JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MICHEZO: Mpambano kati ya Wolves na Arsenal hautochezwa leo baada ya Wolves kuomba usogezwe mbele kwasababu haina wachezaji wa kutosha kutokana na #COVID19 na majeruhi

Kwa jumla Premier League ya England imeahirisha Mechi 15 katika kipindi cha wiki mbili na nusu zilizopita kutokana na visa vya Corona katika timu mbalimbali

Soma - https://jamii.app/EPLPostponed
#Sports
Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema kulingana na mwenendo wa Deni la Taifa kufikia Trilioni 70, ipo siku Nchi itapigwa mnada

Ameongeza "Kipi ni bora, sisi Tanzania ya Miaka 60 tuendelee kukopa madeni makubwa makubwa au tubanane tufanye wenyewe hapa?"

Soma https://jamii.app/NdugaiTZMnada
RAIS SAMIA: TUTAKOPA TUMALIZE MIRADI YA MAENDELEO

Asema hakuna Nchi isiyokopa, na hata Mataifa yaliyoendelea yana Mikopo mikubwa

Ameeleza, "Ukikopa unajenga kwa haraka, ukisubiri ukusanye za kwako utamaliza lini kujenga? Mradi wa Matrilioni unasubiri za kwako utaumaliza lini"

Soma - https://jamii.app/MikopoMaendeleo

#JFLeo
IKULU, DAR: Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema katika miezi michache aliyokaa kwenye Serikali ya Awamu ya Sita, ameona mambo mengi ambayo huko nyuma hayakuwa yakifanyika lakini sasa hivi yanataka kuanza, akisisitiza hatokubali

Soma - https://jamii.app/SSHIkuluDar

#JFLeo
GUINEA: Kiongozi aliyeingia Madarakani kwa kuipindua Serikali, Kanali Mamady Doumbouya ameikabidhi Timu ya Taifa Bendera ili kwenda kushiriki Michuano ya kombe la #AFCON2021

Mamady ameiambia Timu hiyo "Rudini na Kombe la sivyo mtarudisha Fedha zote tulizowekeza kwenu"

#Sports
UFARANSA: Katika kukabiliana na #COVID19, Waziri Mkuu Jean Castex amesema kuanzia Januari 03 kufanyia kazi nyumbani itakuwa lazima kwa angalau siku 3 kwa wiki kwa watakaoweza

Mikusanyiko ya ndani itatakiwa kuwa na watu 2,000 na ya Nje 5,000

Soma https://jamii.app/COVIDFrance

#UVIKO3
GAMBIA: MAHAKAMA YATUPILIA MBALI OMBI LA KUBATILISHA MATOKEO YA UCHAGUZI

Mpinzani Ousainou Darboe alisema Kampeni zilihusisha rushwa

Ilidaiwa Rais Adama Barrow au Wanachama wa Chama chake waliwapa Fedha/Zawadi Wanakijiji ili wapate kura

Soma - https://jamii.app/UchaguziGambia
MAREKANI: WASIO NA DALILI ZA COVID-19 KUJITENGA KWA SIKU TANO

Waliokutwa na Virusi baada ya kujitenga kwa Siku 10 wanapaswa kuvaa Barakoa kwa Siku 5 wanapokuwa karibu na wengine

#Omicron inachukua 73% ya maambukizi ya Corona Nchini Marekani

Soma https://jamii.app/5DaysNteenUS
#UVIKO3
URUSI: MAHAKAMA YAAMURU SHIRIKA LA HAKI ZA BINADAMU KUFUNGWA

Shirika la Memorial limefungwa kwa kuvunja Sheria za kujisajili kama wakala wa Mashirika ya kigeni

Urusi kuna ukandamizaji dhidi ya upinzani na makundi ya Haki za Binadamu

Soma - https://jamii.app/MemorialClosed
#HumanRights
GAVANA BoT: HUWEZI KUTUMIA FEDHA ZA NDANI KWENYE MIRADI

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Florens Luoga amesema Mikopo haikopwi kwa ajili ya kula bali kufanya Miradi ambayo itaendelea kuzalisha na kuleta uhimilivu mzuri wa deni

Akihojiwa na Clouds Media amesema "Nchi haiwezi ikaweka rehani Watu au rasilimali zake na inazitumia ili Serikali iendelee kupata kipato"

Soma - https://jamii.app/LuogaMikopo

#JFLeo
HONG KONG: Polisi wamewakamata Watu sita kutoka Tovuti ya Stand News kwa tuhuma za njama ya kuchapisha uchochezi

Ofisi ya Tovuti hiyo imevamiwa na Maafisa wapatao 200. Polisi wasema waliidhinishwa kukamata nyenzo muhimu za Habari

Soma - https://jamii.app/StandNewsHK

#PressFreedom
NACHINGWEA: Wananchi waliouziwa Ardhi kuanzia Juni 2020 mpaka Desemba 2021 wametakiwa kurudisha Ardhi kwani mauziano hayo ni batili

DC Hashim Komba amesema Serikali ilisitisha ugawaji wa Ardhi tangu Juni 2020 mpaka pale itakapotoa mwongozo rasmi

Soma - https://jamii.app/ViwanjaNachingwea
#COVID19: Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema athari inayotokana na Kirusi cha Corona aina ya Omicron bado ipo juu. Maambukizi ulimwenguni yameongezeka kwa 11% wiki iliyopita

Ushahidi waonesha #Omicron ina ukuaji wa haraka zaidi

Soma - https://jamii.app/WHOOmicron

#UVIKO3
SOMALIA: JUMUIYA ZA KIMATAIFA ZAINGILIA MVUTANO WA RAIS NA WAZIRI MKUU

Rais Mohamed Abdullahi alimsimamisha kazi Waziri Mkuu, Mohammed Roble kufuatia tuhuma za ufisadi, kitendo ambacho Waziri Roble amesema ni jaribio la Mapinduzi

Soma - https://jamii.app/SiasaSomalia
Marekani inapanga kuchukua hatua mpya ili kushinikiza Utawala wa Kijeshi Nchini #Myanmar kurudisha Serikali ya Kiraia kutokana na kukandamizwa kwa Wapinzani

UN imetahadharisha juu ya ongezeko la visa vya ukiukwaji wa Haki za Binadamu

Soma - https://jamii.app/USvsMyanmar

#Democracy
DARFUR, SUDAN: GHALA LA WFP LAVAMIWA NA WATU WENYE SILAHA

Ghala la Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) lilikuwa na Tani 1,900 za Chakula cha Msaada

Darfur imeshuhudia ongezeko la mapigano tangu Oktoba kutokana na migogoro ya ardhi na maji

Soma - https://jamii.app/WFPLooted
ZANZIBAR: Rais Hussein Mwinyi amemteua Charles Martin Hilary kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano - Ikulu

Yusuph Nassor ameteuliwa kuwa
Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya Viwango (ZBS) na Dkt. Idrissa Hija kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Uhaulishaji Ardhi

Soma - https://jamii.app/UteuziZnz3
ASHRAF GHANI: SIKUWA NA NAMNA NYINGINE ZAIDI YA KUKIMBIA AFGHANISTAN

Rais wa zamani wa #Afghanistan amekanusha kuwepo mazungumzo ya kuwaachia #Taliban Madaraka kwa amani, kama walivyodai Maafisa wa zamani wa Afghanistan na Marekani

Soma - https://jamii.app/AshrafGhaniFlee
#JFLeo
AFRIKA KUSINI YALEGEZA KANUNI ZA KUDHIBITI COVID-19

Serikali inaamini Nchi imepita kilele cha Wimbi la Nne

Marufuku ya watu kuwa nje kuanzia saa sita usiku imeondolewa. Mikusanyiko ya ndani haitakiwi kuzidi watu 1,000 na nje watu 2,000

Soma - https://jamii.app/OmicronSA

#UVIKO3
👍1
CHINA: WACHEZAJI MPIRA WAPIGWA MARUFUKU KUCHORA TATTOO

Mamlaka ya Michezo Nchini #China imepiga marufuku Wachezaji wa Timu ya Taifa na Wanamichezo wengine kujichora #Tattoo na kuamuru walionazo waziondoe ili kuwa mfano mzuri kwa Jamii

Soma - https://jamii.app/TattooBanChina
#Sports