JamiiForums
βœ”
55.4K subscribers
33.4K photos
2.04K videos
30.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema Serikali itatekeleza uwekaji wa mfumo wa anwani za makazi kwa Miezi 5 badala ya Miaka 5

Lengo ni kuboresha Mawasiliano katika sehemu mbalimbali ikiwemo makazi, sehemu za biashara na huduma za kijamii

Soma - https://jamii.app/MfumoAnwani

#Governance
UINGEREZA YALEGEZA KANUNI ZA #COVID19

Barakoa hazitokuwa lazima maeneo ya Umma na Shule. Raia hawataendelea kusisitizwa kufanya kazi Nyumbani

Wanasayansi wanaamini Wimbi la maambukizi yaliyotokana na Kirusi cha #Omicron limefikia kilele

Soma - https://jamii.app/KanuniCoronaUK

#UVIKO3 #Governance #JFAfya
AFGHANISTAN: RAIA ZAIDI YA LAKI 5 WAPOTEZA AJIRA SABABU YA TALIBAN

Shirika la Kazi Duniani (ILO) limesema idadi ya ajira zilizopotea huenda zikafikia Laki tisa ifikiapo katikati ya 2022

Makundi athirika ni Wanajeshi, Majaji na Wanawake

Soma - https://jamii.app/ILOAjiraAfghan

#HumanRights
KAZAKHSTAN: WAZIRI WA ULINZI ATIMULIWA KUTOKANA NA GHASIA

Rais Kassym-Jomart Tokayev amemtuhumu Murat Bektanov kutosimama ktk nafasi yake Nchi ilipopata ghasia

Rais alilazimika kuomba Wanajeshi wa Sovieti wakiongozwa na Urusi ili kutuliza ghasia

Soma - https://jamii.app/BektanovRemoved

#Governance
MAREKANI: Mahakama yakataa ombi la Donald Trump la kuzuia kutolewa rekodi za White House kwa jopo linalochunguza vurugu zilizotokea eneo la Bunge

Wafuasi wake walikusanyika kujaribu kusimamisha uidhinishaji wa matokeo ya Uchaguzi wa Urais 2020

Soma - https://jamii.app/TrumpMahakama

#Accountability
ALGERIA: SHULE ZAFUNGWA KUDHIBITI MAAMBUKIZI YA CORONA

Serikali imezifunga Shule kwa muda wa siku 10 na kuimarisha upimaji katika Viwanja vya Ndege kufuatia ongezeko la maambukizi

Wananchi wahimizwa kupata Chanjo ili kupambana na #COVID19

Soma https://jamii.app/COVIDAlgeria

#UVIKO3 #Governance #JFElimu
UMUHIMU WA KUWA NA SHERIA YA ULINZI WA DATA

Maendeleo ya Teknolojia yanaweza kuathiri Ulinzi wa Data Binafsi za Watu, hivyo uwepo wa Sheria hii utawalinda dhidi ya athari zinazoweza kujitokeza

Itahakikisha Haki ya Faragha inasimamiwa na kutekelezwa kwa vitendo kama ilivyoandikwa kwenye Katiba ya Tanzania

Soma - https://jamii.app/UlinziDataTZ

#DataProtection #DigitalRights
MDAU: KIONGOZI NI KIUNGO. ANAPASWA KUWA NA HEKIMA NA ULIMI WENYE STAHA

Kiongozi bora ni kuwa na Ubongo wenye Hekima, unaowaza, kuainisha, kuchambua, na kuweza kufanya tathmini. Awe na kinywa chenye maneno ya uhakika, weledi na nasaha bora

Aghalabu Vitu hivyo vikichagizwa na Kifua kilicho na Moyo wa Wema, Utu na Busara, pasipo na shaka Haki, Umoja, Upendo, Amani vitatamalaki katika Taifa

Soma zaidi - https://jamii.app/StahaKiongozi

#StoriesOfChange #Governance
'SERVER' ZA MSALABA MWEKUNDU ZADUKULIWA. TAARIFA ZA MAELFU ZAATHIRIWA

Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) imesema Taarifa Binafsi za Watu zaidi ya 500,000 zimeathiriwa ktk shambulio hilo, na waliohusika hawajajulikana

Soma - https://jamii.app/ICRCHacked

#DataProtection #DigitalRights
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum imetoa siku 30 hadi Februari 18, 2022 kwa Makao ya watoto yasiyo na leseni kuwasilisha maombi ya usajili

Hadi kufikia Januari 2022, Makao ya Watoto 244 kati ya 473 ndiyo yaliyokidhi vigezo na kupata leseni huku Makao 229 yakiendeshwa kinyume cha taratibu

Soma - https://jamii.app/UsajiliMakaoWtt

#ChildSafety #HakiMtoto
NAFASI YA VYOMBO HURU VYA HABARI KATIKA MAENDELEO YA JAMII

Mdau wa JamiiForums anasema Vyombo vya Habari vinapokuwa Huru vitaweza kuandaa Mijadala ya wazi ya Kimaendeleo bila kuogopa kuchokoza upande wowote kihoja

Wanahabari wataweza kuandaa mijadala ya kisiasa, kuhoji na kutoa mtazamo bila hofu, na hivyo kupatikana suluhisho ya matatizo ya Wananchi

Msome - https://jamii.app/HabariUhuruSOC

#StoriesOfChange #PressFreedom
DKT. TULIA APITISHWA KUWA MGOMBEA WA USPIKA

Dkt. Tulia Ackson ambaye amekuwa akihudumu kama Naibu Spika wa Bunge amepitishwa na Kamati Kuu ya CCM kuwa Mgombea wa nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Soma - https://jamii.app/DktTuliaUspika

#Democracy #Governance
MASHIRIKA YA NDEGE YAHOFIA ATHARI ZA 5G KWENYE MAWASILIANO YA NDEGE

Jana, Januari 19, 2022 huduma ya Mtandao wa 5G ilianza kutumika Nchini Marekani kwa kuwashwa Minara 4500 ambayo inadaiwa inaweza kuathiri mawasiliano ya Ndege za #Boeing777

Mashirika makubwa ikiwemo Emirates, Air India, All Nippon Airways, Japan Airlines, Lufthansa na British Airways yamesitisha safari zake

Soma - https://jamii.app/5GVsAirlines

#5GTechnology #JFTech
MJADALA: NI UMRI GANI SAHIHI WA KUACHA KUMCHAPA MTOTO?

Katika Malezi Wazazi hukutana na changamoto nyingi hasa pale Mtoto anapokuwa mtovu wa Nidhamu. Mbinu mbalimbali hutumika ili kumuweka sawa ikiwemo Viboko

Je, ni wakati gani au umri gani wa kuacha kumpiga/kumchapa Mtoto anapokosea?

Mjadala zaidi - https://jamii.app/KuchapaMtoto

#JFMalezi #Parenthood
#AFCON2021: BINGWA MTETEZI, ALGERIA ATOLEWA

#TeamAlgeria imetolewa kwa kufungwa goli 3-1 na #TeamCotedIvoire katika mchezo wa mwisho wa kundi

Equatorial Guinea imeifunga #TeamSierraLeone goli 1-0

Cote d’Ivoire na #TeamEquatorialGuinea zafuzu kucheza hatua ya mtoano

#JFSports
#LIBERIA: WATU 29 WAFARIKI KWENYE MKANYAGANO WA MAOMBI

Polisi wasema vifo huenda vikaongezeka kwasababu baadhi ya waliojeruhiwa wana hali mbaya

Mchungaji Abraham Kromah aliandaa kusanyiko la Maombi la Siku 2 lililofanyika ktk Uwanja wa Mpira

Soma https://jamii.app/29DeadStampede

#JFMatukio
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema inakadiriwa Watanzania milioni 1.7 wanaishi na Virusi vya UKIMWI huku 12% kati yao wakiwa hawatambui hali zao

Kati ya wanaotambua hali zao, 98% wanatumia Dawa na 92% wamefanikiwa kufubaza makali ya virusi

Soma https://jamii.app/VVUTanzania

#JFAfya
SUDAN: MAJAJI WAKEMEA MAUAJI YA WAANDAMANAJI

Majaji na Waendesha Mashtaka kadhaa wamekemea mauaji ya Waandamanaji wapatao 70 tangu Jeshi kuchukua Madaraka

Wametoa rai ya kumaliza ghasia hizo zilizopelekea zaidi ya watu 2,000 kujeruhiwa

Soma - https://jamii.app/VifoSudan

#Democracy #HumanRights
#COVID19: Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa (CDC) Afrika kimetaka Chanjo zinazotolewa kuwa na muda wa matumizi kati ya miezi 3 hadi 6 ili Mataifa yaweze kupanga usambazaji kikamilifu

10.4% ya Waafrika wameshapata Chanjo kikamilifu

Soma - https://jamii.app/CDCMudaChanjo

#UVIKO3 #JFAfya