JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
NJOMBE: Israel Msigwa maarufu kama 'Mtoa Roho' anatuhumiwa kumuadhibu Mwanaye Haskad Msigwa (7) kwa nyaya za umeme kwa kosa la kukojoa kitandani, na kumsababishia kifo

Mtuhumiwa alikamatwa Februari 3 Mkoani Iringa alipokimbilia kujificha

Soma - https://jamii.app/KifoNjombe

#JFMatukio
SONGWE: MBARONI KWA TUHUMA ZA KUMCHOMA MOTO MTOTO WA MIEZI 6

Mariko Kahinga aliyedai Mkewe alipewa mimba na Mwanaume mwingine atafikishwa mahakamani kwa mujibu wa Sheria

Mama wa Mtoto huyo, Patricia Mwilenga asema Mumewe alikuwa akitamka kauli mbaya

Soma https://jamii.app/SongweBaba

#JFMatukio #HakiMtoto
KIRUSI KIPYA CHA HIV CHAGUNDULIKA UHOLANZI

Kirusi kipya cha HIV/AIDS kimegundulika Nchini Uholanzi na kupewa jina la #VBVariant. Kinadaiwa kushambulia Kinga ya Mtu mara mbili zaidi

Siku mbili zilizopita Kampuni ya #Moderna ilitangaza kuanza majaribio ya Chanjo ya HIV (mRNA-based HIV vaccive) ambapo Watu 56 waliojitolewa watapewa Dozi moja na wengine mbili huku wakifuatiliwa kwa Miezi 6.

Soma - https://jamii.app/VBvariantHIV

#JFAfya
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa agizo kwa IGP Simon Sirro kuwasimamisha kazi RPC na RCO Mkoa wa Mtwara, pamoja na Mkuu wa Kituo cha Polisi eneo alilofia Mfanyabiashara Mussa Hamisi

Viongozi hao wametakiwa kukaa pembeni ili kupisha uchunguzi

Soma - https://jamii.app/PolisiMtwara

#JFUwajibikaji
WAZIRI UMMY: WANAUME JITOKEZENI KUPIMA TEZI DUME

Waziri wa Afya amesema watu 28,610 hufariki dunia kwa Saratani kwa mwaka. Saratani inayoongoza kwa Wanaume ni tezi dume na Wanawake ni mlango wa kizazi

Tezi dume inapimwa kisasa sio kama awali

Soma - https://jamii.app/TeziDume

#JFAfya
URUSI YAFUNGA SHUGHULI ZA SHIRIKA LA UTANGAZAJI LA DW

Urusi imefunga shughuli za Shirika la Habari la DW mjini #Moscow na kuwapokonya Wafanyakazi vibali vya Kazi ili kulipiza kisasi baada ya #Berlin kukifunga kituo cha Russia Today

Soma - https://jamii.app/DWBanRussia
#PressFreedom
NJOMBE: Mganga wa kienyeji aitwaye Joseph Mgunda (41) anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuwaua Suzana Mtitu (38) na Kassim Kitamkanga (35) baada ya dawa ya utajiri aliyowapa kuonekana haifanyi kazi

Anadaiwa kuwaahidi wateja wake utajiri

Soma - https://jamii.app/MgangaAua

#JFMatukio
UTABIRI TMA: KIMBUNGA BATSIRAI KUPIGA KUSINI MAGHARIBI MWA BAHARI

Kimbunga hicho kilijitokeza Januari 27, 2022 na kimesogea Kisiwa cha #Madagascar

Mamlaka imesema uchambuzi unaonesha kutokuwepo kwa uwezekano wa Kimbunga kufika Pwani ya #Tanzania

Soma - https://jamii.app/BatsiraiCyclone
GEITA: Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Naomi amejinyonga kwa kamba ya manila katika choo cha nyumba ya wageni inayomilikiwa na Mumewe

Alifika kwenye nyumba hiyo na kuomba mhudumu amsaidie kumshika Mtoto wa miezi minne akidai anajisikia vibaya

Soma - https://jamii.app/NyumbaYaWageni

#JFMatukio
RIPOTI UN: MALI YAONGOZA KWA VIFO VYA WALINDA AMANI MIAKA 8 MFULULIZO

Wanajeshi 24 na Mfanyakazi 1 wa UN waliuawa Mwaka 2021 huku 19 kati yao wakiuawa nchini Mali

> Inaelezwa kuwa hakuna aliyekamatwa wala kuwajibishwa kwa mauaji hayo


Soma - https://jamii.app/DeathPeaceKeepers

#HumanRights
ARUSHA: James Sindio (16) anatafutwa na Polisi kwa tuhuma za kumuua kaka yake, Zakayo Sindio walipogombana kuhusu kulisha mifugo

> Baba mzazi wa watoto hao, Paulo Sindio alikwenda kuwaamua alikuta tayari Zakayo amechomwa kisu na James

Soma https://jamii.app/NduguWauana

#JFMatukio
MBEYA: Gloria Kibira (38) ambaye ni Afisa Ustawi wa Jamii wa Kituo cha Mahabusu ya Watoto cha Kabwe, Kata ya Iyela amekutwa amenyongwa kwenye nyumba yake ndani ya eneo la Kituo cha Mahabusu

Watu wawili wanahojiwa kubaini chanzo cha mauaji

Soma - https://jamii.app/MbeyaAnyongwa

#JFMatukio
#AFCON2021: #TeamSenegal imetwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kuifunga #TeamEgypt 4-2 kwa mikwaju ya penati

Hii ni mara ya kwanza kwa Senegal kutwaa Ubingwa huo baada ya kucheza jumla ya Fainali tatu za #AFCON

Soma https://jamii.app/SenegalAFCON

#JFSports
TUNISIA: RAIS SAIED AVUNJA BARAZA KUU LA MAHAKAMA

Kitendo hicho kimetajwa kuwa kinyume na Sheria, huku Majaji wakisema hawatokaa kimya. Rais amewashutumu Majaji kwa upendeleo na ufisadi

Julai 2021, Rais huyo alisitisha shughuli za Bunge

Soma - https://jamii.app/TunRaisMajaji

#Democracy
MADAGASCAR: Watu 6 wamefariki baada ya Kimbunga #Batsirai kupiga Kisiwa hicho. Kisiwa cha Mananjary na Miji ya karibu vimekumbwa na uharibifu mkubwa

Zaidi ya Watu 47,000 wameyakimbia makazi yao kutokana na dhoruba iliyoletwa na Mvua kubwa na Upepo mkali

Soma https://jamii.app/BatsiraiMadagascar

#JFMatukio
#COVID19 YATISHIA JITIHADA ZA KUKOMESHA UKEKETAJI

UNICEF imesema mlipuko wa Corona umevuruga programu za kulinda Wasichana na vitendo hivyo

> Inakadiriwa kuwa, visa milioni 2 vya Ukeketaji vinaweza kutokea katika muda wa miaka kumi ijayo

Soma - https://jamii.app/UNICEF-FGM

#EndFGM
JE, WAJUA?: #TeamSenegal imefuzu kushiriki mashindano ya #AFCON mara 15 na kuingia fainali mara tatu, ikipoteza fainali za Mwaka 2002 na 2019

Kocha wa Senegal, Aliou Cisse alikuwa mmoja wa wachezaji waliopoteza penalti ktk fainali 2002

Soma - https://jamii.app/Senegal2022

#AFCON2021 #JFMaarifa #JFSports
AUSTRALIA KUFUNGUA MIPAKA BAADA YA TAKRIBAN MIAKA MIWILI

Itafungua Mipaka kwa Wasafiri waliopata chanjo dhidi ya #COVID19 ifikapo Februari 21

#Australia ni miongoni mwa Nchi zilizoweka kanuni kali zaidi Mipakani kufuatia Mlipuko huo

Soma - https://jamii.app/MipakaAus

#UVIKO3
AU YAKEMEA WIMBI LA MAPINDUZI AFRIKA

Mkuu wa Baraza la Amani na Usalama, Bankole Adeoye asema hakuna wakati katika historia AU ilisimamisha Uanachama wa Mataifa manne ndani ya miezi 12

AU imesitisha Uanachama wa Burkina Faso, Mali, Guinea na Sudan

Soma https://jamii.app/AUCoupsAfrica

#Governance
RAIS SAMIA: KWA SERIKALI MAJI SI BIASHARA, NI HUDUMA

Akiwa Bunda, Mkoani Mara amesema, "Kwa Serikali ndoo moja ya maji ya lita 20 inauzwa kwa Tsh. 37. Wananchi mnaonunua maji ni mashahidi dumu moja la lita 20 mnanunua Tsh. 1,000 na kwenda mbele"

Soma - https://jamii.app/MajiWananchi

#JFSiasa