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule (Prof. Jay) anayetibiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili hadi hapo atakaporuhusiwa

Ametoa kauli hiyo alipofika Muhimbili leo kumjulia hali

Soma - https://jamii.app/SerikaliProfJ

#JFAfya
MADAGASCAR: WALIOFARIKI KUTOKANA NA KIMBUNGA BATSIRAI WAFIKIA 111

#Batsirai kilikuwa Kimbunga cha pili kuathiri Taifa hilo ndani ya muda wa siku 14

Kimbunga Ana kilisababisha Vifo 55 na kupelekea Watu wapatao 130,000 kukosa Makazi

Soma - https://jamii.app/Batsirai111

#JFMatukio
BUNGENI: Mgombea pekee wa nafasi ya Unaibu Spika wa Bunge la Tanzania, Mussa Azzan Zungu (Mbunge wa Ilala) amepata 98.33% ya Kura zilizopigwa

Wabunge 301 walipiga Kura, 296 wamepiga Kura za Ndiyo, 3 wamepiga Kura ya Hapana na Kura 2 zimeharibika

Soma - https://jamii.app/ZunguNaibuSpika

#Democracy
👍1
TANZANIA NA UFARANSA ZASAINI MIKATABA SITA

Miongoni mwa Makubaliano ni Mkataba wa Mkopo wa Masharti Nafuu wa Euro Milioni 178 kwa ajili ya kugharamia Mradi wa Ujenzi wa Barabara wa Mabasi Yaendayo Haraka

Soma - https://jamii.app/MikatabaTZFrance

#Governance
🥰1
#SUDAN: Wanaharakati wanaopinga Mapinduzi wamesema zaidi ya Watu 2,000 wakiwemo Waandishi wa Habari, Wanasiasa wanaokosoa Jeshi na Watetezi wa Haki za Binadamu wamekamatwa bila kushtakiwa tangu Jeshi lilipopindua Serikali Oktoba 2021

Soma - https://jamii.app/SudanArrests
#Democracy