JamiiForums
βœ”
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Kumekuwa na mjadala wa muda mrefu ukiituhumu Demokrasia kukwamisha Maendeleo huku wengine wakidai kuwa ili maendeleo yatokee kunahitajika utawala wa kiimla

Je, wewe una mtazamo gani kuhusu hili?

Ungana nasi katika Mjadala utakaofanyika kuanzia saa 12 jioni kupitia Clubhouse

Link - https://www.clubhouse.com/join/jamiiforums/3RJTuGde/P08pBBww
SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA

Hii ni Kampeni ya Kimataifa ya kila mwaka inayoanza Novemba 25 na kuhitimishwa Desemba 10

Siku hii inalenga kuhamasisha Raia na Mashirika duniani kote kupaza sauti kuhusu kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Wasichana

Soma - https://jamii.app/16DaysActivism

#OrangeTheWorld #16DaysofActivism
Rais Samia Suluhu amesema Tanzania ni miongoni mwa Nchi 10 za Afrika ambazo Uchumi unakua kwa kasi

Asema, "Tumeona viashiria vya Maendeleo kwenye Maendeleo ya mtu. Tumeweza kupunguza kiwango cha umasikini kutoka 28.6% (2015) hadi 26.2% (2020)

Soma - https://jamii.app/MkutanoTaasisiFedha
PROF. BISANDA AOMBA HESLB WAFADHILI WANAFUNZI WANAOSOMA CHUO KIKUU HURIA

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria #Tanzania, Prof Elifas Tozo amesema wanakumbana na changamoto ya Bodi ya Mikopo kutowatambua Wanafunzi wao, hivyo hutoa mikopo kwa wachache

Soma - https://jamii.app/OUTHESLB
BURKINA FASO: Serikali imeongeza muda wa kusitishwa Huduma za Intaneti, ikielezwa hatua hiyo inatokana na sababu za Kiusalama

Wapinzani wa Rais Kabore wameitisha maandamano mapya kupinga Serikali kushindwa kuzuia ghasia zinazofanywa na Wanamgambo

Soma - https://jamii.app/InternetBurkinaFaso
RC MAKALLA: KUNA WANAUME WANANYANYASWA NA WANAWAKE WENYE FEDHA

RC wa Dar amesema β€œWapo Wanaume wanaonyanyaswa. Kuna Wanawake wana Fedha wanahitaji tu Wanaume wa kuwaoa, anaweza kumpa kitu Mwanaume na kumnyang’anya wakiachana”

Soma - https://jamii.app/MakallaGBVMen

#16DaysofActivism2021
UTUMIKISHAJI WATOTO AFRIKA MAGHARIBI NA KATI WAONGEZEKA

Wanatumiwa kama wapiganaji, wapelelezi, wapishi, walinzi na wabeba mizigo

Watoto 21,000 waliandikishwa na Vikosi vya Kijeshi na makundi yenye silaha kati ya 2016 na 2020

Soma - https://jamii.app/ChildLabourWA

#ChildViolence
SERIKALI: NGUVU YA PAMOJA INAHITAJIKA KUKOMESHA UKATILI WA KIJINSIA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema licha ya Sheria kali bado Ukatili unajitokeza

Asema, "Rushwa ya ngono imekua changamoto Vyuo Vikuu na maeneo ya kazi"

Soma - https://jamii.app/VitendoUkatiliTZ

#16DaysofActivism2021
AFRIKA KUSINI: Serikali imeomba Kampuni za Johnson & Johnson na #Pfizer kuchelewesha utoaji wa Chanjo kutokana na kuwa na Chanjo nyingi kwenye maghala

35% ya Wananchi wameshapata Chanjo kamili huku Nchi ikiwa na dozi Milioni 16.8 ghalani

Soma - https://jamii.app/StockVaccineSA

#UVIKO3
Kumekuwa na mjadala wa muda mrefu ukiituhumu Demokrasia kukwamisha Maendeleo huku wengine wakidai kuwa ili maendeleo yatokee kunahitajika utawala wa kiimla

Je, wewe una mtazamo gani kuhusu hili?

Ungana nasi katika Mjadala kuanzia saa 12 jioni kupitia Clubhouse

Link - https://www.clubhouse.com/join/jamiiforums/3RJTuGde/P08pBBww
Aidan Eyakuze: Demokrasia inaturuhusu sisi kama binadamu wa nchi fulani kujiuliza maswali 2 ya msingi

1. Nani atazalisha yale yote tunayohitaji kama binadamu?

2. Nani atalipia uzalishaji huo?

Fuatilia - https://www.clubhouse.com/join/jamiiforums/3RJTuGde/P08pBBww

#JamiiForums #Democracy
Fuatilia Mjadala huu kupitia Clubhouse ya JamiiForums

#Democracy #JamiiForums
Yanayojiri katika Mjadala wa "Je, Demokrasia inakwamisha Maendeleo?" unaoendelea kupitia Clubhouse

#Democracy #JamiiForums
TETESI: MANCHESTER UNITED KUMPA RANGNICK UKOCHA WA MUDA

- Inadaiwa Klabu ya Man. Utd imefikia makubaliano na Kocha Ralf Rangnick (63) ili awe kocha wao wa muda hadi mwisho wa msimu 2021 - 22

- Rangnick amewahi kuwa Kocha wa Hannover, Schalke, Hoffenheim na RB Leipzig

#JFSports
SUDAN: Maelfu ya watu wameandamana Jijini #Khartoum pamoja na Miji mingine. Vikosi vya Usalama vimetumia mabomu ya machozi dhidi ya Waandamanaji huko Omdurman

Wananchi wamepinga Makubaliano yaliyomrejesha Madarakani Waziri Mkuu, Abdalla Hamdok

Soma - https://jamii.app/ProtestsKhartoum