JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
UTAFITI: COVID-19 YABAINIKA KUSHUSHA UZALISHAJI WA MBEGU ZA KIUME

Utafiti uliofanywa kwa Wanaume 120 waliougua na kupona #COVID19 nchini Ubelgiji umebaini ujazo wa mbegu za kiume hupungua kwa wanaume baada ya kupata Ugonjwa huo

Soma - https://jamii.app/MbeguZaKiume

#JFAfya
#AFCON2021: GUINEA, MOROCCO ZAPATA USHINDI

Mchezo wa 2 wa Kundi B kwa siku ya leo, umemalizika kwa #TeamGuinea kupata ushindi wa 1-0 dhidi ya #TeamMalawi

Pia, mchezo wa kwanza wa Kundi C kwa leo, umemalizika kwa #TeamMorocco kupata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya #TeamGhana

#JFSports
KAZAKHSTAN: Rais Kassym-Jomart Tokayev amesema Nchi imerejea katika utulivu, na maandamano yaliyotokea yalikuwa ni jaribio la mapinduzi

Wananchi waliandamana kupinga ongezeko la bei za mafuta. Watu zaidi ya 150 waliuawa kwenye machafuko hayo

Soma https://jamii.app/KazakhstanMapinduzii

#Governance
MYANMAR: KIONGOZI WA KIRAIA AONGEZEWA MIAKA 4 JELA

Mahakama Nchini #Myanmar imemhukumu tena Aung San Suu Kyi miaka mingine 4 kwa kumiliki na kuingiza vifaa vya mawasiliano kinyume cha #Sheria na kuvunja masharti ya kupambana na #COVID19

Soma - https://jamii.app/Suu4yrsJail
#Democracy
UGANDA: SHULE ZAFUNGULIWA BAADA YA MIAKA TAKRIBAN MIWILI

Ili kudhibiti usambaaji wa maambukizi ya #COVID19, Uganda ilifunga Shule tangu Machi 2020

> Mtaala utawekwa sawa ili kuwasaidia Wanafunzi ambao hawakutumia Teknolojia kuendelea kujifunza

Soma https://jamii.app/ShuleUganda

#Governance #JFElimu
AJALI SIMIYU: Takriban Watu 14 wamefariki Dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya magari waliyokuwa wakisafiria kugongana

Kati ya waliopoteza maisha ni Waandishi wa Habari 5 waliokuwa katika msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza

Soma - https://jamii.app/Ajali14Simiyu

#JFMatukio
JE, WAJUA KUWA SPIKA SIO LAZIMA AWE MBUNGE?

Kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, Ibara ya 84(9) iwapo mtu asiye Mbunge akichaguliwa kuwa Spika wa Bunge atatakiwa kuapa kiapo cha Uaminifu

Soma - https://jamii.app/SpikaBunge

#JamiiForums #JFMaarifa
MBINU UNAZOWEZA KUTUMIA KULINDA AFYA YA MACHO YAKO

1. Unashauriwa kuvaa Miwani ya kuzuia Mionzi ya Jua ili kuzuia Mionzi ya UV na hakikisha unatumia Miwani yenye uwezo wa kuzuia Mionzi kwa 99%-100%

2. Kula Mlo wenye Virutubisho Kamili: Virutubisho muhimu kwa utunzaji wa Macho ni Vitamini A, Vitamini E, Vitamini C, Asidi ya Mafuta ya Omega-3, Zinki, Lutein na Zeaxanthin zinazopatikana kwenye Karoti, Mchicha, Samaki na Mayai.

Soma - https://jamii.app/RoutineEyeCare

#JFAfya #EyeCare
#ZIMBABWE: Rais Emmerson Mnangagwa amemfuta kazi Waziri wa Usalama wa Nchi hiyo, Owen Ncube kwa kufanya vitendo visivyofaa kama Kiongozi wa Serikali

Owen anadaiwa kuwatisha baadhi ya Wanachama wa ZANU-PF ktk Uchaguzi wa ndani hivi karibuni

Soma - https://jamii.app/OwenOutZimb

#Accountability
UTAFITI: MAFUA YANAWEZA KUZUIA KUPATA #COVID19

Watafiti wa Imperial College of London wamebaini 'T-Cells' husaidia kuzuia maambukizi. Mafua yamebainika kuzalisha 'T-Cells' nyingi

Chanjo imetajwa kuwa njia thabiti kukabiliana na Corona

Soma - https://jamii.app/CommonCold

#UVIKO3 #JFAfya
RAIS SAMIA: AJIRA NDIYO NGUZO YAKO YA MAISHA, SIO 'BY THE WAY'

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kubadilika wakiajiriwa sekta binafsi hata Serikalini huku akiongeza "sekta binafsi ukizubaa nafasi yako inachukuliwa"

Amefafanua "Nilishawahi kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Zanzibar, wakati ule kesi nyingi nilizokuwa nikipokea ni uzembe, kutokuwa na nidhamu sehemu za kazi, umefiwa na shangazi wa shangazi yako unakwenda kuzika bila kutoa taarifa"

Soma - https://jamii.app/SamiaAjira

#Governance
MDAU: MAMBO YANAYOWEZA KUKUSABABISHIA LAANA KWENYE MAISHA

1. Kumdhulumu Mtu: Jasho la Mtu huzaa mikosi. Machozi na manung'uniko anayoyatoa Mtu aliyeumizwa kwa kudhulumiwa, hugeuka laana

2. Kuua au kutoa kafara: Damu ya Mtu ni laana, Damu ya Mtu ni mkosi, Damu ya Mtu ni nuksi. Ukisikia kuwa kuna vitu havina midomo lakini vinaongea, basi ni Damu ya Mtu

3. Kumkana au kumtukana Mzazi: Vitabu vya Mungu vinaeleza, "Waheshimu Baba na Mama upate kheri na miaka mingi Duniani"

Soma - https://jamii.app/TabiaLaana

#StoriesOfChange #JFMdau
KENYA YAZUIA NDEGE ZA UAE

Mamlaka ya Usafiri wa Anga (KCAA) yapiga marufuku ndege za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kujibu marufuku iliyowekwa kwa ndege za Kenya

UAE iliweka marufuku baada ya kubaini udanganyifu katika vipimo vya #COVID19

Soma - https://jamii.app/KenyaVsUAE

#Governance
#UGANDA: MWANDISHI ASHTAKIWA KWA KUTUMA TAARIFA ZA KASHFA DHIDI YA RAIS NA MWANAE

Kakwenza Rukirabashaija anayetuhumiwa kutuma taarifa za kashfa kuhusu Rais na Mtoto wake kwenye #Twitter amefunguliwa mashtaka 2 ya Mawasiliano ya kukera

Soma - https://jamii.app/RukirabashaijaCourt

#FreeSpeech
UTEUZI: Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Mhifadhi William Simon Mwakilema kuwa Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA)

Anachukua nafasi ya Dkt. Allan Herbert Kijazi ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi

Soma - https://jamii.app/UteuziTANAPA

#Governance
MDAU: KUMPIGA/KUMGOMBEZA MTOTO KWA KUFANYA VIBAYA DARASANI SIO KUMSAIDIA

Anasema Binadamu tunatofautiana uwezo wa kuelewa mambo. Kuna Watoto uwezo wao wa Darasani ni mdogo lakini ana kipaji au uwezo fulani ni vizuri kumuendeleza upande huo ili kumsaidia

Ameongeza, kama Mtoto kila siku anaenda Shuleni, anahudhuria kila kipindi na kufanya kazi za nyumbani (home work), ya nini kumchapa anaposhika namba za chini? Usitumie kigezo kimoja kumpima Mwanao.

Mjadala zaidi - https://jamii.app/KuchapaWttMasomo
#Malezi
HOJA: WOSIA NI JAMBO MUHIMU LINALOSAHAULIKA NA WENGI

Mshiriki wa #StoriesOfChange asema kutoacha wosia husababisha Wajane na Watoto wa Marehemu kupoteza Haki kwa kukosa mwongozo wa mgawanyo wa mali

Ashauri watu kuandika wosia ili kupunguza migogoro

Soma https://jamii.app/WosiaMirathi

#JFMdau
Jamii Forums tunawatakia Watanzania wote Maadhimisho mema ya Miaka 58 ya Mapinduzi matukufu ya #Zanzibar

Mapinduzi ya Zanzibar yalitokea Mwaka 1964 ili kumuondoa Madarakani Sultani wa Zanzibar na Serikali yake, iliyoundwa hasa na Waarabu

#MapinduziZanzibar #JamiiForums
WHO: 50% YA WATU BARANI ULAYA WATAAMBUKIZWA OMICRON

Shirika la Afya (WHO) lasema nusu ya watu wataambukizwa #Omicron kipindi cha wiki 6 - 8 zijazo

Makadirio yanatokana na Visa vipya Milioni 7 vilivyoripotiwa Ulaya wiki ya kwanza ya 2022

Soma - https://jamii.app/OmicronUlaya

#UVIKO3 #JFAfya
PWANI: Athumani Ramadhani (20), Maneno Hamis (23) na Abdallah Rajabu (21) wamefariki baada ya kulipukiwa na Chuma walichookota kinachodhaniwa kuwa ni bomu

Wanaojihusisha kuuza na kununua Vyuma chakavu watakiwa kuwa waangalifu wanapokusanya

Soma - https://jamii.app/VifoBomuPwani

#JFMatukio
👍1