JamiiForums
βœ”
54K subscribers
34.1K photos
2.26K videos
31K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
DKT. TULIA APITISHWA KUWA MGOMBEA WA USPIKA

Dkt. Tulia Ackson ambaye amekuwa akihudumu kama Naibu Spika wa Bunge amepitishwa na Kamati Kuu ya CCM kuwa Mgombea wa nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Soma - https://jamii.app/DktTuliaUspika

#Democracy #Governance
MASHIRIKA YA NDEGE YAHOFIA ATHARI ZA 5G KWENYE MAWASILIANO YA NDEGE

Jana, Januari 19, 2022 huduma ya Mtandao wa 5G ilianza kutumika Nchini Marekani kwa kuwashwa Minara 4500 ambayo inadaiwa inaweza kuathiri mawasiliano ya Ndege za #Boeing777

Mashirika makubwa ikiwemo Emirates, Air India, All Nippon Airways, Japan Airlines, Lufthansa na British Airways yamesitisha safari zake

Soma - https://jamii.app/5GVsAirlines

#5GTechnology #JFTech
MJADALA: NI UMRI GANI SAHIHI WA KUACHA KUMCHAPA MTOTO?

Katika Malezi Wazazi hukutana na changamoto nyingi hasa pale Mtoto anapokuwa mtovu wa Nidhamu. Mbinu mbalimbali hutumika ili kumuweka sawa ikiwemo Viboko

Je, ni wakati gani au umri gani wa kuacha kumpiga/kumchapa Mtoto anapokosea?

Mjadala zaidi - https://jamii.app/KuchapaMtoto

#JFMalezi #Parenthood
#AFCON2021: BINGWA MTETEZI, ALGERIA ATOLEWA

#TeamAlgeria imetolewa kwa kufungwa goli 3-1 na #TeamCotedIvoire katika mchezo wa mwisho wa kundi

Equatorial Guinea imeifunga #TeamSierraLeone goli 1-0

Cote d’Ivoire na #TeamEquatorialGuinea zafuzu kucheza hatua ya mtoano

#JFSports
#LIBERIA: WATU 29 WAFARIKI KWENYE MKANYAGANO WA MAOMBI

Polisi wasema vifo huenda vikaongezeka kwasababu baadhi ya waliojeruhiwa wana hali mbaya

Mchungaji Abraham Kromah aliandaa kusanyiko la Maombi la Siku 2 lililofanyika ktk Uwanja wa Mpira

Soma https://jamii.app/29DeadStampede

#JFMatukio
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema inakadiriwa Watanzania milioni 1.7 wanaishi na Virusi vya UKIMWI huku 12% kati yao wakiwa hawatambui hali zao

Kati ya wanaotambua hali zao, 98% wanatumia Dawa na 92% wamefanikiwa kufubaza makali ya virusi

Soma https://jamii.app/VVUTanzania

#JFAfya
SUDAN: MAJAJI WAKEMEA MAUAJI YA WAANDAMANAJI

Majaji na Waendesha Mashtaka kadhaa wamekemea mauaji ya Waandamanaji wapatao 70 tangu Jeshi kuchukua Madaraka

Wametoa rai ya kumaliza ghasia hizo zilizopelekea zaidi ya watu 2,000 kujeruhiwa

Soma - https://jamii.app/VifoSudan

#Democracy #HumanRights
#COVID19: Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa (CDC) Afrika kimetaka Chanjo zinazotolewa kuwa na muda wa matumizi kati ya miezi 3 hadi 6 ili Mataifa yaweze kupanga usambazaji kikamilifu

10.4% ya Waafrika wameshapata Chanjo kikamilifu

Soma - https://jamii.app/CDCMudaChanjo

#UVIKO3 #JFAfya
DEMOKRASIA NA MIFUMO YA UWAJIBIKAJI

#Demokrasia ni nguvu ya wengi katika kufanya maamuzi yanayohusu Umma na kuweka usawa wa Kisiasa katika matumizi ya nguvu hiyo. Ni lazima iwape Wananchi uwezo wa kujieleza na kuwasilisha hoja zao

Kuwepo kwa Mifumo ya #Uwajibikaji katika Demokrasia ni kuhakikisha Maafisa wa Serikali wanatoa huduma kwa Watu, vinginevyo wanawajibishwa ipasavyo ikiwa hawatafanya hivyo

Soma - https://jamii.app/DemocracyAccountability

#Democracy #Accountability
MATUKIO YA UKATILI WA KIJINSIA YAMEKITHIRI, HATUA ZICHUKULIWE

Mdau wa JamiiForums.com anashauri kuwepo Agenda Maalum za kupambana na tatizo hili kwani Ukatili dhidi ya Wanawake, Wanaume na hata Watoto unafanyika kila siku

Anasema tunapaswa kulipokea jambo hili kama janga la Taifa

Soma - https://jamii.app/UkatiliJamii

#StoriesOfChange #UkatiliKijinsia
SABABU ZINAZOPELEKEA WATU KUAMUA KUJIUA

1. Matatizo ya Afya ya Akili: Watu wengi hufanya maamuzi ya kujaribu kujiua baada ya kupatwa na Msongo wa Mawazo au Sonona

2. Kupitia Matukio mabaya: Mtu ambaye amepitia matukio mabaya ikiwemo Ukatili Utotoni, Ubakaji, Unyanyasaji wa kimwili au Vita yuko katika hatari kubwa ya kujiua, hata miaka mingi baada ya tukio hilo

Soma - https://jamii.app/ReasonsSuicide

#MentalHealth #SuicideAttempts
MICHEZO: Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Duniani limewavua Mikanda ya Ubingwa wa WBF Intercontinental Mabondia wa Tanzania, Hassan Mwakinyo (Champez) na Ibrahim Class kutokana na kutotetea mikanda hiyo kwa muda mrefu kama sheria za WBF zilivyo

Soma https://jamii.app/MwakinyoNoWBF

#JFSports
TCRA YAAGIZWA KUELEKEZA KAMPUNI ZA MAWASILIANO KUSITISHA BEI MPYA ZA VIFURUSHI

Waziri wa Habari amesema "Kuna gharama kidogo zimeongezeka kwa baadhi ya Mitandao ya Simu. Tunataka Mawasiliano yawe rahisi, bora na kisasa"

Asema Serikali inatambua pengine ni mahitaji ya Soko, lakini kasi ya kuongeza gharama hizo isiwe kubwa

Soma - https://jamii.app/NapeBeiVifurushi

#DigitalRights
MDAU: MITANDAO NI KICHOCHEO KIPYA CHA DEMOKRASIA NA MABADILIKO

Mshiriki wa #StoriesOfChange anasema baadhi ya taarifa ambazo zimesaidia Serikali, Vyama vya Siasa, Asasi za Kiraia, Mashirika ya Dini na Makundi mbalimbali ya Jamii kuchukua hatua zilianzia Mitandaoni

Anashauri Mitandao ya kijamii itumike vizuri, na uwekezaji mkubwa ufanyike kwenye Teknolojia ili kuwafikia wengi zaidi

Soma - https://jamii.app/MitandaoSOC

#Democracy
IRINGA: ASKARI ASHIKILIWA NA TAKUKURU KWA RUSHWA

Taratibu za kumfikisha Mahakamani Koplo Steven Philimoni Mchomvu ambaye picha zake zimesambaa Mitandaoni zinaendelea

Askari huyo wa Usalama Barabarani alikamatwa akipokea Rushwa inayofikia Tsh. 152,000 kutoka kwenye Magari

Soma - https://jamii.app/PCCBAskari

#KemeaRushwa #JFUwajibikaji
MUTAHABA: WANAFUNZI KUTOWAPENDA WALIMU WA HESABU HUCHANGIA KUFELI

Kamishna wa Elimu, Dkt. Lyabwene Mutahaba, amesema sababu nyingine ya Wanafunzi kufanya vibaya ni mazingira ya ufundishaji kutokuwa rafiki

Amefafanua, "Baadhi ya Shule Mwalimu akitoa Hesabu 10 anakuwa na mzigo wa fimbo. Mwanafunzi atakayekosa Hesabu 5 atachapwa viboko 5, akikosa 3 atachapwa fimbo 3"

Soma - https://jamii.app/KufeliHisabati

#JFElimu
MVUA ZAATHIRI MIUNDOMBINU YA UMEME

Upepo mkali na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali Nchini zimeathiri Miundombinu ya Umeme

Shirika la Umeme lasema hali hiyo imepelekea baadhi ya watu kukosa huduma ya umeme kwa nyakati tofauti

Soma - https://jamii.app/TZMvuaUmeme
RAIS SAMIA: SERIKALI ITASHIRIKIANA NA MACHIFU

Akishiriki Tamasha la Utamaduni amesema, "Kumekuwa na maneno mengi kuhusu Serikali na Uchifu. Tumeamua kuwa na jukwaa la pamoja baina ya Serikali, Machifu na Wazee wa Kimila ili kuhifadhi Desturi zetu"

Soma - https://jamii.app/SerikaliMachifu

#JFSiasa
ARUSHA: MKE WA MTU ADAIWA KUULIWA NA MCHEPUKO WAKE

Mwili wa Teddy Mallya umekutwa umetupwa ktk Shamba la Migomba ukiwa na majeraha ikiwemo ya kung’atwa

Emmanuel Lazaro anadaiwa kutekeleza mauaji hayo akimtuhumu marehemu kutoa ujauzito wake

Soma - https://jamii.app/MkeKifoHawara

#GBV #UkatiliKijinsia #JFMatukio