JamiiForums
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
TANZANIA KUANZA KUTUMIA 5G

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dr. Jabir Kuwe amesema Tanzania inaelekea kuanza kutumia huduma ya 5G

> Majaribio ya #5G yatafanyika kuhakikisha kasi ya Teknolojia inayotakiwa inapatikana ili kuongeza Huduma ya Mawasiliano ya #Data nchini

Soma https://jamii.app/Tz5G

#DigitalRights
SHERIA YA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI KUTUNGWA

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari amesema Wizara yake iko mbioni kupeleka Bungeni muswada wa Sheria ya Kulinda Taarifa Binafsi iili kulinda FARAGHA na TAARIFA za mwananchi

- Wizara inaandaa sheria hiyo ili kulinda FARAGHA na TAARIFA binafsi za wananchi katika hatua ya Ukusanyaji, Usafirishaji, Matumizi na Utunzaji wa taarifa hizo kwa kuwa Taasisi mbalimbali zinatumia taarifa husika

Soma > https://jamii.app/Tz5G
INDIA: MAAMBUKIZI YA #COVID19 YAFIKIA MILIONI 25

Visa vipya 263,533 vimerekodiwa saa 24 zilizopita na kupelekea idadi kuwa Milioni 25.23

Idadi ya maambukizi imekuwa ikipungua ktk Taifa hilo ambalo Hospitali zimekuwa zikilazimika kukataa wagonjwa

Soma > https://jamii.app/India25Mil
WAPALESTINA 200 WAMEUAWA KATIKA MGOGORO NA ISRAEL

> Vilevile, Waisrael 10 wameuawa na katika mgogoro huo ulioanza Mei 10, 2021

> Katika Shambulizi la Mei 17, 2021 Kamanda Mwandamizi wa Palestina, Hussam Abu Harbeed aliuawa

Soma https://jamii.app/PalestineIsrael
ETHIOPIA: #TIGRAY YAKUMBWA NA HOFU YA MAGONJWA KWA KUKOSA HUDUMA ZA AFYA

Kutokana na uharibifu wa Vituo vingi vya Afya, kuna wasiwasi wa kuibuka kwa milipuko

Shirika la Afya lasema takriban watu Milioni 5 wanahitaji msaada hususan wa Chakula

Soma https://jamii.app/WHOTigray
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Mei 18, 2021 amezindua Kiwanda cha Ushonaji cha Jeshi la Polisi, Bohari Kuu Kurasini

Pia amekagua gwaride maalum lililoandaliwa kwa heshima yake

Soma > https://jamii.app/RaisSamiaDar
RAIS SAMIA AWATAKA POLISI WASITUMIE MAKOSA KAMA KITEGA UCHUMI

> Amewataka Polisi wasijikite kwenye kutoza faini badala yake wajikite ktk kudhibiti makosa

> Amesema hayo baada ya Polisi kusema wamepungukiwa mapato kutokana na kupungua kwa makosa

Soma https://jamii.app/RaisSamiaDar
RAIS SAMIA: UDHIBITI WA VITENDO VYA UJAMBAZI UTATUMIKA KUTENGUA NA KUTEUA MAKAMANDA WA POLISI

Katika hotuba yake, amesema miongoni mwa vigezo vitakavyotumika kuteua au kutengua Makamanda wa Mikoa ni udhibiti wa ujambazi ikiwemo wa kutumia silaha

Soma > https://jamii.app/RaisSamiaDar
UTAPELI MITANDAONI: RAIS SAMIA AHOJI USAJILI KWA KUTUMIA ALAMA ZA VIDOLE

- Rais asema vitendo vya wizi mitandaoni bado vinaendelea licha ya usajili huo

- Ametaka Polisi kushirikiana na TCRA na Taasisi za Fedha za Umma na Binafsi kumaliza kero hii

Soma > https://jamii.app/RaisSamiaDar
RAIS SAMIA ATAKA SHERIA YA PF3 KUANGALIWA

Amesema wanaopata ajali wanaumia kwa viwango tofauti na wengine huhitaji kushughulikiwa haraka

Asema, "Hii #Sheria muiangalie, Mtu anapofikishwa Hospitali apate huduma mambo mengine ya Kipolisi yaendelee"

Soma https://jamii.app/RaisSamiaDar
Papai ni miongoni mwa matunda yenye Vitamin K ambayo ni muhimu katika Afya ya Mifupa

- Ulaji wa Papai husaidia katika kuimarisha Afya ya Mifupa na kudhibiti kupasuka kwa Mifupa

- Pia Papai lina Madini ya Calcium, Potassium, Magnesium na Copper

#JamiiForums #LisheChakula
UTOFAUTI WA UFAULU KWA SHULE ZA BARA NA VISIWANI WAUNDIWA KAMATI

Sekondari za #Tanzania Bara na Zanzibar zimelalamikiwa kuwa na utofauti ktk ufaulu wa Wanafunzi

Waziri Jafo ateua Wajumbe 7 watakaoshauri kuhusu uboreshaji wa Elimu na Ufaulu

Soma - https://jamii.app/ElimuMuungano
MBUNGE: BAJETI YA WIZARA YA UJENZI HAINA MATUMAINI KWA WATANZANIA

Edwin Swale amesema Bajeti hiyo imeanza vibaya, Wabunge wanailalamikia na Waziri amekata tamaa

Ahoji sababu za Bajeti ya Barabara Jimboni kwake kupunguzwa kutoka Bilioni 5 mpaka 2

Soma > https://jamii.app/BajetiUjenzi
RAIS SAMIA AWATAKA POLISI KUHARAKISHA UCHUNGUZI WA KESI

> Ili kupunguza mrundikano Magerezani, Rais amewaagiza Polisi kufuta kesi za kubambikiza na kuharakisha Uchunguzi wa kesi

> Asema TAKUKURU wameshafuta kesi 147 zilizobambikizwa kwa Watu

Soma https://jamii.app/RaisSamiaDar
Papai ni chanzo kikuu cha virutubisho muhimu vinavyotoa kinga dhidi ya Magonjwa mbalimbali

Vitamin C na Vitamin A ambayo inapatikana mwilini kutokana na kirutubisho aina ya beta-carotene kilichomo ktk Papai ni muhimu kwa kuimarisha Kinga ya mwili

Soma https://jamii.app/FaidaPapai

#JamiiForums #LisheChakula
KAGERA: WANAWAKE WALALAMIKIWA KUKAA KINYUMBA NA WANAFUNZI WA SHULE ZA SEKONDARI

Baadhi ya Wanawake wa Kata ya Kashai wamelaumiwa kuwa na mahusiano ya kinyumba na Wanafunzi wa kiume wa Shule za Sekondari Ihungo na Kahororo hali inayosababisha utoro

Soma https://jamii.app/WanawakeBukoba
JAKAYA KIKWETE: KUNA HATARI YA JANGA LA AJIRA KUTOKANA NA ELIMU HAFIFU

Asema kutokana na hilo, kuna hatari ya nusu ya Ajira zilizopo kutoweka ifikapo 2050

Amesema Elimu inayotolewa Afrika ilitolewa miaka 50 hadi 70 iliyopita kwa Nchi zilizoendelea

Soma https://jamii.app/JKElimuAjira
WANAOHONGA ILI KUUNGANISHIWA UMEME, KUCHUKULIWA HATUA

Waziri wa Nishati, Dkt. Kalemani ametaka wanaotoa Tsh. 200,000 kwa Makandarasi badala ya Tsh. 27,000 wachukuliwe hatua kwani husababisha upendeleo

> Pia, Makandarasi wanaopokea watawajibishwa

Soma https://jamii.app/MakandarasiUmeme
NI KWELI BILA 'TENDO LA NDOA' HAKUNA NDOA?

Mdau wetu anadai hata wakati wa matatizo, jambo la kufanya ni kutafuta suluhisho na si Mwanandoa kumnyima unyumba mwenzie

> Wengine wanatofautiana naye wakidai NDOA ni zaidi ya TENDO hilo...

Nini maoni yako kuhusu hili?

Fuatilia mjadala huu https://jamii.app/MdauJFNdoa
TANESCO YAKIRI KUHUSU KUKOSEKANA KWA HUDUMA YA KUNUNUA UMEME

TANESCO imekiri kuwa na hitilafu tangu Mei 17, 2021 na kusababisha baadhi ya wateja kushindwa kununua umeme

> TANESCO imeomba wateja wawe wavumilivu muda huu ambao tatizo linatatuliwa

Soma https://jamii.app/TANESCOLUKU