JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KUTOKUWA NA CHA KUFICHA, HAIMAANISHI FARAGHA YAKO ISIHESHIMIWE

Watu wengi hudhani ‘Kukosa cha kuficha’ humaanisha Faragha haina umuhimu. Lakini hata kama chumbani hauna kitu cha kuibwa haina maana uache mlango wazi

Suala la faragha ni zaidi ya kuogopa vitu kuibwa, bali kuwa na staha ya vitu vyako. Hata kama unahisi hauna cha kupoteza Mtandaoni, jali kuhusu faragha yako

Soma - https://jamii.app/DataPrivacy
#DataPrivacy
UN: KILA SEKUNDE 24 MTU 1 HUFARIKI KWA AJALI ZA BARABARANI

Idadi hiyo ni sawa na Watu 3 ndani ya dakika Moja. 90% ya vifo vya Barabarani hutokea Nchi za kipato cha chini na kati

UN imetoa wito wa umuhimu wa kupunguza mwendokasi ili kuzuia ajali

Soma - https://jamii.app/AjaliVifo
KESI YA MBOWE: Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imetupilia mbali Hoja 3 zilizotolewa na Utetezi

Mawakili Upande wa Utetezi walipinga kitabu cha kumbukumbu za mahabusu cha Kituo Kikuu cha Polisi, Dar es Salaam kupokelewa kama kielelezo cha ushahidi Upande wa Mashtaka

Soma - https://jamii.app/JajiPingamizi3

#JFLeo
GEITA: AHUKUMIWA MIAKA 3 AU FAINI YA TSH MILIONI 2 KWA KUPOKEA RUSHWA

Aliyekuwa Kaimu Mkuu wa Idara ya Maji Wilaya ya Geita, Eng. Rael Buliba alipokea rushwa ya Tsh. Milioni 75 kutoka kwa Mkandarasi ili kuongeza muda wa kusambaza mabomba ya Maji

Soma - https://jamii.app/Milioni2Faini
ZANZIBAR: UNGUJA YATAJWA KUONGOZA KWA UKAHABA NA USHOGA

Waziri Dkt. Saada Salum Mkuya amesema #Unguja ina Wanawake 4,854 na Pemba 700 wanaofanya Biashara ya kuuza miili yao

Wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja #Zanzibar ni 3,300

Soma - https://jamii.app/UshogaUkahaba
MAPUNGUFU KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO

Ripoti ya CAG ilibaini Mamlaka ya Serikali za Mitaa 152 hazikupokea Tsh. Bilioni 410.4 sawa na 46% ya Fedha za Miradi ya Maendeleo kwa Mwaka wa Fedha 2019/20

Hazina na Washirika wa Maendeleo hawakutoa Fedha za Miradi ya Maendeleo kiasi cha Tsh. Bilioni 53.4 sawa na 22% ya Bajeti iliyoidhinishwa

Soma - https://jamii.app/MapungufuMiradi

#JFUwajibikaji
Jamii Forums inatoa nafasi 2 za ajira kwa Wasanifu Grafiki (Graphic Designers)

MAJUKUMU: Kuandaa na kusanifu picha kulingana na mahitaji, Kuandaa na kuhariri picha mjongeo zitakazotumika kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii

Kwa Maelezo zaidi tembelea - https://jamii.app/GraphicDesignersJF
MDAU: UWAJIBIKAJI NI KICHOCHEO CHA UTAWALA BORA

Anasema Nchi hukumbwa na madhara makubwa kwa kukosa Utawala Bora, ikiwemo kuongezeka vitendo vya unyanyasaji, upendeleo, rushwa, wizi na ubadhirifu wa mali za Umma

Kupitia Shindano la #StoriesOfChange amesisitiza suala la Uwajibikaji wa Viongozi kuhakikisha wanatawala kwa kufuata Misingi ya Haki na Usawa

Soma - https://jamii.app/UwajibikajiViongozi

#Accountability
DAR: RC Amos Makalla ametangaza Jumamosi ya kila mwisho wa Mwezi kutumika kufanya usafi kwa mkakati aliouita ‘Safisha Pendezesha Dar es Salaam’

Katika mkakati huo baadhi ya nyumba za Watu binafsi, Mashirika na Kampuni zimetakiwa kupakwa rangi

Soma - https://jamii.app/UsafiDar
#JFLeo
HOJA: LIPIA TANGAZO MTANDAONI ILI KUPATA WATEJA WANAOHITAJI BIDHAA YAKO

Mdau wa Jamiiforums.com ameandika kuhusu umuhimu wa kulipia matangazo mtandaoni ambapo hufanya bidhaa yako imfikie Mtu mwenye uhitaji nayo badala ya kumfikia Mtu yeyote

Teknolojia ya Mtandao kama #Facebook kwa matangazo yanayolipiwa huyafanya yawafikie Watu ambao walishawahi kutafuta bidhaa unayoitangaza hivyo utapata Watu wenye uhitaji na kuuza

Soma - https://jamii.app/SponsoredAds
#SponsoredAds
SERIKALI: UKIJENGA KWENYE MAENEO HATARISHI TUTABOMOA

Waziri wa Ardhi, William Lukuvi ametangaza kuvunja Nyumba zilizo maeneo hatarishi na mabondeni hata kama wamiliki wana Hati

Asema walio maeneo hatarishi mara nyingi hupewa Hati kijanja janja

Soma - https://jamii.app/NyumbaKubomolewa
MAREKANI YATAJWA KUPOROMOKA KIDEMOKRASIA

Ripoti ya Taasisi ya Kimataifa ya Demokrasia na Usaidizi wa Uchaguzi(#IDEA) imeitaja Marekani kurudi nyuma Kidemokrasia tangu 2019

Mtu 1 kati ya Watu 4 Duniani anaishi ktk Taifa linalorudi nyuma Kidemokrasia

Soma https://jamii.app/DemocracyUS
#ETHIOPIA: Wakati vita ya mwaka mzima kati ya Serikali ya Ethiopia na Vikosi vya TPLF ikikaribia Addis Ababa, Waziri Mkuu Abiy Ahmed asema ataongoza Vikosi vya Usalama

Wajumbe wamejaribu kusuluhisha mvutano lakini kumekuwa na maendeleo kidogo

Soma https://jamii.app/AbiyEthiopia
#JFLeo
SONGWE: Watu 24 wa Kijiji cha Chang’ombe wanashikiliwa kwa tuhuma za kuzingira Kituo cha Polisi Galula wakidai mikoba ya Waganga wa Jadi iliyokamatwa na Askari

Waganga maarufu lambalamba wanadaiwa kuwadhalilisha Watu wakiwatuhumu ni wachawi

Soma - https://jamii.app/24Songwe

#JFLeo
Jamii Forums inatoa nafasi 2 za ajira kwa Wasanifu Grafiki (Graphic Designers)

MAJUKUMU: Kuandaa na kusanifu picha kulingana na mahitaji, Kuandaa na kuhariri picha mjongeo zitakazotumika kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii

Kwa Maelezo zaidi tembelea - https://jamii.app/GraphicDesignersJF
Ripoti ya CAG 2019/20 ilibaini zaidi ya Miradi ya Maendeleo 68 yenye thamani ya Tsh. Bilioni 18.3 ilikuwa imekamilika lakini haitumiki. Miradi hii ilitekelezwa kwenye Mamlaka ya Serikali za Mitaa 40

Ilihusisha Miradi ya Ujenzi wa Masoko, Ujenzi wa Hospitali za Wilaya, Vituo vya Afya na Zahanati, Ujenzi wa Miundombinu ya Shule (nyumba za Walimu, Vyoo na Madarasa) na ujenzi wa maeneo ya machinjio

Soma - https://jamii.app/MapungufuMiradi

#JFUwajibikaji
FAHAMU TATIZO LA KUTOKWA NA DAMU KWENYE FIZI (1)

Mara nyingi kuvimba au kutokwa Damu kwenye Fizi huweza kusababishwa na magonjwa mbalimbali ya Kinywa na Meno ambayo husababishwa na kutofanya usafi wa Kinywa kwa usahihi au maambukizi ya Bakteria ambao husababisha utando mgumu kwenye Meno

Ugonjwa wa Fizi ni hatari kwa kuwa hautambuliki mapema

Soma - https://jamii.app/FiziDamu

#Afya
Rais Samia asema bado Askari wanalalamikiwa kwa masuala kadhaa ikiwemo kushikilia Leseni za Madereva kwa muda mrefu au kuwalazimisha kulipa faini papo hapo

Pia, amesema kuna ukamataji mwingi wa Vyombo, na Pikipiki nyingi zimepangwa Vituo vya Polisi

Soma https://jamii.app/KeroAskari
RAIS SAMIA: VIJANA WAHANGA WAKUBWA WA AJALI ZA BARABARANI

Amesema takwimu zinaonesha zaidi ya 90% ya Ajali za Barabarani husababishwa na makosa ya kibinadamu ikiwemo mwendokasi, kutovaa mikanda na kupita gari lingine bila tahadhari

Soma - https://jamii.app/VijanaAjali

#JFLeo
TANESCO: TAASISI ZA SERIKALI NI CHANGAMOTO KWA KUTOLIPA BILI ZA UMEME

Changamoto nyingine ni Watu kutumia vyanzo vingine vya Nishati kwa kuwa TANESCO haina uthabiti wa huduma

Pia, Uharibifu wa miundombinu, gharama na ushindani wa matumizi ya Maji

Soma - https://jamii.app/ChangamotoTANESCO