JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
TAKWIMU: Vitabu vya Biashara kwa Wanafunzi wa Kidato cha 5 na 6 ni vichache ikilinganishwa na masomo mengine

Mwaka 2021, kulikuwa na vitabu 378 vya Accountancy, 392 Commerce na 4,057 Economics. Shule za Serikali zina vitabu vingi zaidi vya Kemia

Soma - https://jamii.app/VitabuBiashara
SERIKALI: HATUJABAINI KIRUSI CHA OMICRON MPAKA SASA

Yasema Maabara ya Taifa imekuwa ikichunguza mabadiliko ya kirusi kuangalia uwepo wa anuai zinazotokana na mabadiliko ya #COVID19, ikiwemo Omicron

Wananchi wasisitizwa kuchukua tahadhari

Soma https://jamii.app/OmicronTZ

#UVIKO3
UCHAGUZI GAMBIA: Mamlaka zimemtangaza Rais Adama Barrow kuwa mshindi wa Uchaguzi Mkuu, akipata takriban 53% ya Kura huku Mpinzani Ousainou Darboe akipata 28%

Awali, Darboe na Wagombea wengine walisema wasingekubali matokeo ya Uchaguzi

Soma - https://jamii.app/BarrowGambia

#JFLeo
INDIA: WANANCHI WACHOMA MAGARI YA JESHI BAADA YA WENZAO KUUAWA KIMAKOSA

Kiongozi wa Jimbo la Nagaland, Neiphiu Rio ameamuru kufanyika uchunguzi wa haraka

Wanajeshi walililenga kwa risasi lori moja na kusababisha vifo vya Watu 6

Soma - https://jamii.app/JeshiLauaRaia

#HumanRights
SUDAN: JESHI LASEMA LITAACHIA MADARAKA BAADA YA UCHAGUZI

Jenerali Abdel Fattah al-Burhan asema Jeshi litaacha kujishughulisha na Siasa baada ya Uchaguzi wa mwaka 2023

Takriban watu 44 wamefariki kutokana na maandamano ya kupinga Jeshi

Soma - https://jamii.app/JeshiSiasaSudan

#JFLeo
Katika ukaguzi wa uendeshaji wa Mfuko wa Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, CAG alibaini;

65% ya Mikopo iliyotolewa kwenye Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu haikurejeshwa

Kwa mwaka 2019/20, CAG alionesha Mamlaka za Serikali za Mitaa 130 zilitoa Mikopo yenye thamani ya Tsh. Bilioni 42.9, lakini Tsh. Bilioni 27.8 sawa na 65% ya mikopo hiyo haikurejeshwa

Soma - https://jamii.app/MfukoUwezeshaji

#JFUwajibikaji
MDAU: MATATIZO YATOKANAYO NA UKOSEFU WA LISHE BORA KWA MTOTO

(i) Matatizo ya ukuaji: Mtoto yeyote ambaye lishe yake ni duni, huwa na matatizo ya ukuaji. Ili Mtoto akue vizuri lazima kuwe na Protini ya kutosha ambayo hufanya kazi ya kuujenga Mwili

(ii) Mtoto kuishiwa nguvu: Hii huwakuta Watoto wengi sana, ambao mara nyingi hukonda kupita kiasi. Mwili huitaji Vyakula kama Wanga, Protini na Mafuta ili uweze kuzalisha nguvu

Msome - https://jamii.app/LisheBoraAkili

#StoriesOfChange
DKT. NDUGULILE: CHANGAMOTO YA DARAJA LA KIGAMBONI NI TOZO

Mbunge wa Kigamboni amesema Changamoto kubwa ni tozo, akitolea Mfano wa Daladala moja kutozwa Tsh. 5,000 kila linapopita

Amuomba Rais Samia kuliangalia jambo hilo ili kuleta nafuu kwa Watu

Soma - https://jamii.app/TozoDarajaKigmb
RAIS SAMIA: NITAENDELEA KUZUNGUKA KUWAAMBIA WAWEKEZAJI WAJE TANZANIA

Asema, "Kama nimekubali kubeba mzigo wa kuongoza Nchi, kuna mambo kadhaa yaliyoelekezwa ndani ya Ilani niyatimize. Sitayatimiza kwa kukaa Dodoma/Magogoni, lazima nikaonane na watu"

Soma https://jamii.app/SSHWawekezajiTZ
KENYA: WASAFIRI WOTE KULAZIMIKA KUWA NA CHETI CHA CHANJO

Kenya imetangaza hatua kali zinazolenga kuzuia kuenea kwa aina mpya ya #COVID19

Waziri wa #Afya amesema ni lazima kwa wageni kuwa na cheti cha Chanjo kabla ya kuingia Nchini humo

Soma - https://jamii.app/CertVaccineKE
#UVIKO3
MYANMAR: AUNG SAN SUU KYI AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 4

Kiongozi huyo aliyetolewa Madarakani na Jeshi akutwa na hatia ya uchochezi na kuvunja Kanuni za Corona

Aung San Suu Kyi yupo kifungo cha nyumbani tangu Februari, na anakabiliwa na Mashtaka 11

Soma https://jamii.app/AungSanSuu4
COVID-19: DALILI AMBAZO HUWAPATA WATU WACHACHE

WHO imetaja dalili hizo ni Kupata maumivu ya kichwa, Kuwashwa kooni, Maumivu mwilini, kuhara, upele au vidole kubadilika rangi na macho kuwa mekundu

Unasisitizwa kwenda Kituo cha Afya ukizipata

Soma https://jamii.app/LessCommon

#UVIKO3
Vitendo vya Rushwa ya Ngono vinaendelea kushamiri kutokana na Uelewa mdogo wa Jamii juu ya #Sheria zinazozuia rushwa hiyo

Pia, Watendewa huogopa kutoa taarifa kwa hofu ya kuachishwa kazi, kunyimwa huduma, kuachishwa masomo au kufelishwa kwa makusudi kwa Wanafunzi hasa wa Vyuo Vikuu

Je, umewahi kuombwa Rushwa ya Ngono au kushuhudia Mtu akiombwa Rushwa ya Ngono?

#16DaysofActivism2021
MDAU: UMUHIMU WA MTU/JAMII KUIFAHAMU AFYA YA AKILI

1. Husaidia kuweza kutambua changamoto ndogondogo zinazoweza kupelekea tatizo la Akili ikiwemo Msongo wa Mawazo ambao usipopatiwa ufumbuzi, hupelekea tatizo la Akili liitwalo Sonona (#Depression)

2. Kuitambua Afya ya Akili kunasaidia kupambana na shida ya kiwewe (Post Traumatic #Stress Problem) inayosababishwa na majanga mbalimbali ikiwemo kufiwa na Mtu wa karibu sana

Msome - https://jamii.app/BenefitsAfyaAkili

#StoriesOfChange
AFRIKA KUSINI: Rais Cyril Ramaphosa anasema Hospitali zinaandaliwa kulaza wagonjwa zaidi, wakati Kirusi cha #Omicron kikiendelea kuenea na kupelekea Wimbi la 4

Amewataka Wananchi kuvaa barakoa na kuepuka misongamano ili kupunguza maambukizi

Soma https://jamii.app/Wave4SA

#UVIKO3
GOBA, DAR: Watu wanne (Wanawake 2 na Wanaume 2) wameripotiwa kufariki dunia huku wengine 17 wakijeruhiwa baada ya jengo lililokuwa linajengwa eneo la Goba kwa Awadhi Jijini Dar es Salaam kuangukia nyumba za jirani

Soma - https://jamii.app/GobaVifo4

#JFLeo
LUDEWA: AJINYONGA BAADA YA KUTOTAJWA JINA KWENYE MISA

Raban Razalo (48) amejinyonga na waya kwa madai ya kutoridhishwa na kitendo cha Mchungaji kutomtaja jina wakati wa misa ya shukrani iliyofanywa na Mkewe baada ya Mtoto wao kupona mguu

Soma - https://jamii.app/BabaKifoPadri
RIPOTI: WATENGENEZAJI WA SILAHA HAWAJAPATA ANGUKO LA KIUCHUMI

Kampuni 100 za juu zimeshuhudia ongezeko la faida kwa 1.3% licha ya Uchumi wa Dunia kushuka kwa zaidi ya 3%

Marekani inaongoza ktk utengenezaji na mauzo ikiwa na Kampuni 41 kati ya 100

Soma - https://jamii.app/SIPRI2021
ETHIOPIA: Serikali imesema Vikosi vyake vimeidhibiti tena Miji ya Dessie and Kombolcha ambayo ilishikiliwa na wapiganaji wa TPLF

Hofu ya Wapiganaji kuingia Mjini #AddisAbaba imepelekea Nchi kadhaa kuwahimiza Raia wao kuondoka Nchini humo

Soma - https://jamii.app/EthiopiaWaasi
Shirika la Afya Duniani limesema vikwazo ktk Huduma za Afya vilivyotokana na COVID-19 vimepelekea vifo 69,000 zaidi vya Malaria mwaka 2020

Takriban watu 627,000 duniani (wengi watoto) kutoka Mataifa ya Afrika walifariki kwa Malaria mwaka 2020

Soma https://jamii.app/WHOMalaria