JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
RAIS SAMIA: KAZI ZIPO NYINGI, NI VIJANA KUCHAKARIKA NA KUONA FURSA

Asema Vijana wengi wanasubiri Ajira wanapomaliza kusoma, lakini hawahangaiki kutafuta fursa za kazi

Kuhusu changamoto ya Mitaji amesema ipo Mifuko inayotoa Mikopo kwa Vijana, lakini bado haijatosheleza kutokana na idadi yao kuwa kubwa

Soma - https://jamii.app/KaziFursaVijana

#Governance
KAZAKHSTAN: Maandamano yaliyoanza kufuatia ongezeko la bei ya mafuta yametajwa kuwa mabaya zaidi tangu Uhuru. Waandamanaji 26 wameuawa hadi sasa

Vikosi vinavyoongozwa na Urusi vimewasili kusaidia kudhibiti Waandamanaji ambao sasa wanaipinga Serikali

Soma - https://jamii.app/KazakhstanProtests

#HumanRights
Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa(CDC) kimesema ‘lockdown’ sio tena njia bora ya kukabiliana na maambukizi ya #COVID19 yanayoendelea kuitesa Dunia

Kimehimiza kutumia Afya ya Umma na Jamii ili kupunguza Maambukizi pamoja na kupata Chanjo

Soma https://jamii.app/LockdownSuluhu

#UVIKO3 #JFAfya
ETHIOPIA: SERIKALI YATOA MSAMAHA KWA WAFUNGWA WA UPINZANI

Hatua hiyo ni jitihada moja wapo kuleta maridhiano ya kitaifa na kuhamasisha amani

Miongoni mwa walioachiwa huru ni Viongozi kadhaa wa TPLF ambayo imepigana na Serikali kwa zaidi ya mwaka 1

Soma - https://jamii.app/RebelsFreedEth

#Governance
MDAU: MABADILIKO YANAYOWEZA KUTATUA CHANGAMOTO MBALIMBALI NCHINI

Kilimo: Anashauri Kilimo cha kisasa kutiliwa mkazo, na umwagiliaji uwezeshwe ili kuondokana na utegemezi wa mvua

Uchumi: Maslahi ya wafanyakazi yaboreshwe ili kuleta uadilifu na kupunguza mianya ya rushwa

Kuwe uongozi wenye kutambua Haki za Binadamu na usiokuwa na upendeleo

Msome - https://jamii.app/MabadilikoSOC

#StoriesOfChange #JFMdau
UMMY MWALIMU AREJESHWA WIZARA YA AFYA

Katika Mabadiliko ya Baraza la Mawaziri, Rais Samia amemhamisha Waziri Ummy Mwalimu kutoka TAMISEMI, na sasa atakuwa Waziri wa Afya

Dkt. Dorothy Gwajima anaenda Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Mahitaji Maalum

#Governance
HUSSEIN BASHE ATEULIWA KUWA WAZIRI WA KILIMO

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Hussein Bashe kuwa Waziri wa Kilimo. Awali Bashe alikuwa Naibu Waziri wa Wizara hiyo

Anthony Mavunde ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Kilimo

#Governance
PROF. ADOLF MKENDA AHAMISHIWA WIZARA YA ELIMU

Aliyekuwa Waziri wa Kilimo, Prof. Adolf Mkenda amehamishiwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ambayo awali Prof. Joyce Ndalichako alikuwa Waziri

Rais Samia amemhamisha Prof. Ndalichako kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu; Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu

#Governance
#UTEUZI: Rais Samia Suluhu amembadilisha Wizara George Simbachawene aliyekuwa Wizara ya Mambo ya Ndani kwenda Wizara ya Katiba na Sheria

Pia, amembadilisha Innocent Bashungwa aliyekuwa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwenda Wizara ya Ofisi ya Rais - TAMISEMI

#JFUteuzi #Governance
👍1
MOHAMED MCHENGERWA KUWA WAZIRI WA UTAMADUNI

Rais Samia amemhamishia Mohamed Omary Mchengerwa aliyekuwa Ofisi ya Rais, Menejimenti, Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwenda Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ambayo awali ilikuwa chini ya Innocent Bashungwa

#Governance
#UTEUZI: Rais Samia Suluhu Hassan amembadilisha Wizara, Ashatu Kijaji aliyekuwa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwenda Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara

#JFUteuzi #Governance
#UTEUZI: Rais Samia Suluhu Hassan amembadilisha Wizara Jenista Mhagama aliyekuwa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu kwenda Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora

#JFUteuzi #Governance
#UTEUZI: Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Angelina Mabula kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Pia, amemteua Ridhiwani Kikwete kuwa Naibu Waziri wa Wizara hiyo

#JFUteuzi #Governance
#UTEUZI: Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Pindi Chana kuwa Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu atakayeshughulika na Sera, Bunge na Uratibu

#JFUteuzi #Governance
RAIS SAMIA ABADILI WIZARA 3

Ameunganisha Wizara ya Uwekezaji na Wizara ya Viwanda na Biashara kuwa na Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara

Ameunda Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum na Wizara ya Afya kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

#Governance
#AFCON2021: NANI KUWA BINGWA?

Michuano hiyo inaanza kesho Januari 9, kwa wenyeji #TeamCameroon kuivaa #TeamBurkinaFaso majira ya saa 1:00 jioni (EAT)

#TeamAlgeria ambaye ni Bingwa Mtetezi, #TeamCameroon, #TeamSenegal na #TeamEgypt zinapewa nafasi kubwa kuwa Bingwa

#JFSports
JWTZ wamekanusha taarifa zilizochapishwa katika YouTube channel ya News24 ikiwa na kichwa 'MKUU WA MAJESHI AINGILIA KATI SAKATA LA RAIS NA SPIKA'

> Wamesema wanafanya kazi kwa weledi na hawaingilii masuala ya kisiasa

Soma https://jamii.app/KanushoJWTZ

#Accountability
#AFCON2021: CAMEROON YAANZA KWA USHINDI

- Mtayarishaji wa Mashindano hayo #TeamCameroon imeanza kwa ushindi wa goli 2-1 dhidi ya #TeamBurkinaFaso katika mchezo wa ufunguzi

- Mchezo unaofuata saa 4:00 usiku (EAT) ni kati ya #TeamEthiopia na #TeamCapeVerde

#JFSports
KILIMANJARO: BINTI ADAIWA KUMUUA MAMA YAKE KWA TAMAA YA MALI

Wendy anadaiwa kumuua Mama yake mzazi (Mama Ipepu) ambaye ni Nesi mstaafu wa KCMC

Ni takriban mwaka sasa watu wamekuwa wakimuulizia Mama huyo na kuambiwa amekwenda kutibiwa nje ya Nchi

Soma - https://jamii.app/BintiKifoMama

#JFMatukio
USWISI: WANAJESHI WATAKIWA KUACHA KUTUMIA WHATSAPP, SIGNAL NA TELEGRAM

Kwasababu ya ulinzi wa taarifa, Wanajeshi wametakiwa kutumia Mtandao wa Uswisi uitwao Threema Messenger

Jeshi litagharamia kuwa na Threema ambayo ni Dola 4.35 (Tsh. 8,900)

Soma - https://jamii.app/SwissArmy

#Governance