JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Prof. Abel Makubi, Katibu Mkuu Wizara ya Afya amesema Wasafiri wote wanaoishia Nchi za Marekani, UAE, baadhi ya Nchi za Ulaya na India watatakiwa kufanyiwa kipimo cha haraka cha #COVID19 kabla ya kuondoka

Aidha, Wasafiri wote wanaunganisha Ndege kupitia #Tanzania wanapaswa kufanya kipimo cha haraka Uwanjani ndani ya Saa 6 kabla ya kusafiri

Soma - https://jamii.app/CovidTestTrav
#UVIKO3
TANZANIA YAPOKEA DOZI 376,320 ZA CHANJO YA MODERNA

Hii ni Awamu ya Kwanza kwa aina hii ya Chanjo kuingia Nchini. Dozi hizo zitatumika kuchanja Watu 188,160

Hadi sasa Tanzania imepokea Dozi 6,408,950 zikijumuisha #Sinopharm, J&J na #Pfizer

Soma - https://jamii.app/ModernaTZ
#UVIKO3
ALIYEKUWA ASKOFU MKUU WA TAG AFARIKI DUNIA

Askofu Prof. Ranwell Mwenisongole alikuwa Mchungaji Kiongozi wa City Christian Center (CCC) Upanga na Askofu Mkuu Awamu ya Pili

Alikuwa akisumbuliwa na Maradhi ya Kisukari na Shinikizo la Damu

Soma - https://jamii.app/RIPMwenisongole
TANZIA: ASKOFU DESMOND TUTU AFARIKI DUNIA

Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, Askofu Desmond Tutu ambaye alishiriki kupambana na ubaguzi wa rangi Afrika Kusini amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 90

> Taarifa za kifo chake zimetangazwa na Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa

Soma https://jamii.app/DesmondTutu
JAJI WEREMA: NCHI IMEPITIA WAKATI MGUMU MIAKA 5 ILIYOPITA

Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Awamu ya Nne, Jaji Frederick Werema amesema Rais kuwa na madaraka makubwa bila kuhojiwa ni hoja ya wanaodai #Katiba Mpya tangu mwaka 1992

Soma - https://jamii.app/JajiWerema

#JFSiasa
WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR AKUTWA NA #COVID19

Waziri Nassor Ahmed Mazrui amethibitishwa kuwa na Virusi vya Corona. Ana dalili za wazi ikiwemo homa kali na maumivu ya viungo

Wananchi wahimizwa kuchukua tahadhari na kupata Chanjo ili kujikinga

Soma https://jamii.app/WaziriWaAfya

#UVIKO3
RAIS WA ZAMANI WA UGIRIKI, KAROLOS PAPOULIAS AFARIKI DUNIA

Rais Karolos Papoulias aliyeongoza Ugiriki 2005 hadi 2015 amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 92

Pia alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje mwaka 1985 hadi 1989, na 1993 hadi 1996

Soma - https://jamii.app/RaisUgiriki

#JFLeo
AFGHANISTAN: WANAWAKE WATAKIWA KUSINDIKIZWA KATIKA SAFARI NDEFU

Taliban imesema Wanawake wanaotaka kusafiri zaidi ya KM 72 wasipewe usafiri isipokuwa wakiwa na ndugu wa kiume wa karibu

Wamiliki magari wahimizwa kutopandisha Wanawake wasiovaa Hijabu

Soma https://jamii.app/SafariWanawake
UFARANSA: WATU 104,611 WAKUTWA NA COVID-19 NDANI YA SAA 24

Idadi hiyo haijawahi kufikiwa Nchini humo tangu kuingia kwa janga la Corona

Idadi ya waliolazwa vitengo vya uangalizi maalum imepanda kutoka Wagonjwa 28 na kufikia Watu 3,282

Soma - https://jamii.app/CoronaSpikeFrance

#UVIKO3
WAZIRI SIMBACHAWENE AAGIZA ASKOFU MWINGIRA AHOJIWE NA POLISI

Ni kufuatia tuhuma alizotoa ikiwemo kutishiwa maisha

Asema ni tuhuma nzito, akihoji kwanini hatoi taarifa Polisi

Aelekeza RPC Kanda Maalum Dar kumtafuta Askofu Mwingira kwa maelezo zaidi

Soma https://jamii.app/MwingiraPolisi
UFISADI: RAIS WA SOMALIA ASIMAMISHA MADARAKA YA WAZIRI MKUU

Asema ni kufuatia Uchunguzi wa tuhuma za Waziri Mohammed Roble kujipatia ardhi kilaghai

Roble amesimamishwa siku moja baada ya yeye na Rais kutuhumiana kuchelewesha Uchaguzi wa Bunge

Soma - https://jamii.app/PMSomalia
AFGHANISTAN: Serikali ya Taliban imezivunja Tume mbili za Uchaguzi pamoja na Wizara mbili za Amani na masuala ya Bunge

Yasema Asasi hizo hazina maana kulingana na hali ya #Afghanistan na itazifufua Tume na Wizara endapo kutakuwa na haja

Soma - https://jamii.app/TumeUchagTaliban

#Democracy
WAFUNGWA 5,704 WAPATA MSAMAHA WA RAIS

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametoa msamaha kwa wafungwa 5,704 kwa masharti mbalimbali

Msamaha haujahusisha Wafungwa wanaotumikia adhabu kadhaa zikiwemo za makosa ya kujaribu kuua na Uhujumu Uchumi

Soma - https://jamii.app/MsamahaWafungwa
POLISI: ASKOFU MWINGIRA AANZE KUHOJIWA NDANI YA SAA 24

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar, Jumanne Muliro amesema hatua hiyo imefikiwa baada ya kufuatilia kauli zinazodaiwa kutolewa na Askofu huyo, na kuona zinajenga hofu na chuki kwa Wananchi

Soma - https://jamii.app/MwingiraSaa24
JAJI MWAMBEGELE ATEULIWA KUWA MWENYEKITI WA TUME YA UCHAGUZI

Rais Samia amemteua Jaji Jacob Casthom Mwambegele kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)

Anachukua nafasi ya Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage aliyemaliza muda wake

Soma - https://jamii.app/ViongoziUteuzi

#JFLeo
KENYA: BABA AUA MWANAYE KWA KUMSUMBUA USINGIZINI

James Tarus (73) anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumuua Mwanaye(31) kwa kumgonga na mbao

Kijana alirudi amelewa na kumwamsha Baba yake huku akinyanyua kitanda, jambo lililomkasirisha Mzee

Soma https://jamii.app/SonDeadSleep
#JFLeo
MDAU: SABABU ZINAZOPELEKEA BIASHARA ZA VIJANA WENGI KUFA

1. Kukosekana kwa sababu yenye mashiko kwanini wameanza Biashara: Biashara imara inajengwa kwa msingi imara wa kwanini Biashara hii na sio nyingine

2. Usimamizi mbovu: Usimamizi ni moja ya mambo muhimu katika kukuza Biashara lakini Watu wamekuwa hawachukulii uzito unaostahili. Wengine huweka Watu wenye malengo tofauti na wasio na uchungu na Biashara

Soma - https://jamii.app/BiasharaVijana

#StoriesOfChange
ZAIDI YA SAFARI 6,000 ZA NDEGE ZAFUTWA

Kulingana na tovuti ya Flightware.com zaidi ya safari 6,000 za Ndege zimefutwa Duniani kote tangu Desemba 25

Mashirika mengi yametaja Kirusi cha #Omicron kuwa sababu ya kufuta safari hizo

Soma - https://jamii.app/OmicronFlights
#UVIKO3
MWANAMUZIKI DEFAO AFARIKI DUNIA

Mwanamuziki Mkongwe wa Rhumba kutoka Congo, Francoise Lulendo Matumona maarufu General Defao amefariki baada ya kuugua kwa muda mfupi

Alijizolea umaarufu mkubwa kwa miondoko yake ya Ndombolo and Ekibinda Nkoi

Soma https://jamii.app/DefaoDies
#JFLeo
POLAND: RAIS AKATAA SHERIA TATA YA HABARI

Rais Andrzej Duda ametumia Kura Turufu (Veto) kukataa Sheria ya Umiliki wa Vyombo vya Habari

Wakosoaji walisema Sheria hiyo inalenga kunyamazisha Kituo cha TVN24 ambacho hukosoa Serikali

Soma - https://jamii.app/PolandRaisVeto

#PressFreedom