JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MSUMBIJI: KIONGOZI WA WANAMGAMBO ANAYEDAIWA NI MTANZANIA AUAWA

> Tuahil Muhidim aliyeuawa Januari 30 anadaiwa kuongoza mashambulizi na kuushikilia mji wa Macimboa da Pria mwaka 2020

> Pia, anadaiwa kuteka Watawa 2 wa Kibrazili kwa wiki zaidi ya 3

Soma https://jamii.app/KiongoziWanamgambo

#JFMatukio
BUNGENI: UCHAGUZI WA SPIKA KUFANYWA LEO

Wagombea ni Dkt. Tulia Ackson, Abdulla Mohammed Said, Mhandisi Aivan Jackson Maganza, David Mwaijolele, George Gabriel Bussungu, Kunje Ngombale Mwiru, Maimuna Kassim, Ndonge Ndonge na Saidoun Abrahaman Khatib

Soma https://jamii.app/Uspika2022

#Democracy
DKT. TULIA ACKSON AJIUZULU NAFASI YA NAIBU SPIKA

Dkt. Tulia Ackson amejiuzulu nafasi ya Naibu Spika baada ya kuteuliwa na Chama cha CCM kugombea nafasi ya Uspika

Taarifa ya kujiuzulu imetolewa na Katibu wa Bunge mbele ya Wabunge leo kwenye zoezi la Uchaguzi wa Spika

#Democracy
UTEUZI: Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Zuhura Yunus Abdallah kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais - Ikulu, akichukua nafasi ya Jaffar Haniu ambaye atapangiwa kazi nyingine

Yunus alikuwa Mtayarishaji wa Vipindi na Mtangazaji wa BBC

Soma - https://jamii.app/ZuhuraIkulu

#Governance
BURKINA FASO: Jeshi la #BurkinaFaso limetangaza kurejesha #Katiba, wiki moja baada ya kutwaa Madaraka katika Taifa hilo la Ukanda wa Sahel

Tangazo hilo limetolewa katika mazungumzo na wapatanishi wa Kimataifa kutoka ECOWAS na UN

Soma - https://jamii.app/KatibaBurkinaFaso
#Democracy
BUNGENI: Waliyosema baadhi ya Wagombea wa nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Februari 01, 2022 wakati wakiomba kura kwa Wabunge

Wagombea tisa wanawania nafasi iliyoachwa wazi baada ya aliyekuwa Spika, Job Ndugai kujiuzulu

#Democracy
DKT. TULIA ACKSON ACHAGULIWA KUWA SPIKA WA BUNGE

Aliyekuwa Naibu wa Spika wa Bunge amepata Kura za Wabunge wote 376 huku Wagombea wenzake nane wakiambulia 0

Dkt. Tulia (CCM) anaandika Historia ya kuwa Spika wa pili Mwanamke

Soma - https://jamii.app/DktTuliaSpika

#Democracy
MATUKIO 176 YA MAUAJI YARIPOTIWA NDANI YA MWAKA 1. SERIKALI YAUNDA KAMATI

Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni asema Mikoa inayoongoza ni Kagera, Dodoma, Tabora, Mara, Kigoma na Songwe

Kamati iliyoundwa yatakiwa kutoa taarifa baada ya siku 21

Soma - https://jamii.app/KamatiMauaji

#JFUwajibikaji #HumanRights
MIAMALA YA M-PESA YASHUKA KWA 24.8%

Vodacom imebainisha kushuka kwa miamala kwa robo ya mwisho ya mwaka 2021. Watumiaji wa M-Pesa wamepungua kwa 4.4%

> Tozo zilizowekwa zimetajwa kuwa chanzo cha kushuka kwa miamala

Soma https://jamii.app/MiamalaYashuka

#JFUchumi
IRINGA: MACHINGA WAGOMA KUHAMIA WALIPOPANGIWA. WASEMA ENEO SI RAFIKI

Wafanyabiashara wadogo wamegomea Uongozi wa Manispaa wakisema eneo ni dogo na si rafiki

Katibu wa Machinga Mkoa, Joseph Kilienyi amesema watagoma hadi wapatiwe maeneo rafiki

Soma - https://jamii.app/IringaMachinga

#JFBiashara
MDAU: EPUKA KUJITIBU MWENYEWE KWA KUTUMIA TAARIFA ZA MTANDAONI - 1

Anasema unapoona Changamoto yoyote Kiafya unapaswa kuwasiliana na Mtoa huduma wa Afya ili kupata ushauri au Matibabu

Lakini kutokana na Maendeleo ya Teknolojia, Watu wengi siku hizi hatupendi kufanya hivi na tunajiridhisha na majibu ya Mtandaoni na kutumia Dawa zinazopendekezwa

Tembelea - https://jamii.app/KujitibuMtandaoni

#JFAfya
MADHARA UNAYOWEZA KUPATA KWA KUTUMIA TAARIFA ZA MTANDAONI KUJITIBU

1. Hatari ya kutumia Dawa zisizo na ufanisi: Dawa zinatumika kutibu lakini zina madhara pale zinapotumika kinyume na utaratibu unaohitajika

2. Kudhani tatizo ni dogo kuliko uhalisia: Taarifa hizi zinaweza kufanya upuuze kumuona Daktari. Utaendelea kuugua Maradhi yaleyale na kuathirika zaidi.

Soma - https://jamii.app/KujitibuMtandaoni

#JFAfya
BALOZI WA SWEDEN AITEMBELEA JAMIIFORUMS

Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Anders Sjoberg leo Februari 1, 2022 ametembelea ofisi za JamiiForums na kukutana na watendaji na mwakilishi wa Bodi ya Wakurugenzi wa JF

> Ameweza kujua namna Jamii Forums inavyoendesha shughuli zake katika kuhakikisha inafanya uchechemuzi wa Haki za Kidijitali, Uwajibikaji, Demokrasia na Utawala Bora nchini Tanzania

#JamiiForums