JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
JE, WAIFAHAMU NJIA YA KUZIKA YA AQUAMATION?

#Aquamation ni namna ya uzikaji ambayo imekuwepo tangu miaka ya 1880. Njia hii huyeyusha Maiti na kufanya iwe Majivu kabisa tofauti na njia ya kuchoma

Ndivyo namna Desmond Tutu alivyochagua kuzikwa

Soma - https://jamii.app/Aquamation

#JFMaarifa
SUDAN: Utawala wa Kijeshi umeonywa kutofanya uamuzi wa upande mmoja wa uteuzi wa Waziri Mkuu mpya

Marekani, Uingereza, Norway na Umoja wa Ulaya zimesema hazitamuunga mkono Waziri Mkuu atakayeteuliwa iwapo wadau wa kiraia hawatahusishwa

Soma - https://jamii.app/UteuziWaziriSudan

#Democracy
UFARANSA YARIPOTI AINA MPYA YA #COVID19, WAKIITA 'IHU'

Watu 12 wamekutwa na kirusi hicho kiitwacho B.1.640.2 au IHU

> Shirika la Afya Duniani (WHO) likithibitisha uwepo wa kirusi hicho kitaweza kuitwa 'Pi' ndio herufi inayoifuata #Omicron

Soma https://jamii.app/UfaransaIHU

#UVIKO3 #JFAfya
MAREKANI: Mshauri wa Masuala ya Kitabibu wa Ikulu, Dkt. Anthony Fauci amesema tafiti kuhusu Watoto wa miezi 6 hadi miaka 5 kupatiwa Chanjo ya #COVID19 zinaendelea na ndani ya kipindi cha nusu Mwaka majibu yatakuwa yameshatoka

Soma - https://jamii.app/FauciVaccines

#UVIKO3 #JFAfya
RIPOTI: Shirika la Umoja wa Mataifa la Kukabiliana na Dharura linasema zaidi ya watu Milioni 6.4 katika maeneo kame ya Mashariki na Kusini mwa Ethiopia watahitaji msaada wa chakula

Vita ya Serikali na TPLF vimeacha mamilioni wakihitaji misaada

Soma - https://jamii.app/WatuMsaadaETH
NIGERIA: MAGENGE YA UHALIFU KUTAMBULIKA KAMA MAKUNDI YA KIGAIDI

Serikali imefanya hivyo kuimarisha Usalama kufuatia ongezeko la ghasia

Magenge hayo yamekuwa yakifanya mashambulizi, kuvamia vijiji, kuiba mifugo na kuteka nyara watu ili kulipwa fedha

Soma - https://jamii.app/UhalifuNigeria

#Governance
SERIKALI: WANAOFICHA WATOTO KUANZA SHULE WACHUKULIWE HATUA

Waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu ameagiza Mikoa kutosita kuwachukulia hatua Wazazi/Walezi hao

Asema kufikia Desemba 31 Wanafunzi 488,780 wa Darasa la Awali wameandikishwa Shule za Serikali

Soma - https://jamii.app/ShuleWatotoTAMISEMI

#JFElimu
SPIKA JOB NDUGAI AJIUZULU

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo leo Januari 06, 2022 ikiwa ni siku chache tangu kusambaa kwa video ambayo alinukuliwa akisema ipo siku Nchi itauzwa kutokana na madeni

Amesema ameandika Barua ya kujiuzulu kwa Katibu Mkuu wa CCM na uamuzi huo ni binafsi na hiari, na ameuchukua kwa kuzingatia maslahi mapana ya Nchi, Serikali na Chama

Soma - https://jamii.app/NdugaiAjiuzulu

#Accountability #JFUwajibikaji
#COVID19: Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema Visa Milioni 9.5 vimeripotiwa ulimwenguni Wiki iliyopita

Mkuu wa WHO, Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema Kirusi cha #Omicron hakipaswi kuainishwa kama 'Hakina makali' kwani kinaua watu

Soma - https://jamii.app/OmicronWHO

#UVIKO3 #JFAfya
SUDAN: Takriban Watu 60 wameripotiwa kufariki na wengine kujeruhiwa ktk maandamano ya kupinga Utawala wa Kijeshi Nchini humo

Waandamanaji walitawanywa kwa Risasi na Mabomu ya machozi jambo linalokwamisha Juhudi za kuleta mabadiliko ya Kidemokrasia

Soma - https://jamii.app/SudanMaandamano

#HumanRights #Democracy
👍1
Bunge limesema taratibu za Uchaguzi wa Spika baada ya Job Ndugai kujiuzulu jana Januari 06, 2022 zinaendelea

Kamati zilizokuwa zikutane kuanzia Januari 10, pamoja na zile zilizotakiwa kukutana kuanzia Januari 17, 2022 hazitakutana wakati huo

Soma https://jamii.app/BungeSpikaTZ

#Democracy
RAIS SAMIA: KAZI ZIPO NYINGI, NI VIJANA KUCHAKARIKA NA KUONA FURSA

Asema Vijana wengi wanasubiri Ajira wanapomaliza kusoma, lakini hawahangaiki kutafuta fursa za kazi

Kuhusu changamoto ya Mitaji amesema ipo Mifuko inayotoa Mikopo kwa Vijana, lakini bado haijatosheleza kutokana na idadi yao kuwa kubwa

Soma - https://jamii.app/KaziFursaVijana

#Governance
KAZAKHSTAN: Maandamano yaliyoanza kufuatia ongezeko la bei ya mafuta yametajwa kuwa mabaya zaidi tangu Uhuru. Waandamanaji 26 wameuawa hadi sasa

Vikosi vinavyoongozwa na Urusi vimewasili kusaidia kudhibiti Waandamanaji ambao sasa wanaipinga Serikali

Soma - https://jamii.app/KazakhstanProtests

#HumanRights
Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa(CDC) kimesema ‘lockdown’ sio tena njia bora ya kukabiliana na maambukizi ya #COVID19 yanayoendelea kuitesa Dunia

Kimehimiza kutumia Afya ya Umma na Jamii ili kupunguza Maambukizi pamoja na kupata Chanjo

Soma https://jamii.app/LockdownSuluhu

#UVIKO3 #JFAfya
ETHIOPIA: SERIKALI YATOA MSAMAHA KWA WAFUNGWA WA UPINZANI

Hatua hiyo ni jitihada moja wapo kuleta maridhiano ya kitaifa na kuhamasisha amani

Miongoni mwa walioachiwa huru ni Viongozi kadhaa wa TPLF ambayo imepigana na Serikali kwa zaidi ya mwaka 1

Soma - https://jamii.app/RebelsFreedEth

#Governance
MDAU: MABADILIKO YANAYOWEZA KUTATUA CHANGAMOTO MBALIMBALI NCHINI

Kilimo: Anashauri Kilimo cha kisasa kutiliwa mkazo, na umwagiliaji uwezeshwe ili kuondokana na utegemezi wa mvua

Uchumi: Maslahi ya wafanyakazi yaboreshwe ili kuleta uadilifu na kupunguza mianya ya rushwa

Kuwe uongozi wenye kutambua Haki za Binadamu na usiokuwa na upendeleo

Msome - https://jamii.app/MabadilikoSOC

#StoriesOfChange #JFMdau
UMMY MWALIMU AREJESHWA WIZARA YA AFYA

Katika Mabadiliko ya Baraza la Mawaziri, Rais Samia amemhamisha Waziri Ummy Mwalimu kutoka TAMISEMI, na sasa atakuwa Waziri wa Afya

Dkt. Dorothy Gwajima anaenda Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Mahitaji Maalum

#Governance
HUSSEIN BASHE ATEULIWA KUWA WAZIRI WA KILIMO

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Hussein Bashe kuwa Waziri wa Kilimo. Awali Bashe alikuwa Naibu Waziri wa Wizara hiyo

Anthony Mavunde ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Kilimo

#Governance
PROF. ADOLF MKENDA AHAMISHIWA WIZARA YA ELIMU

Aliyekuwa Waziri wa Kilimo, Prof. Adolf Mkenda amehamishiwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ambayo awali Prof. Joyce Ndalichako alikuwa Waziri

Rais Samia amemhamisha Prof. Ndalichako kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu; Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu

#Governance
#UTEUZI: Rais Samia Suluhu amembadilisha Wizara George Simbachawene aliyekuwa Wizara ya Mambo ya Ndani kwenda Wizara ya Katiba na Sheria

Pia, amembadilisha Innocent Bashungwa aliyekuwa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwenda Wizara ya Ofisi ya Rais - TAMISEMI

#JFUteuzi #Governance
👍1