JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
DROO YA #UEFA: MAN. UTD YAPANGIWA PSG, CHELSEA YAPEWA LILLE

- Droo ya Klabu Bingwa Ulaya hatua ya 16 Bora imefanyika leo ambapo Bingwa Mtetezi, Chelsea atakutana na Lille

- PSG itakutana na Man. Utd, Man. City itaivaa Villarreal na Liverpool itakutana na Salzburg

#JFSports #UCL
Taarifa ya Mwezi ya Maendeleo ya Uchumi inayotolewa na BoT imeonesha 23.2% ya Fedha zinazokopwa nje ya Nchi zimetumika kwa usafiri na Mawasiliano Oktoba 2021

16.2% ya Fedha hizo hutumika kwa ustawi wa Jamii na Elimu. Sekta ya Utalii imetumia 1.0%

Soma - https://jamii.app/DeniFedha
IRINGA: WATU 9 WAFARIKI KWA AJALI YA GARI LA MAGAZETI

Watu tisa wamefariki na wengine 3 kujeruhiwa baada ya Gari lililokuwa linatokea Dar kuelekea Mbeya kupata ajali Kijiji cha Mahenge

Chanzo cha Ajali hiyo ni Mwendokasi

Soma - https://jamii.app/AjaliMagazeti

#JamiiForums
#UEFA: DROO YA HATUA YA 16 KURUDIWA

- UEFA imesema droo hiyo itachezeshwa upya baada ya Man. Utd kwa bahati mbaya kupangwa dhidi ya Villarreal wakati timu hizo zimetoka kundi moja

- Pia, Man. Utd kuondolewa kama moja ya timu zinazoweza kukutana na Atletico Madrid

#JFSports
BoT: NDANI YA MWAKA, MASHIRIKA YA UMMA YAMEONGEZA KUKOPA NJE KWA 1024.2%

Taasisi za Umma zilikuwa zinadaiwa Tsh. Bilioni 119.1 Oktoba 2020 na Oktoba 2021 zinadaiwa Tsh. Trilioni 1.174

Deni la Taifa limeongezeka kwa Tsh. Trilioni 10.1 ndani ya Mwaka

Soma https://jamii.app/MashirikaYaUmma
Unafahamu vitu vinavyoweza kukuweka katika hatari ya kupata Kiharusi?

Je, ni kwa kiasi gani mwenendo wako wa maisha unaweza kupelekea kupata Kiharusi?

Kufahamu zaidi, Ungana nasi katika Mjadala na Wataalamu utakaofanyika Clubhouse leo Desemba 13

Link - https://www.clubhouse.com/join/jamiiforums/YcIowdFT/xkaQ6BkE
DROO YA #UCL: CHELSEA vs LILLE, MAN. UTD vs ATLETICO

- Baada ya droo ya hatua ya 16 Bora kurudiwa, Chelsea imepewa Lille huku Man. Utd ikipewa Atletico Madrid

- PSG itakutana na R. Madrid, Juventus vs Villarreal, Man. City vs Sporting CP na Liverpool vs Inter Milan

#JFSports
Fuatilia Mjadala huu unaoendelea hivi sasa ndani ya Clubhouse ya JamiiForums

Link - https://www.clubhouse.com/join/jamiiforums/YcIowdFT/xkaQ6BkE

#JamiiForums
Yanayojiri katika Mjadala kuhusu Magonjwa ya Kiharusi na Kupooza unaoendelea hivi sasa kupitia Clubhouse

Ungana nasi - https://www.clubhouse.com/join/jamiiforums/YcIowdFT/xkaQ6BkE

#JamiiForums #Stroke #Kiharusi
JF SCHEDULED MAINTENANCE

Kuanzia saa Sita Kamili hadi saa Nane Kamili usiku wa leo tovuti ya JamiiForums.com itakuwa haipatikani kufuatia maboresho yanayotarajiwa kufanyika wakati huo

Tunashukuru kwa kuendelea kutumia huduma zetu na asante kwa ushirikiano wako

#JamiiForums
MAREKANI: Wamarekani 40,000 wametapeliwa kupitia matangazo ya kujifanya Kampuni inatoa zawadi. Utapeli unaozidi kukua kwa miaka 3 iliyopita

Kwa miezi tisa ya mwanzo ya Mwaka 2021 jumla ya Dola milioni 148 sawa na Tsh. Bilioni 340.6 zimetapeliwa

Soma - https://jamii.app/UtapeliWaZawadi