JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
NDEGE ZA #SOMALIA ZAPIGWA MARUFUKU KUINGIA ANGA LA KENYA

Mamlaka ya Anga imesema ndege za dharura za kitabibu na walio na ujumbe wa masuala ya kibinadamu ya UN zitaruhusiwa kuingia

> #Kenya na Somalia zimekuwa na mzozo wa Mpaka tangu 2014

Soma https://jamii.app/NdegeSomaliaKenya
#JFLeo
WHO: MTU 1 KATI YA 500 ANAWEZA KUPATA CHANJO KWA NCHI ZINAZOENDELEA

Shirika la Afya Duniani limesema hali ilivyo kwa Nchi zinazoendelea ni tofauti ikilinganishwa na Nchi zilizoendelea, ambapo mtu 1 kati ya 4 amepata Chanjo ya Ugonjwa wa #COVID19

Soma > https://jamii.app/ChanjoUpatikanaji
SIMIYU: MUME AUA MKEWE KISHA NAYE KUJINYONGA KUTOKANA NA WIVU WA MAPENZI

Edward Manyangu(41) Mkazi wa Busega anadaiwa kumuua Dalali Maunga(41) kwa kumpiga na kitu kizito kichwani akimtuhumu kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Mwanaume mwingine

Soma - https://jamii.app/VifoNdoaBusega
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
WALIMU KUWA NA ARI KAMA MWALIMU YUSUPH KUNAWEZA KUONGEZA UELEWA WA WANAFUNZI?

Mwalimu Yusuph Mohamed Yusuph ni Mwalimu wa Shule ya Msingi Ikorongo Mkoani Mara anayeonekana akifundisha kwa kutumia mbinu nyingi za kuwaburudisha Watoto

Je, ari na ubunifu alionao unaweza kuongeza thamani katika Uelewa wa Wanafunzi wanaofundishwa?

#JamiiForums #Elimu
EPL: MANCHESTER CITY YACHUKUA UBINGWA
-
Ushindi wa bao 2-1 wa #LeicesterCity dhidi ya #ManchesterUnited umeipa nafasi #ManchesterCity kuchukua ubingwa wa ligi hiyo ikiwa na Michezo mitatu mkononi

#JFSports #JFLeo
HOSPITALI YA MUHIMBILI KUANZA KUPANDIKIZA MIMBA

Kwa mwaka 2021/22 Muhimbili itapandikiza Uboho (Bone Marrow) kwa wenye Kansa ya Damu, kutoa huduma za upandikizaji Mimba (IVF) na ujenzi wa jengo la Wagonjwa Binafsi lenye vitanda 200

Soma - https://jamii.app/IVFMuhimbili
Leo tarehe 12 Mei ni Siku ya Kimataifa ya Wauguzi

> Tunatambua kuwa Upatikanaji wa Huduma Bora za #Afya unawategemea sana Wauguzi

> Wauguzi: Hutoa huduma ya Afya kwa Wajawazito, Mama na Mtoto na Hutoa Chanjo mbalimbali

> Pia, huwahudumia waathirika wa magonjwa mbalimbali yakiwemo Kansa, Corona, UKIMWI, ajali na mengine mengi yanayoambukiza na yasiyoambukiza

> Kwa ujumla, Wauguzi ni watu wa Msaada sana kwetu
URUSI KULETA SHERIA YA KUMZUIA NAVALNY NA WAFUASI WAKE KUWA WABUNGE

Muswada utawasilishwa Mei 18, 2021 na endapo ukipitishwa, #Sheria itawazuia Wanachama wa "Siasa kali" kuwa Wabunge (Alexei Navalny na Wananchi wanaokiunga mkono Chama chake)

Soma https://jamii.app/RussiaPoliticsLaw
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
RAIS SAMIA AWASILI UGANDA KUHUDHURIA UAPISHO WA MUSEVENI

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu, amewasili #Uganda kuhudhuria sherehe za kuapishwa Rais Yoweri Museveni

> Museveni alitangazwa mshindi wa Uchaguzi kwa kupata 58.64% ya Kura

Soma https://jamii.app/SamiaUganda

#M7SwearsIn2021
AFRIKA KUSINI YAPENDEKEZA MWANAMKE KUWA NA MUME ZAIDI YA MMOJA

Idara ya Mambo ya Ndani imependekeza Sheria ya kuwaruhusu Wanawake kuolewa na Mwanaume zaidi ya mmoja (#Polyandry)

Pia, Ndoa za Wahindi, Wayahudi, Waislamu na Rastafarian zitambuliwe

Soma - https://jamii.app/PolyandrySA
GAZA: WAPALESTINA 36 WAUAWA BAADA YA KUSHAMBULIWA NA ISRAEL

Mbali na vifo, watu wengine 250 wamejeruhiwa kufuatia mashambulizi ya maroketi ambayo yameanguka katika bomba la mafuta na kusababisha moto mkubwa

> Kundi la Hamas limeapa kulipa kisasi

Soma https://jamii.app/GazaMashambulizi
YOWERI MUSEVENI AAPISHWA KUWA RAIS WA UGANDA KWA MIAKA MINGINE MITANO

Rais Yoweri Museveni ameapishwa kwa mara ya sita mfululizo kuliongoza Taifa hilo hadi mwaka 2026

Museveni amekuwa Kiongozi wa #Uganda tangu mwaka 1986

Soma - https://jamii.app/MuseveniSworn
TANGA: WATENDAJI WATATU KUFUKUZWA KAZI KWA UBADHIRIFU

Baraza la Madiwani Handeni limewafukuza kazi Watendaji wa Kata kwa matumizi mabaya ya Fedha za Serikali

> Mahakama iliwakuta na hatia Watendaji wawili, Juma Kikoti na Juma Kidungwe

Soma https://jamii.app/WatendajiWaKijiji
NJIA ZA KUJIJENGEA UAMINIFU KWENYE BIASHARA YAKO

Jenga uhusiano mzuri na Wateja: Toa huduma bora, wajali Wateja wanapopata changamoto na kuwa tayari kutatua changamoto zao

Tekeleza unachoahidi: Hakuna kitu kinapoteza Imani ya Wateja kama kuahidi akija kwako atapata kitu fulani halafu asikipate

Soma zaidi - https://jamii.app/UaminifuBiashara
#Biashara
DAR: POLISI WAUA WATATU WANAOSHUKIWA KUWA MAJAMBAZI

Tukio limetokea Mbagala ambapo Polisi imesema watu hao walikuwa kwenye pikipiki ikidhaniwa walijiandaa kufanya ujambazi

Walikaidi amri walipoambiwa wasimame na kuanza kuwarushia Polisi risasi

Soma https://jamii.app/Majambazi3DSM
CHINA YAIPA TANZANIA MSAADA WA TSH. BILIONI 35.37

Tanzania imepokea Tsh. Bilioni 35.37 zitakazotumika kwa miradi ya Maendeleo itakayokubaliwa na China na Tanzania

> Baadhi ya miradi ni kuboresha Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kuwa Chuo Kikuu

Soma https://jamii.app/ChinaTzMsaada