JamiiForums
52.9K subscribers
34.3K photos
2.43K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
RAIS SAMIA AMPOKEA RAIS MUSEVENI

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amempokea Rais wa Uganda, Yoweri Museveni katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere

> Rais Museveni amepewa salamu ya kijeshi, kukagua Gwaride na kuelekea Ikulu kwa mazungumzo ya faragha

#JamiiForums
UGANDA: Exim Bank imechukua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa #Entebbe na mali nyingine za Uganda baada ya kushindwa kulipa mkopo wa Dola milioni 207(Tsh. Bilioni 476.7)

> Majadiliano ya kuongezewa muda wa marejesho yaligonga mwamba

Soma https://jamii.app/EntebbeAirport
SERIKALI: KUNA TISHIO LA WIMBI LA NNE LA CORONA

Kutokana na kuibuka aina mpya ya Kirusi cha Corona kiitwacho #Omicron kinachosemekana kuwa na uwezo wa kusambaa haraka, Wizara ya Afya imesisitiza Wananchi kuendelea kujitokeza kupata chanjo

Pia, imehimiza uvaaji barakoa, unawaji mikono, kufanya mazoezi na kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima

Soma - https://jamii.app/TishioWimbi4

#UVIKO3
Rais Samia amesema #Tanzania itanunua Sukari kutoka Uganda huku akikosoa kauli ya Waziri wa Kilimo, Prof. Adolf Mkenda kuhusu kutokutoa vibali vya kununua Sukari nje ya nchi

> Prof. Mkenda alisema Sukari kutoka nje inaua Viwanda vya ndani

Soma https://jamii.app/UgandaSukari
#JFLeo
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
UGANDA: Shirika la Ndege la #Uganda limetangaza kuongeza Senene katika orodha ya Vyakula vinavyotolewa kwenye Ndege katika safari zake za Kimataifa

Hatua hiyo imekuja baada ya Wasafiri kufurahia Senene waliokuwa wanauzwa na mchuuzi ktk Ndege

Soma https://jamii.app/SeneneUganda
#JFLeo
PEMBA: Watu 5 wamefariki, 12 wamelazwa baada ya kula samaki Kasa. Watatu kati ya 12 waliolazwa wana hali mbaya

> Kamanda wa Polisi Kaskazini Pemba, ACP Juma Khamis amesema ulaji wa Kasa na Bunju umepigwa marufuku baada ya kubainika kuwa na sumu

Soma https://jamii.app/PembaSamaki
NEYMAR AUMIA KIFUNDO CHA MGUU AKIWA UWANJANI

Mchezaji wa PSG, Neymar (29) ameumia kifundo cha mguu wakati timu yake ilipokuwa ikichuana na klabu ya St Etienne

> Neymar alionekana kuugulia maumivu makali dakika 5 kabla ya kipenga cha mwisho

Soma https://jamii.app/NeymarAnkle
AFRIKA KUSINI: Rais Cyril Ramaphosa ametoa wito kwa Nchi za Ulaya na Marekani kuondoa vikwazo vya safari kwa Mataifa ya Kusini mwa Afrika yenye Kirusi cha #Omicron

Asema vikwazo vinaongeza ubaguzi kwa Mataifa husika na maumivu ya Kiuchumi

Soma - https://jamii.app/CyrilBanTravel
#UVIKO3
DALILI NNE ZA COVID-19 AMBAZO HUTOKEA KWA WENGI

WHO imetaja dalili hizo ni kupata homa, kikohozi, kuhisi uchovu usio wa kawaida pamoja na kupoteza uwezo wa kuhisi ladha au harufu

Ukizipata, fika haraka Hospitali ili kupima na kutibiwa

Soma - https://jamii.app/ComonSymptoms

#UVIKO3
Je, umewahi kujiuliza nini kitatokea endapo utashindwa kutumia Uwezo ulio nao?

1. Utashindwa kufanya maamuzi sahihi juu ya Maisha yako. Mtu asiyeweza kugundua na kuendeleza Uwezo wake huwa ktk hatari ya kukosa mwelekeo

2. Kukosa kutambua Uwezo wako (potential) kutakufanya uwe mtumwa na utatumika kuendeleza kusudi la Mtu mwingine

Mshiriki wa 'Stories Of Change' anasema kiwango cha Elimu siyo sababu ya kushindwa kuendeleza Uwezo ulio nao

Soma zaidi - https://jamii.app/TumiaPotential
#StoriesOfChange
Rwanda imesitisha safari zake za Ndege kwenda Afrika Kusini, #Zambia na Zimbabwe pamoja na kurejesha Karantini ya siku 7 kwa wote wanaotoka kwenye Nchi hizo

Wasafiri watatakiwa kukaa Karantini ya saa 24 kwa gharama zao ili kufanyiwa Vipimo

Soma - https://jamii.app/RWBanFlightsSA
#UVIKO3
Kutokana na udhaifu katika mifumo ya ukusanyaji wa mapato, kuna uwezekano mkubwa wa Serikali kupoteza Tsh. Bilioni 265.85 kutokana na vitendo vya Rushwa, Udanganyifu na Ubadhirifu

Katika Serikali Kuu, kumekuwa na ongezeko la upotevu wa mapato kutoka Tsh. Bilioni 7.7 kwa 2018/19 mpaka Tsh. Bilioni 38.7 kwa Mwaka 2019/20

Soma - https://jamii.app/UpotevuFedha
#JFUwajibikaji
AUSTRALIA KUTUNGA SHERIA YA KUONESHA UTAMBULISHO WA WATUMIAJI WA MITANDAO

Imepanga kutunga Sheria hiyo kuiwajibisha Mitandao ya Kijamii kwa maudhui yanayochapishwa na watumiaji

Serikali yasema Uhuru wa kutoa maoni unapaswa kuendana na Uwajibikaji

Soma - https://jamii.app/WasiojulikanaMitandaoni
WHO YAHIMIZA KUTOFUNGIA MATAIFA KWA HOFU YA KIRUSI CHA OMICRON

Shirika la Afya Duniani limesisitiza kufuata Kanuni za Kisayansi za Kimataifa za 2005

Limesema Afrika Kusini na Botswana ni za kupongezwa kwa kuwa na uwazi kuhusu #Omicron

Soma - https://jamii.app/SABotswana
#UVIKO3
Wizara ya Mambo ya nje ya #Morocco imesitisha Safari za Ndege za kuingia Nchini humo kwa muda wa wiki 2 kutokana na aina mpya ya Kirusi cha #Omicron

Asilimia 66 ya Watu wa Taifa hilo tayari wamepokea walau dozi moja ya Chanjo ya #COVID19

Soma - https://jamii.app/MoroccoFlightsBan
#UVIKO3
Waziri wa Kilimo, Prof. Adolf Mkenda amesema bei za mafuta ya kupikia zimepanda kwasababu 55% ya mafuta yanaagizwa kutoka nje

Athari za #COVID19 zimefanya uzalishaji kuwa finyu. Sababu nyingine ya bei kupanda ni gharama za usafirishaji

Soma - https://jamii.app/MafutaKupikia

#JFLeo
Sheria zinazolinda na kuzuia #UkatiliWaKijinsia Mitandaoni ni pamoja na Kanuni ya Maudhui ya Mtandaoni (OCR) 2020 ambayo inakataza kurusha Maudhui ya Udhalilishaji ikiwamo Picha/Video za Utupu

Ukatili wa Kijinsia Mtandaoni unazidi kukithiri kutokana na Uelewa mdogo wa Watumiaji, Utamaduni wa Jamii kukaa kimya badala ya kukemea pale unapoona Vitendo vya Ukatili

Soma - https://jamii.app/SheriaUkatiliOnline

#16DaysofActivism