JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MATUMIZI MABAYA YA FEDHA NI ADUI WA MAFANIKIO

Kutokuwa na mpangilio wa matumizi ya Pesa ni changamoto inayowakumba wengi ambapo Mtu hutamani kununua kila anachokiona mbele yake

Kukopa pesa ovyo hupelekea madeni yanayowaelemea Watu. Baadhi ya Watu wanakopa bila kuangalia faida au hasara za Mkopo na kujikuta wakilipa Madeni kwa miaka mingi

Soma - https://jamii.app/MatumiziFedha
#Uchumi
NJOMBE: DC AAGIZA KITUO CHA AFYA KUACHA KUWATOZA FEDHA WATOTO CHINI YA MIAKA MITANO

Kituo cha Afya Makambako huwatoza Watoto Tsh. 4000 ili kumuona Daktari ambapo ni kinyume na Sera ya Afya ya 2007

> Mkuu wa Wilaya ameagiza kusitishwa kwa tabia hiyo

Soma https://jamii.app/WatotoKulipa
ZIMBABWE: MKE WA MUGABE AITWA MAHAKAMANI KWA KUMZIKA MUMEWE KINYUME NA MILA

Waraka wa Chifu Zvimba umemtaka Grace Mugabe kuufukua mwili ili uzikwe tena kulingana na utamaduni wa Watu wa Zvimba

Pia, alipe faini ya Ng’ombe na Mbuzi kwa kukiuka Mila

Soma - https://jamii.app/GraceMugabeCourt
ISRAEL vs PALESTINA: Mpaka sasa Vifo vya Wapalestina vimefikia 83 huku Watu 480 wakijeruhiwa kutokana na Mapigano yanayoendelea

- Mapigano hayo kati ya Israel na kundi la Wanamgambo wa #Hamas yamesababisha uharibifu mkubwa huko Gaza

#GazaUnderAttack #IsraelPalestineConflict
FAINALI YA UEFA KATI YA MAN. CITY NA CHELSEA KUCHEZWA URENO

Mchezo wa Fainali ya kuwania Kombe la Klabu Bingwa Ulaya kati ya #ManchesterCity na #Chelsea umehamishiwa Ureno kutokana na UEFA na Serikali ya Uingereza kutofikia muafaka wa mchezo huo kuchezwa Wembley

UEFA ililazimika kutafuta uwanja mbadala kutokana na mlipuko wa Ugonjwa wa #COVID19 katika nchi ya Uturuki uliosababisha Uingereza kuiweka nchi hiyo katika nchi hatari za kutembelea

#JamiiForums #UCL #JFSports
MAMBO YA KUZINGATIA IKIWA UNAFIKIRIA KUANZA KUJENGA NYUMBA YAKO

1. Fedha: Kabla ya kuanza ujenzi hakikisha una chanzo kizuri cha mapato ambacho kitakurahisishia shughuli ya ujenzi. Pia, ni vyema kuwa makini na matumizi ya fedha katika kila hatua ya ujenzi

2. Mchoro/Ramani: Ikiwa tayari una Kiwanja basi jitahidi kutafuta Msanifu Majengo (Architect) atakayekupa ushauri wa kitaalamu kulingana na kile unachokitaka

Soma - https://jamii.app/NyumbaUjenzi
#Ujenzi
MDAU: JITAHIDI USIWE SABABU YA NDOA YA RAFIKI YAKO KUVUNJIKA

> Anafafanua, kuvunjika kwa ndoa huweza kuwa na madhara makubwa kwa watoto na wewe kama rafiki usiwe sababu ya hilo

> Anasema rafiki unapaswa kuwa mshauri mzuri ili ndoa iweze kudumu

Soma https://jamii.app/UrafikiNdoa
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amemsimamisha kazi Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali zinazomkabili kuanzia leo, Mei 13, 2021

- Aidha, Rais Samia amefanya teuzi za Viongozi mbalimbali ambao uteuzi wao unaanza leo

#JFLeo
TUNAWATAKIA SIKUKUU NJEMA YA EID-AL-FITR

> Bodi, Menejimenti na Wafanyakazi wote wa JamiiForums wanawatakia Waislamu na watu wote kwa ujumla Sikukuu njema ya #EidAlFitr

> Asante kwa kuendelea kuwa pamoja nasi; tunawatakia mapumziko mema!

#EidMubarak #Eid #EidUlFitr
CDC-USA: WALIOMALIZA KUPATA CHANJO WANAWEZA KUTOVAA BARAKOA

Kwa waliomaliza kupatiwa chanjo ya #COVID19 wanaweza kuendelea na shughuli walizosimamisha kwa sababu ya Corona

> Hawatakuwa na haja ya kuvaa barakoa wala kuweka umbali kati ya mtu na mtu

Soma https://jamii.app/BarakoaCDC
KENYA: MAHAKAMA YA JUU YAZUIA MAPENDEKEZO YA KUBADILISHA KATIBA

Mahakama imesema mpango wa BBI ni hatua binafsi ya Rais Kenyatta ambaye hana Mamlaka ya Kisheria kuanzisha mchakato wa mabadiliko yoyote ya #Katiba

Mpango huo unapendekeza mgawanyo wa Madaraka baina ya Makabila hasimu ili kuzuia ghasia zinazotokea kila baada ya Uchaguzi

Soma - https://jamii.app/CourtBBIKE
TAFITI: #COVID19 INAWEZA KUPELEKEA UHANITHI

Watafiti wameandika ktk Jarida la Afya ya Wanaume kuwa Corona huathiri mishipa ya Damu hivyo huweza kupelekea uhanithi

> Wameona haja ya Wanaume kuangaliwa zaidi katika Chanjo ili kuepuka tatizo hilo

Soma https://jamii.app/UhanithCorona
MAREKANI: KAMPUNI YA MAFUTA YADAIWA KULIPA DOLA MILIONI 5 KWA WADUKUZI

Usafirishaji wa Mafuta ktk Bomba la Colonial Pipeline, linalobeba zaidi ya galoni Milioni 100 ulisitishwa Mei 7 kwasababu ya shambulio la Kimtandao ila shughuli zilirejea Mei 13

Soma https://jamii.app/ColonialPipelineBack
CHINA YAFANIKIWA KUPELEKA KIFAA KATIKA SAYARI YA 'MARS'

China imekuwa nchi ya pili ktk historia kufanikiwa kufikisha kifaa ktk Sayari Nyekundu au 'Mars' kwa Kiswahili inaitwa 'Mirihi'

Kifaa hicho kimetua, Mei 15, 2021 Asubuhi kitatafiti uwepo wa maisha kwa miezi 3

Soma https://jamii.app/MarsChina
KINONDONI: WALIMU 1,333 KUPANDISHWA VYEO

> Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) Wilaya ya Kinondoni ipo hatua za mwisho za kukamilisha zoezi la kupandisha vyeo/madaraja Walimu wa Shule za Msingi na Sekondari wa Manispaa ya Kinondoni wenye sifa

Soma https://jamii.app/WalimuVyeo
MAAMBUKIZI YA #COVID19 YARIPOTIWA KUPUNGUA INDIA

Mji wa #Delhi umeshuhudia visa 8,506 vya maambukizi ndani ya saa 24 zilizopita

Katika Mji wa kibiashara wa #Mumbai, maambukizi yameshuka kufikia visa pungufu ya 2,000 kutoka 11,000 kwa siku

Soma - https://jamii.app/FallCoronaIndia
ABOUBAKARI KUNENGE ATEULIWA RC PWANI

Rais Samia Suluhu amemteua Aboubakari Kunenge kuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani

Kabla ya uteuzi Kunenge alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na anachukua nafasi ya Mhandisi Evarist Ndikilo ambaye amestaafu

#JFLeo