JamiiForums
55.4K subscribers
33.4K photos
2.03K videos
30.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Ashatu Kijaji ametoa siku 3 kwa Tume ya Ushindani (FCC) kutoa sababu ya kupanda kwa bei za vinywaji Baridi Nchini

Pia, ametoa siku saba kwa FCC kueleza sababu za kupanda kwa bei za vifaa vya ujenzi

Soma - https://jamii.app/FCCBeiSoda

#JFBiashara
#Uganda inakabiliwa na uhaba wa Mafuta ya Petroli kutokana na foleni kubwa ya Magari ya kusafirisha bidhaa hiyo kwenye mipaka ya Busia na Malaba

Foleni inakadiriwa kufika hadi Kilometa 70 kutokana na Madereva kulazimika kufanyiwa vipimo vya Corona

Soma - https://jamii.app/LackPetrolUG
UTEUZI: Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Mcha Hassan Mcha kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA)

Vilevile, Balozi Celestine Joseph Mushy ameteuliwa na Rais Samia kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Austria

Soma - https://jamii.app/UteuziViongozi2

#Governance
AFGHANISTAN: Kundi la Wataalamu 36 wa Haki za Binadamu kutoka Umoja wa Mataifa limesema Viongozi wa Taliban wanafanya Ubaguzi na Ukatili wa Kijinsia dhidi ya Wanawake

Jumuiya ya Kimataifa yasisitizwa kuongeza kasi ya misaada ya kibinadamu

Soma - https://jamii.app/WomenTaliban

#WomensRights #Governance
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: MABASI YA MIKOANI KUONGOZWA NA ASKARI WA BARABARANI

Akizungumza na JamiiForums, Kamanda Onesmo Lyanga amesema Watakuwa wanaweka Askari kwenye Basi la Kwanza, na Mabasi mengine hayatakiwi kulipita hilo basi la kwanza

Lengo ni kudhibiti ajali zinazotokana na Uzembe. Utaratibu huo pia umeonekana kufanyika kwa Mabasi yatokayo Mbeya kama kwenye Video

Soma - https://jamii.app/MabasiEscort
AFGHANISTAN: MATETEMEKO YA ARDHI YAUA ZAIDI YA WATU 20

Matetemeko hayo ya kipimo cha 4.9 na 5.3 yaliathiri Mkoa wa Kaskazini Magharibi wa Badghis, na kupelekea nyumba na majengo kuporomoka

Watoto 4 ni miongoni mwa waliofariki kwenye vifusi

Soma - https://jamii.app/AfghanQuakes

#JFUwajibikaji
MDAU: MABADILIKO YANAYOCHOCHEA UONGOZI BORA

Uwepo wa Katiba inayokidhi matakwa ya wananchi: Ili Nchi yoyote ipige hatua katika Nyanja ya Utawala Bora na Uwajibikaji, katiba ni suala muhimu kwani husaidia kuwakumbusha Viongozi wajibu wao ili wasivuke mipaka katika utendaji

Sera Bora na Mifumo stahiki katika utumiaji wa Rasilimali: Afrika imebarikiwa na rasilimali mbalimbali lakini kutokuwepo mikakati mbadala katika utumiaji imepelekea wachache kujinufaisha

Soma - https://jamii.app/UongoziBoraSOC

#StoriesOfChange #Governance
#AFCON2021: SENEGAL, GUINEA ZAFUZU HATUA YA MTOANO

#TeamSenegal imefuzu kucheza hatua ya mtoano ya michuano baada ya kutoka sare ya 0-0 na #TeamMalawi

Aidha, #TeamGuinea imefuzu kwenda hatua hiyo licha ya kufungwa goli 2-1 na #TeamZimbabwe katika mechi ya mwisho

#JFSports
SUDAN: Baadhi ya maduka na Ofisi vyafungwa kutokana na mgomo wa siku 2 uliochochewa na vifo vya waandamanaji

Takriban 71 wameuawa na zaidi ya 2,000 kujeruhiwa tangu Mapinduzi ya Kijeshi Oktoba 2021. Waandamanaji wataka Jeshi kuachana kabisa na Siasa

Soma https://jamii.app/71DeadSudan

#Democracy
SONGWE: MJAMZITO AUAWA KWA KUCHOMWA KISU NA MUMEWE

Subira Kibona (16) Mkazi wa Ileje amefariki kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali mgongoni kisha Mwili wake kuchomwa Moto na Shukrani Kamwela (16)

Alipotea nyumbani tangu Januari 13 baada ya Shukrani kumwambia waende kwa Mganga kutafuta Dawa ya Tumbo

Soma - https://jamii.app/MjaKifoIleje

#UkatiliKijinsia #JFMatukio
GHARAMA ZA VIFURUSHI VYA INTANETI ZAPANDA

Wadau wameshuhudia mabadiliko ktk bei za Vifurushi, ikionekana Kampuni za Mawasiliano zimepunguza ukubwa wa Vifurushi vya awali huku Wananchi wakilalamika kutofahamishwa kuhusu hatua hiyo

Soma - https://jamii.app/VifurushiIntaneti

#DigitalRights
#COVID19: Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema kwa wiki iliyopita pekee, Kirusi cha #Omicron kimepelekea maambukizi mapya Milioni 18 ulimwenguni

WHO imeeleza wasiwasi wake kuhusu Nchi nyingi kuwa na kasi ndogo ya utoaji Chanjo

Soma - https://jamii.app/KirusiOmicronWHO

#UVIKO3 #JFAfya
'THE AFRICAN RENAISSANCE': SANAMU REFU ZAIDI BARANI AFRIKA

Sanamu inapatikana Nchini #Senegal na ina urefu wa Mita 49. Ilizinduliwa Aprili 2010 na aliyekuwa Rais kwa wakati huo, Abdoulaye Wade

Sanamu hii ilikusudiwa kuashiria ushindi wa ukombozi wa Afrika na kushindana na Statue of Liberty na Eiffel Tower kama kivutio cha Watalii

Soma - https://jamii.app/AfricanRenaissance

#JFMaarifa #JFHistoria
#AUSTRIA: KUANZIA FEBRUARI WASIOCHANJWA KUTOZWA FAINI HADI TSH. 9,414,826

Kuanzia Februari Chanjo kwa Watu wazima itakuwa ni lazima na wote ambao watagoma kuchanjwa watatozwa faini

Sheria hiyo imepangwa kutumika hadi Januari 31, 2024

Soma - https://jamii.app/MustVaccineAustria

#UVIKO3 #JFAfya
AFGHANISTAN: Mullah Hasan Akhund anayekaimu nafasi ya Waziri Mkuu wa Nchi hiyo amesema Utawala wa #Taliban umekidhi vigezo vyote hivyo utambuliwe na Serikali za Kimataifa

Serikali zimekuwa zikisita kuitambua Taliban tangu ichukue Madaraka Agosti 2021

Soma - https://jamii.app/UongoziTaliban

#Governance
MDAU: BAADHI YA WANAUME HUTUMIA POSA KUWALAGHAI WANAWAKE

Anasema kutokana na Wanawake wenye msimamo kutokukubali kufanya baadhi ya mambo bila utambulisho wowote kwa Wazazi, hupelekea Wanaume kutafuta washenga uchwara na baadaye kuingia Mitini bila Kuoa

Anafafanua, Posa zisizokamilika kuwa Ndoa husababisha Msongo wa Mawazo na Mfadhaiko wa Akili kwa Mwanamke na huleta hali ya kukata tamaa ya maisha

Soma - https://jamii.app/PosaFeki

#StoriesOfChange #JFMdau
UINGEREZA: WABUNGE WAWASILISHA BARUA ZA KUTOKUWA NA IMANI NA BORIS

Wabunge 11 wa Chama cha Kihafidhina cha Waziri Mkuu, Boris Johnson wamewasilisha barua za kutokuwa na imani na Kiongozi huyo

Kisheria barua 54 zinahitajika ili kutekeleza kura hiyo

Soma https://jamii.app/KuraImaniBoris

#Accountability
UJERUMANI YAREKODI MAAMBUKIZI MAPYA 112,323

Imetajwa kuwa idadi kubwa zaidi tangu kuanza Mlipuko wa #COVID19. Maambukizi yamefikia 8,186,850

Waziri wa Afya anaamini idadi ya Visa ambavyo havijaripotiwa ni mara mbili ya takwimu za sasa

Soma - https://jamii.app/VisaUjerumani

#UVIKO3 #JFAfya
MDAU: FAIDA ITAKAYOPATIKANA TAIFA LIKIWEKEZA KWA VIJANA

Kupunguza utegemezi wa Wataalamu kutoka Nje: Taifa likiwekeza vya kutosha na kwa ubora, uhakika wa kupata wataalamu mbalimbali utakuwepo

Kukuza Biashara, Uchumi wa Nchi na Maendeleo: Taifa likiwekeza kwa Vijana, litajihakikishia kukuza Uchumi na kurahisisha kukua kwa Maendeleo

Soma - https://jamii.app/VijanaSOC

#StoriesOfChange #JFMdau
AFYA: SEHEMU ZA SIKIO AMBAZO HUWEZA KUATHIRIWA KIAFYA

1. Sikio la nje: Huwa na Ngozi laini ambayo inaweza kuumizwa kwa vidonda au kujikuna kwa kidole kichafu au kwa kutumia vijiti

2. Sikio la kati: Inaweza kupata matatizo kama kiwambo cha Sikio kuumizwa kwa kuingiza kitu ndani ya sikio, mlio mkubwa au Bakteria

3. Sikio la ndani: Huumia kama kelele zimezidi au kupokea mlio mkubwa wa mlipuko wa karibu unaoweza kuharibu Neva ndogo

Soma - https://jamii.app/AfyaSikio

#JFAfya