JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
BURKINA FASO: Jeshi la #BurkinaFaso limetangaza kurejesha #Katiba, wiki moja baada ya kutwaa Madaraka katika Taifa hilo la Ukanda wa Sahel

Tangazo hilo limetolewa katika mazungumzo na wapatanishi wa Kimataifa kutoka ECOWAS na UN

Soma - https://jamii.app/KatibaBurkinaFaso
#Democracy
BUNGENI: Waliyosema baadhi ya Wagombea wa nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Februari 01, 2022 wakati wakiomba kura kwa Wabunge

Wagombea tisa wanawania nafasi iliyoachwa wazi baada ya aliyekuwa Spika, Job Ndugai kujiuzulu

#Democracy
DKT. TULIA ACKSON ACHAGULIWA KUWA SPIKA WA BUNGE

Aliyekuwa Naibu wa Spika wa Bunge amepata Kura za Wabunge wote 376 huku Wagombea wenzake nane wakiambulia 0

Dkt. Tulia (CCM) anaandika Historia ya kuwa Spika wa pili Mwanamke

Soma - https://jamii.app/DktTuliaSpika

#Democracy
MATUKIO 176 YA MAUAJI YARIPOTIWA NDANI YA MWAKA 1. SERIKALI YAUNDA KAMATI

Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni asema Mikoa inayoongoza ni Kagera, Dodoma, Tabora, Mara, Kigoma na Songwe

Kamati iliyoundwa yatakiwa kutoa taarifa baada ya siku 21

Soma - https://jamii.app/KamatiMauaji

#JFUwajibikaji #HumanRights
MIAMALA YA M-PESA YASHUKA KWA 24.8%

Vodacom imebainisha kushuka kwa miamala kwa robo ya mwisho ya mwaka 2021. Watumiaji wa M-Pesa wamepungua kwa 4.4%

> Tozo zilizowekwa zimetajwa kuwa chanzo cha kushuka kwa miamala

Soma https://jamii.app/MiamalaYashuka

#JFUchumi
IRINGA: MACHINGA WAGOMA KUHAMIA WALIPOPANGIWA. WASEMA ENEO SI RAFIKI

Wafanyabiashara wadogo wamegomea Uongozi wa Manispaa wakisema eneo ni dogo na si rafiki

Katibu wa Machinga Mkoa, Joseph Kilienyi amesema watagoma hadi wapatiwe maeneo rafiki

Soma - https://jamii.app/IringaMachinga

#JFBiashara
MDAU: EPUKA KUJITIBU MWENYEWE KWA KUTUMIA TAARIFA ZA MTANDAONI - 1

Anasema unapoona Changamoto yoyote Kiafya unapaswa kuwasiliana na Mtoa huduma wa Afya ili kupata ushauri au Matibabu

Lakini kutokana na Maendeleo ya Teknolojia, Watu wengi siku hizi hatupendi kufanya hivi na tunajiridhisha na majibu ya Mtandaoni na kutumia Dawa zinazopendekezwa

Tembelea - https://jamii.app/KujitibuMtandaoni

#JFAfya
MADHARA UNAYOWEZA KUPATA KWA KUTUMIA TAARIFA ZA MTANDAONI KUJITIBU

1. Hatari ya kutumia Dawa zisizo na ufanisi: Dawa zinatumika kutibu lakini zina madhara pale zinapotumika kinyume na utaratibu unaohitajika

2. Kudhani tatizo ni dogo kuliko uhalisia: Taarifa hizi zinaweza kufanya upuuze kumuona Daktari. Utaendelea kuugua Maradhi yaleyale na kuathirika zaidi.

Soma - https://jamii.app/KujitibuMtandaoni

#JFAfya
BALOZI WA SWEDEN AITEMBELEA JAMIIFORUMS

Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Anders Sjoberg leo Februari 1, 2022 ametembelea ofisi za JamiiForums na kukutana na watendaji na mwakilishi wa Bodi ya Wakurugenzi wa JF

> Ameweza kujua namna Jamii Forums inavyoendesha shughuli zake katika kuhakikisha inafanya uchechemuzi wa Haki za Kidijitali, Uwajibikaji, Demokrasia na Utawala Bora nchini Tanzania

#JamiiForums
BEI YA PETROLI YASHUKA, DIZELI YAPANDA

Bei ya Petroli na Mafuta ya Taa yaliyopokelewa kupitia Bandari ya Dar es Salaam zimepungua kwa Tsh. 21 na Tsh. 44 kwa Lita mtawalia huku Mafuta ya Dizeli yakipanda kwa Tsh. 13 kwa Lita

> Bei za rejareja za mafuta kwa Mikoa ya Kusini zimebaki zilivyo

Soma https://jamii.app/BeiEWURA

#JFUchumi
#COVID19: Denmark imeondoa masharti ya Uvaaji Barakoa kwenye Usafiri wa Umma, Madukani, kwenye Migahawa pamoja na amri ya kuonesha cheti cha Chanjo maeneo ya Burudani na Mapumziko

Maafisa wa Afya wasema idadi ya wagonjwa mahututi imepungua

Soma - https://jamii.app/VizuiziOffDen

#UVIKO3 #Governance
👍1
MABADILIKO YA KANUNI: CHANELI ZA KULIPIA RUKSA KURUSHA MATANGAZO YA KIBIASHARA

Ili kuboresha Huduma ya Mawasiliano nchini, Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imerekebisha baadhi ya kanuni za Leseni za mwaka 2018

Kuanzia sasa, chaneli za kulipia zitaruhusiwa kurusha matangazo ya kibiashara yasiyozidi dakika 5 kwa saa. Mabadiliko haya ni katika kanuni ya 16. Awali, chaneli za kulipia hazikuruhusiwa kuweka matangazo ya biashara

#JamiiForums #DigitalRights
ADA YA MASAFA YAFUTWA KWA WENYE MIUNDOMBINU YA UTANGAZAJI KIDIJITI

Marekebisho ya Kanuni ya Leseni ya mwaka 2018 imefuta ada ya masafa kwa wenye miundombinu ya utangazaji wa kidijiti (Multiplex Operators) ili kuleta unafuu kwa wawekezaji

Serikali imefanya hivyo ili kuchochea uanzishaji wa vituo vya utangazaji vya kijamii katika maeneo ambayo hayajafikiwa na redio. Leseni ya vituo vya utangazaji wa kijamii vinakuwa na leseni ndogo

#JamiiForums #DigitalRights