JamiiForums
52.9K subscribers
34.3K photos
2.43K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
DKT. TULIA ACKSON ACHAGULIWA KUWA SPIKA WA BUNGE

Aliyekuwa Naibu wa Spika wa Bunge amepata Kura za Wabunge wote 376 huku Wagombea wenzake nane wakiambulia 0

Dkt. Tulia (CCM) anaandika Historia ya kuwa Spika wa pili Mwanamke

Soma - https://jamii.app/DktTuliaSpika

#Democracy
MATUKIO 176 YA MAUAJI YARIPOTIWA NDANI YA MWAKA 1. SERIKALI YAUNDA KAMATI

Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni asema Mikoa inayoongoza ni Kagera, Dodoma, Tabora, Mara, Kigoma na Songwe

Kamati iliyoundwa yatakiwa kutoa taarifa baada ya siku 21

Soma - https://jamii.app/KamatiMauaji

#JFUwajibikaji #HumanRights
MIAMALA YA M-PESA YASHUKA KWA 24.8%

Vodacom imebainisha kushuka kwa miamala kwa robo ya mwisho ya mwaka 2021. Watumiaji wa M-Pesa wamepungua kwa 4.4%

> Tozo zilizowekwa zimetajwa kuwa chanzo cha kushuka kwa miamala

Soma https://jamii.app/MiamalaYashuka

#JFUchumi
IRINGA: MACHINGA WAGOMA KUHAMIA WALIPOPANGIWA. WASEMA ENEO SI RAFIKI

Wafanyabiashara wadogo wamegomea Uongozi wa Manispaa wakisema eneo ni dogo na si rafiki

Katibu wa Machinga Mkoa, Joseph Kilienyi amesema watagoma hadi wapatiwe maeneo rafiki

Soma - https://jamii.app/IringaMachinga

#JFBiashara
MDAU: EPUKA KUJITIBU MWENYEWE KWA KUTUMIA TAARIFA ZA MTANDAONI - 1

Anasema unapoona Changamoto yoyote Kiafya unapaswa kuwasiliana na Mtoa huduma wa Afya ili kupata ushauri au Matibabu

Lakini kutokana na Maendeleo ya Teknolojia, Watu wengi siku hizi hatupendi kufanya hivi na tunajiridhisha na majibu ya Mtandaoni na kutumia Dawa zinazopendekezwa

Tembelea - https://jamii.app/KujitibuMtandaoni

#JFAfya
MADHARA UNAYOWEZA KUPATA KWA KUTUMIA TAARIFA ZA MTANDAONI KUJITIBU

1. Hatari ya kutumia Dawa zisizo na ufanisi: Dawa zinatumika kutibu lakini zina madhara pale zinapotumika kinyume na utaratibu unaohitajika

2. Kudhani tatizo ni dogo kuliko uhalisia: Taarifa hizi zinaweza kufanya upuuze kumuona Daktari. Utaendelea kuugua Maradhi yaleyale na kuathirika zaidi.

Soma - https://jamii.app/KujitibuMtandaoni

#JFAfya
BALOZI WA SWEDEN AITEMBELEA JAMIIFORUMS

Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Anders Sjoberg leo Februari 1, 2022 ametembelea ofisi za JamiiForums na kukutana na watendaji na mwakilishi wa Bodi ya Wakurugenzi wa JF

> Ameweza kujua namna Jamii Forums inavyoendesha shughuli zake katika kuhakikisha inafanya uchechemuzi wa Haki za Kidijitali, Uwajibikaji, Demokrasia na Utawala Bora nchini Tanzania

#JamiiForums
BEI YA PETROLI YASHUKA, DIZELI YAPANDA

Bei ya Petroli na Mafuta ya Taa yaliyopokelewa kupitia Bandari ya Dar es Salaam zimepungua kwa Tsh. 21 na Tsh. 44 kwa Lita mtawalia huku Mafuta ya Dizeli yakipanda kwa Tsh. 13 kwa Lita

> Bei za rejareja za mafuta kwa Mikoa ya Kusini zimebaki zilivyo

Soma https://jamii.app/BeiEWURA

#JFUchumi
#COVID19: Denmark imeondoa masharti ya Uvaaji Barakoa kwenye Usafiri wa Umma, Madukani, kwenye Migahawa pamoja na amri ya kuonesha cheti cha Chanjo maeneo ya Burudani na Mapumziko

Maafisa wa Afya wasema idadi ya wagonjwa mahututi imepungua

Soma - https://jamii.app/VizuiziOffDen

#UVIKO3 #Governance
👍1
MABADILIKO YA KANUNI: CHANELI ZA KULIPIA RUKSA KURUSHA MATANGAZO YA KIBIASHARA

Ili kuboresha Huduma ya Mawasiliano nchini, Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imerekebisha baadhi ya kanuni za Leseni za mwaka 2018

Kuanzia sasa, chaneli za kulipia zitaruhusiwa kurusha matangazo ya kibiashara yasiyozidi dakika 5 kwa saa. Mabadiliko haya ni katika kanuni ya 16. Awali, chaneli za kulipia hazikuruhusiwa kuweka matangazo ya biashara

#JamiiForums #DigitalRights
ADA YA MASAFA YAFUTWA KWA WENYE MIUNDOMBINU YA UTANGAZAJI KIDIJITI

Marekebisho ya Kanuni ya Leseni ya mwaka 2018 imefuta ada ya masafa kwa wenye miundombinu ya utangazaji wa kidijiti (Multiplex Operators) ili kuleta unafuu kwa wawekezaji

Serikali imefanya hivyo ili kuchochea uanzishaji wa vituo vya utangazaji vya kijamii katika maeneo ambayo hayajafikiwa na redio. Leseni ya vituo vya utangazaji wa kijamii vinakuwa na leseni ndogo

#JamiiForums #DigitalRights
KIGOMA: Helman John (23) anatuhumiwa kumuua Mama yake Mzazi, Selina William (63) kwa kumpiga na mpini wa jembe. Kijana huyo alikuwa akimdai Mama yake Tsh. 300,000

Watu 10 wameuawa katika matukio tofauti Mkoani humo ndani ya Mwezi Januari

Soma - https://jamii.app/KigomaMauaji

#JFMatukio
RAIS SAMIA: KATIKA KUTOA MAAMUZI UTU WA MTU UTAZAMWE

Asema Mahakama inapaswa kuzingatia #Sheria ili kutenda Haki kwa wote bila kujali hali ya Mtu, Kijamii au Kiuchumi

Ameongeza "Kubwa kwa wewe unayetoa Haki ni kuisikiliza nafsi yako. Je, hapa natenda Haki au sitendi? Katika kutoa maamuzi Utu wa Mtu nao utazamwe"

Soma - https://jamii.app/SamiaHaki

#JFSheria
Rais Samia Suluhu Hassan amesema suala la Anuani za Makazi litakamilika kabla ya Sensa

> Kauli ya Rais inakuja baada ya Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Hamis Juma kuomba kukamilika kwa suala hilo akisema linarahisisha utoaji huduma za Mahakama

Soma https://jamii.app/AnuaniMakazi

#JFSheria
Spika wa Bunge la Tanzania, Dkt. Tulia Ackson amesema Wananchi hushiriki ktk kutunga Sheria

> Ameongeza kuwa Bunge linapopokea Muswada huita Wadau na kutoa tangazo la kuhitaji mawazo kutoka kwa Wananchi ambapo Wananchi hupata fursa ya kushiriki

Soma https://jamii.app/SheriaWananchi

#JFSheria
TABORA: Mwanafunzi wa Darasa la Nne, Maria Kazungu (13) ameuawa na kunyofolewa sehemu za siri huku masikio yakitobolewa na kitu chenye ncha kali

Ongezeko la matukio ya mauaji Nchini yameilazimu Serikali kuunda Kamati ya uchunguzi

Soma - https://jamii.app/MwanafunziTabora

#JFMatukio
BUNGENI: Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato asema hakutakuwa na makali ya mgao wa Umeme kama ilivyotarajiwa awali

Mgao wa Umeme ulitarajiwa kuanza Februari 1, 2022 kwa lengo la kufanya marekebisho ya Mitambo, hali iliyozua taharuki

Soma - https://jamii.app/MakaliMgaoUmeme

#ServiceDelivery