JamiiForums
52.9K subscribers
34.3K photos
2.42K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Yanayojiri katika Mjadala wa "Je, Demokrasia inakwamisha Maendeleo?" unaoendelea kupitia Clubhouse

#Democracy #JamiiForums
TETESI: MANCHESTER UNITED KUMPA RANGNICK UKOCHA WA MUDA

- Inadaiwa Klabu ya Man. Utd imefikia makubaliano na Kocha Ralf Rangnick (63) ili awe kocha wao wa muda hadi mwisho wa msimu 2021 - 22

- Rangnick amewahi kuwa Kocha wa Hannover, Schalke, Hoffenheim na RB Leipzig

#JFSports
SUDAN: Maelfu ya watu wameandamana Jijini #Khartoum pamoja na Miji mingine. Vikosi vya Usalama vimetumia mabomu ya machozi dhidi ya Waandamanaji huko Omdurman

Wananchi wamepinga Makubaliano yaliyomrejesha Madarakani Waziri Mkuu, Abdalla Hamdok

Soma - https://jamii.app/ProtestsKhartoum
Ili kutatua kasoro zilizoainishwa katika Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo, Serikali inashauriwa kuwezesha Halmashauri kukamilisha miradi iliyoanza kabla ya kuanza miradi mipya

Pia, Taasisi ya WAJIBU inashauri Wizara ya Fedha na Mipango (Hazina) pamoja na watekeleza miradi kufuata makubaliano waliojiwekea na Washirika wa Maendeleo

Soma - https://jamii.app/MapungufuMiradi

#JFUwajibikaji
AINA MPYA YA KIRUSI CHA CORONA YAGUNDULIKA AFRIKA KUSINI

Wanasayansi Nchini humo wameelezea wasiwasi wao kuhusu aina mpya ya Kirusi cha Corona kiitwacho B.1.1.529

Wataalamu wa Shirika la Afya Duniani(WHO) wanatarajiwa kukutana kukitathmini

Soma https://jamii.app/NewVariantSA

#UVIKO3
Jamii Forums inatoa nafasi 2 za ajira kwa Wasanifu Grafiki (Graphic Designers)

MAJUKUMU: Kuandaa na kusanifu picha kulingana na mahitaji, Kuandaa na kuhariri picha mjongeo zitakazotumika kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii

Kwa Maelezo zaidi tembelea - https://jamii.app/GraphicDesignersJF
MADHARA YA UKATILI WA KIJINSIA MITANDAONI

Ukatili una madhara Kisaikolojia, na unaweza kupelekea watendewa kupata Msongo wa Mawazo/kupoteza mwelekeo

Pia, inajenga hofu na kuvunja moyo Wanawake kushiriki kwenye ngazi za Uongozi

Soma - https://jamii.app/UkatiliMitandao

#16DaysofActivism
MDAU: MAPENDEKEZO YA HATUA ZA KUCHUKUA KUPUNGUZA WIZI WA FEDHA ZA UMMA

Amesisitizia suala la Uwazi akisema ukiwepo, ni rahisi hata kwa Wananchi kufuatilia na kutoa taarifa mapema pale inapoonekana mradi unafanyika ndivyo sivyo

Anasema TAKUKURU haitakiwi ifanye kazi kwa kupewa maelekezo bali inatakiwa inuse viashiria vya rushwa kila sehemu na ijikite zaidi kufanya kazi kwa kushirikiana na wananchi

Soma Makala yake - https://jamii.app/WiziFedhaUmma

#StoriesOfChange
AFYA: Namna Mgonjwa anavyojieleza kwa Daktari ni muhimu. Baadhi ya masuala ya kuzingatia unapojieleza kwa Daktari ni;

1) Usimwambie Daktari Ugonjwa wako (Diagnosis), bali mueleze dalili ulizonazo: Kufahamu Ugonjwa ni kazi ya Daktari, unachotakiwa kufanya ni kuelezea dalili zako

2) Usiseme uongo wala kuficha kitu kuhusu Afya yako: Kumdanganya Daktari kutapelekea ashindwe kubaini tatizo. Anategemea maelezo yako kuweza kugundua tatizo

Soma - https://jamii.app/KujielezaDaktari

#Afya
#COVID19: Mataifa kadhaa yakiwemo Singapore, Ufaransa, Kenya na Japan yameanza kuchukua hatua baada ya Afrika Kusini kuripoti aina mpya ya Kirusi cha Corona

WHO yasema itachukua wiki kadhaa kuelewa madhara ya Kirusi cha B.1.1.529

Soma - https://jamii.app/NewVariantSA

#UVIKO3
RAIS MUSEVENI KUFANYA ZIARA YA KIKAZI TANZANIA

Rais wa Uganda na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan watafanya mazungumzo na kushiriki ufunguzi wa kongamano la biashara

Rais Museveni atatembelea Bandari ya Dar na kukagua mradi unaoendelea wa SGR

Soma https://jamii.app/ZiaraMuseveni
Takwimu kutoka tovuti ya Global Stats Counter zinaonesha kivinjari (Browser) cha Chrome kinachomilikiwa na Kampuni ya #Google kinatumiwa na watu wengi zaidi

Kinatumiwa na zaidi ya 64% ya watumiaji wote wa intaneti duniani, ikifuatiwa na kivinjari cha Safari

#JamiiForums
Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI, Ummy Mwalimu amewaagiza wakuu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha Wanafunzi wanapumzika wakati wa likizo ili kujifunza mambo ya kijamii

Amelaumu tabia ya kubidhaisha Elimu kwa kuwatoza Fedha Wazazi kipindi cha likizo

Soma - https://jamii.app/LikizoWanafunzi

#JFLeo
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amefunguliwa kesi kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka

> Kesi hiyo inatarajiwa kuanza kusikilizwa Desemba 3, 2021

Soma https://jamii.app/Desemba3

#JFLeo
MAREKANI: Kirusi cha COVID19 aina ya Omicron kilichogundulika Afrika Kusini kimeonekana kuwa hatari zaidi

> Raia kutoka Botswana, Eswatini, Lesotho, Malawi, Mozambique, Namibia, Afrika Kusini na Zimbabwe hawataruhusiwa kuingia Marekani

Soma https://jamii.app/OmicronVariant

#UVIKO3