JamiiForums
βœ”
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MARUDIO YA MITIHANI YA UTABIBU NTA LEVEL 5 KUFANYIKA KUANZIA DESEMBA 13

Mitihani itafanyika pamoja na Mitihani ya marudio kwa Wanafunzi ambao hawakufanya vizuri Mitihani ya awali

Ratiba za Mitihani kwa kozi zote za #Afya zimetumwa Vyuoni

Soma - https://jamii.app/NTALevel5Dec13

#JFLeo
Ndoa za Utotoni ni ukiukwaji mkubwa wa Haki za Binadamu kwa Wasichana. Sheria ya Ndoa bado inaruhusu Mtoto wa Kike kuolewa na umri wa miaka 15

Takwimu za Utafiti wa Idadi ya Watu na Afya (TDHS), 2015-2016 zilionesha 36% ya Mabinti wenye miaka 20 hadi 24 waliolewa kabla hawajatimiza miaka 18

Soma - https://jamii.app/SheriaNdoaWatoto

#16DaysOfActivism2021
MDAU: MFUMO WA ELIMU UBADILISHWE, MIAKA YA KUSOMA IPUNGUZWE

Anasema Jamii ya Watanzania inaamini Mtoto mwadilifu ni yule anayefuata njia sahihi za Masomo. Inamtaka aanze kwa kusoma mpaka Darasa la Saba kisha afaulu hadi Chuo Kikuu

Anaeleza, kutokana na mabadiliko ya teknolojia na jamii kiujumla, ni lazima kuwepo namna ya kubadili Mfumo mzima wa Elimu hasa katika kupunguza idadi ya miaka ambayo Wanafunzi hutumia kwenye masomo

Soma - https://jamii.app/MfumoElimuSOC

#StoriesOfChange
SERIKALI KUFANYA MSAKO KWA WATAKAOFUNDISHA WATOTO WAKATI WA LIKIZO

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Dkt. Leonard Akwilapo amesema Shule zote za Serikali na Binafsi zitapelekewa Barua kuweka msisitizo wa utekelezaji wa agizo hilo

Asema Maafisa Elimu wamesoma somo la Saikolojia na wanajua umuhimu wa mapumziko katika makuzi ya Mtoto hivyo hawapaswi kufungia Macho vitendo hivi

Soma - https://jamii.app/MsakoShuleLikizo
Wakimbizi wa Rohingya walio Uingereza na Marekani wamefungua Mashtaka dhidi Kampuni ya Meta (Facebook). Wanadai Fidia ya Dola za Marekani Bilioni 150 wakisema Mitandao ya Kampuni hiyo ilichochea ghasia dhidi yao

Soma - https://jamii.app/FBSued
KENYA: POLISI AUA WATU 6 AKIWEMO MKEWE KISHA KUJIUA

Benson Imbatu alienda nyumbani akiwa na AK47 kisha kuanzisha ugomvi na Mkewe, Carol Imbatu

Majirani na Waendesha Pikipiki waliouawa walisogea karibu na nyumbani kwake baada ya kusikia risasi

Soma - https://jamii.app/PolisiAua6
USINYWE POMBE KUPINDUKIA BAADA YA KUPATA CHANJO YA COVID-19

WHO inasema unywaji pombe kistaarabu baada ya Chanjo hauna madhara

Inashauriwa kunywa kistaarabu walau kwa wiki 2 baada ya kupata chanjo ili kuipa nafasi ifanye kazi kwa ufanisi

Soma - https://jamii.app/ChanjoPombeKiasi

#UVIKO3
MDAU: SHULE ZINATUWEKA KATIKA UMASIKINI PASIPO KUJUA

Anasema Shule hazitufundishi kuhusu Maisha. Wanafunzi wanatumia miaka mingi Shuleni bila kufundishwa jinsi ya kupata Fedha, Afya ya Akili, Kodi, usimamizi wa muda n.k

Una maoni gani kuhusu hoja za Mshiriki huyu wa 'Stories Of Change'?

Msome zaidi - https://jamii.app/ShuleUmasikini
#StoriesOfChange
Mapungufu yaliyobainishwa na CAG 2019/20 katika Ukaguzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu yamesababisha athari mbalimbali

Kiasi ambacho hakikurejeshwa na kiasi ambacho hakijatengwa kimefikia Tsh. Bilioni 30.9. Kama kiasi hicho kingekopeshwa kwa vikundi vya watu 10 na kila kikundi kupewa Tsh. Milioni 5, kingeweza kuwasaidia watu 61,800

Soma - https://jamii.app/MfukoUwezeshaji

#JFUwajibikaji
MBEYA: MKUU WA MKOA AZUIA LIKIZO KWA WATUMISHI WA SERIKALI

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amesema hatopokea barua za likizo pasipo kupata taarifa za kukamilika kwa ujenzi wa Madarasa, Madawati na maeneo yaliyotengwa kwaajili ya Machinga

Soma - https://jamii.app/NoLikizoMbeya
#JFLeo
ULINZI WA TAARIFA ZAKO KWENYE KOMPYUTA

1. Hakikisha una 'Update Window' yako ili kuweza kuwa katika usalama zaidi. Ili usipate tabu ya kufanya hivi basi ni vizuri kuweka 'Automatic Updates'

2. Zingatia Matumizi ya #AntiVirus zenye nguvu ambazo zitaweza kukulinda na mashambulizi hasa ya Kimtandao

3. Kama unatumia sana Mtandao kwenye shuguli zako hakikisha una 'Addons' zinazoweza kukuonesha ubora wa tovuti unazotembelea

Soma - https://jamii.app/SecureLaptop
#DataProtection
TANESCO: TANZANIA KUUZA UMEME KENYA, UGANDA NA MALAWI

TANESCO imesema mchakato wa kuuza umeme nje ya nchi umeanza kwa ujenzi wa njia za usambazaji kwenda Malawi, Uganda na Kenya

> Shirika limesema β€œTutakapokuwa na umeme mwingi zaidi, tutauza nje ya nchi”

Soma https://jamii.app/UmemeNjeNchi
Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema Chanjo dhidi ya #COVID19 ambazo tayari zipo bado zinapaswa kuwalinda watu wanaopata maambukizi ya Kirusi cha #Omicron

Shirika lasema hakuna dalili ya aina mpya inayokataa Chanjo kuliko aina nyingine

Soma - https://jamii.app/ChanjoOmicron

#UVIKO3
Marekani imetangaza vikwazo dhidi ya Mkuu wa Idara ya Ujasusi wa Jeshi la #Uganda, Meja Jenerali Abel Kandiho kwa ukiukwaji wa #HakiZaBinadamu uliofanywa chini ya uangalizi wake

Imesema Maafisa wa Jeshi wamenyanyasa Raia kwa kukosoa Serikali

Soma - https://jamii.app/UGSanctions
MTWARA: RC ATOA SAA 48 ZA KUKAMILISHA MADARASA 452

Brigedia Jenerali Marco Gaguti ameagiza Halmashauri zote kukamilisha Madarasa yanayojengwa kwa Fedha za #COVID19 hadi kufikia Desemba 10

Madarasa hayo yatakuwa na thamani ya Tsh. bilioni 11.67

Soma - https://jamii.app/Saa48MadrsMTW
ONGEZEKO LA MATUKIO YA UKATILI MAJUMBANI

Kifungu cha 66 cha Sheria ya Ndoa, kimegusia adhabu kwa Wenza, kwamba hakuna Mtu anayeruhusiwa kutoa adhabu kwa Mwenza wake, lakini hakijatoa adhabu kwa mhalifu wa kosa hilo

Aidha, kifungu hiki kinazuia Unyanyasaji wa Kimwili kati ya Wanandoa, na kuacha aina nyingine za Unyanyasaji ambao ni pamoja na Kihisia, Kisaikolojia, Ngono na Kiuchumi

#16DaysOfActivism2021
MUSOMA: Marco Saidi (68) amekamatwa kwa tuhuma za kuwalewesha abiria kwenye Mabasi yanayofanya safari zake kati ya Mwanza - Musoma na kuwaibia

Anadaiwa kuweka Dawa ya Kienyeji ya Khabharagata kutoka Congo kwenye Maji, Soda, Biskuti na Pipi

Soma - https://jamii.app/MbaroniKuleweshaAbiria

#JFLeo
MDAU: VICHOCHEO VYA MABADILIKO ILI TANZANIA TUNAYOITAKA IPATIKANE

1) Utawala wa Sheria na wa Haki: Kuna umuhimu wa kuwa si tu na Katiba Mpya, bali Katiba bora inayoweka misingi mizuri ya mgawanyo mzuri wa madaraka na mamlaka na uendeshaji wa shughuli za Serikali na Sera za Taifa

2) Uhuru wa Maoni: Wananchi wana Haki ya kutoa maoni na kufikisha ujumbe wao kwa Mamlaka husika kwa njia zinazokubalika Kikatiba

Soma - https://jamii.app/MabadilikoTZ

#StoriesOfChange
CHINA YATAJWA KUWA MKAMATAJI MKUBWA ZAIDI WA WAANDISHI WA HABARI

Ripoti ya Reporters Without Borders inasema Wanahabari 127 wanashikiliwa hivi sasa

China imekuwa ikifanya kile kilichotajwa kama kampeni ya ukandamizaji dhidi ya Uandishi wa Habari

Soma - https://jamii.app/RipotiRSFChina
Katika siku za karibuni mitandao ya kijamii na Mifumo ya Kidijitali imekuwa maeneo muhimu kwa Jamii ya Tanzania kutumia #UhuruWaKujieleza na kupigania haki zao nyingine

Tukifurahia Miaka 60 ya Uhuru wa #Tanganyika ni kwa kiwango gani tumeweza kuitumia mifumo ya Dijitali katika kusimamia Haki za Binadamu, Demokrasia na Utawala Bora?

Ungana nasi katika Mjadala huu utakaofanyika kupitia Clubhouse Desemba 9, 2021

#JamiiForums #DigitalSpaces #Democracy