JamiiForums
53.7K subscribers
34.2K photos
2.32K videos
31.1K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
#AFCON2021: HATUA YA MTOANO KUENDELEA KESHO

Hatua ya makundi ya michuano hiyo inayofanyika Cameroon imemalizika Januari 20, 2021.

Timu 16 zilizofuzu kucheza hatua ya mtoano zitaendelea na michuano kesho.

Je, ni timu gani unaipa nafasi ya kuweza kuondoka na Kombe?

#JFSports
UTURUKI: Polisi Nchini humo wanamshikilia Mwanahabari Sedef Kabas kwa madai ya kumtusi Rais Recep Tayyip Erdogan kwenye Runinga na #Twitter

Kumtusi Rais ni uhalifu Nchini Uturuki na huenda ukasababisha kifungo cha miaka minne jela.

Soma - https://jamii.app/KabasArrested

#PressFreedom
DODOMA: WATU WATANO WA FAMILIA MOJA WAUAWA

Waliouawa ni Mume, Mke, Watoto wawili na Mjukuu mmoja ambao ni Wakazi wa kijiji cha Zanka wilayani Bahi

Kamanda wa Polisi Mkoani humo, Onesmo Lyanga amesema miili yao inafanyiwa Uchunguzi

Soma - https://jamii.app/Vifo5Dodoma

#JFMatukio
YAOUNDE, CAMEROON: MOTO WAUA TAKRIBAN WATU 16 NA KUJERUHI 8

Serikali imesema Ripoti ya Awali inaonesha moto ulisababishwa na milipuko ya fataki ambazo mara nyingi zinatumika maeneo hayo

Milipuko hiyo ilipelekea hofu na mkanyagano

Soma - https://jamii.app/NightClubFire

#JFMatukio
#AFCON2021: BURKINA FASO YAFUZU KUINGIA ROBO FAINALI

- #TeamBurkinaFaso imefanikiwa kuingia hatua ya robo fainali kwenye michuano hiyo baada ya kuifunga #TeamGabon kwa mikwaju ya penati 7-6

- Timu hizo zilimaliza dakika 120 za mchezo zikiwa zimefungana goli 1-1

#JFSports
BURKINA FASO: Waziri wa Ulinzi, Aime Barthelemy amesema Rais wa Nchi hiyo, Rorch Marc Christian Kabore hayuko kizuizini

> Amekiri uwepo wa ghasia ktk kambi za Jeshi ambapo milio ya risasi imesikika. Pia, Wananchi waliandamana kutaka Rais ajiuzulu

Soma https://jamii.app/BurkinaFasoMapinduzi

#Governance
ARMENIA: RAIS AJIUZULU AKISEMA KATIBA HAIMPI MAMLAKA YA KUTOSHA

Rais Armen Sarkissian amewasilisha maombi ya kujiuzulu akisema anaamini Katiba haimpi madaraka ya kutosha kushawishi matukio

Nafasi ya Waziri Mkuu inaonekana kuwa kubwa kuliko ya Rais

Soma https://jamii.app/SarkissianResigns

#Governance
Siku ya Kimataifa ya Elimu huadhimishwa kila Januari 24. Kwa mujibu wa Takwimu za Umoja wa Mataifa, hivi leo Watoto na Vijana Milioni 258 hawaendi Shule

Pasipo Elimu Bora, Nchi hazitofanikiwa kufikia Usawa wa Kijinsia na kupiga vita umasikini ambao unawaacha nyuma Mamilioni ya Watoto, Vijana na Watu wazima

Soma - https://jamii.app/WorldEduDay

#EducationDay #JFElimu
#AFGHANISTAN: Wajumbe wa Taliban wamepanga kukutana na Maafisa wa Nchi za Magharibi, leo Januari 24 kuomba Fedha zilizofichwa ktk Benki za Marekani

Baadhi ya Wanaharakati wamefanya maandamano kupinga hatua ya #Taliban kupewa nafasi ya mazungumzo

Soma - https://jamii.app/TalibanMazungumzo

#Governance
REUTERS YARIPOTI RAIS WA BURKINA FASO KUSHIKILIWA NA JESHI

Taarifa ya kushikiliwa kwa Rais Kabore inakuja saa kadhaa baada ya Waziri wa Ulinzi kukanusha tukio hilo

Magari ya msafara wa Rais yadaiwa kuonekana na alama za risasi na Damu

Soma - https://jamii.app/RaisBurkinaFaso

#Democracy
TCRA YAZUIA KIPINDI CHA EFATHA KWA MIEZI MITATU

Kamati ya Maudhui ya TCRA imesema Kituo cha Star TV kimeonesha uzembe na udhaifu katika kusimamia kipindi cha EFATHA Ministries kwa kuruhusu maudhui yenye ukakasi, kinyume na Kanuni za Mawasiliano

Star TV yapewa onyo na kuamriwa kuomba radhi kwa siku tatu mfululizo

Soma - https://jamii.app/EFATHA-TCRA

#DigitalRights
WAZIRI UMMY: MADUKA YA DAWA YALIYO NDANI YA MITA 500 ZA HOSPITALI KUONDOLEWA

Asema yapo kinyume cha Sheria, akihoji "Hospitali Dawa hakuna lakini kwenye Maduka ya Nje zipo"

Ni siku chache baada ya Wadau ndani ya JamiiForums.com kusema yanachangia kukosekana kwa Dawa Hospitalini

Soma https://jamii.app/MadukaDawa

#JFAfya
UHOLANZI: Polisi Nchini humo wamemkuta Mtu mmoja akiwa hai ktk Uwanja wa Ndege wa #Amsterdam ambapo alijibanza kwenye Tairi la mbele

Safari kutoka Afrika Kusini hadi Amsterdam huchukua Saa 11 ambapo Ndege hupumzika kwa Saa 1 #Nairobi, Kenya

Soma - https://jamii.app/MzamiajiAmsterdam

#JFMatukio
ELIMU YA SARATANI ITOLEWE KWA WATANZANIA

Mshiriki wa #StoriesOfChange anasema hapa Nchini, watu wachache tu ndiyo wana Elimu sahihi kuhusu visababishi na Matibabu ya Saratani

Anasema watu waishio maeneo ya Vijijini na yasiyo na Huduma nzuri za Afya wanapata Elimu hiyo wakishapata Ugonjwa, jambo ambalo haliwasaidii

Anashauri Serikali na wadau wengine kuweka kipaumbele kwenye suala hili

Soma - https://jamii.app/CancerSOC

#JFAfya
ATHARI ZA COVID-19 KWENYE SEKTA YA ELIMU

#CoronaVirus imeathiri Sekta ya Elimu Duniani kote, na masomo ya takriban Wanafunzi Bilioni 1.6 wa Shule na Vyuo yaliathiriwa mwanzoni mwa mlipuko huo

Watoto kutoka Familia za chini hawakupata nafasi ya kuendelea na Masomo yao kama wengine kutokana na changamoto za Umeme na Vifaa vya kielektroniki

Soma - https://jamii.app/WorldEduDay

#EducationDay #JFElimu
ISRAEL YADHIBITI #OMICRON BAADA YA KUTOA DOZI YA NNE

Wizara ya #Afya ya Israel imesema Watu wenye umri wa miaka 60 na kuendelea waliopata Chanjo ya nne wameonesha kuwa na kinga ya Ugonjwa mara tatu zaidi kuliko wale waliopata Dozi tatu

Soma - https://jamii.app/DoziYaNne

#UVIKO3 #JFAfya
DAR: Mkuu wa Mkoa, Amos Makalla amesema Kamati imebaini Moto uliounguza Soko la Karume ulisababishwa na mshumaa uliowasha na mateja wanaojihifadhi katika vibanda

Wafanyabiashara wameruhusiwa kurejea na Serikali imeweka mpango mzuri kuzuia Moto

Soma - https://jamii.app/MatejaMoto

#JFMatukio
MWANZA: WALIOHUSIKA NA MAUAJI YA WATU WATATU WA FAMILIA MOJA WAKAMATWA

Jeshi la Polisi limesema waliokamatwa wamekiri kufanya mauaji chanzo kikiwa migogoro ya kibiashara

> Panga lililotumika kwa mauaji lipo kwa mkemia ili kupimwa vinasaba

Soma https://jamii.app/MauajiMwanza

#JFMatukio
TOZO ZA SIMU NI KIKWAZO KWA UCHUMI WA KIDIGITALI NCHINI

Mshiriki wa Stories of Change anasema Serikali imeweka Tozo ili kupata Fedha lakini gharama zitashindwa kuwavutia Watu zaidi hivyo Uchumi wa Kidigitali unaweza kuporomoka

Soma - https://jamii.app/TozoDigitali

#StoriesOfChange #DigitalRights
BURKINA FASO: JESHI LAMPINDUA RAIS KABORE. LASIMAMISHA KATIBA NA KUVUNJA SERIKALI

Mbali na Rais Roch Kabore kupinduliwa, Jeshi pia limesema Bunge limevunjwa na Mipaka ya Nchi imefungwa

Jeshi limesisitiza Mchakato huo umefanyika bila ghasia

Soma - https://jamii.app/KaboreOusted

#Democracy #Governance