JamiiForums
βœ”
52.6K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
TABIA NJEMA INAJENGWA NA MALEZI, DINI AU NI HULKA ASILIA YA MTU?

- Mdau wa JamiiForums anasema kuna Watoto ambao wamelelewa na Watu wenye Maadili mema na misingi ya Dini lakini wao wana Tabia mbaya

- Wengine hawakupata Malezi mazuri wala misingi ya Dini lakini wana tabia njema. Je, tabia njema inajengwa na Malezi, Dini au ni Hulka asilia ya Mtu?

Mjadala - https://jamii.app/TabiaDiniMalezi
#Maisha
KOROGWE-TANGA: MADIWANI WAJISAIDIA VICHAKANI

Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe unaotumiwa na Madiwani umeripotiwa kuwa na uhaba wa matundu ya vyoo

> DC Kissa Kasongwa amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo lakini amesema ipo nje ya uwezo wake

Soma https://jamii.app/MadiwaniKorogwe
MICHEZO: Mchezo wa kati ya Simba na Coastal Union uliopangwa kuchezwa Mei 11 umeahirishwa na utapangiwa tarehe nyingine

- Simba wanasafiri siku hiyo kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya robo fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika(CAFCL) dhidi ya Kaizer Chiefs Mei 14

#Sports
EDINSON CAVANI AONGEZA MKATABA HADI JUNI 2022 MAN U

> Bodi ya Manchester Utd pamoja na Kocha Ole Gunnar Solskjær walikuwa wakimshawishi #Cavani kuongeza mkataba

> Klabu hiyo ya Jijini #Manchester inajipanga kutangaza makubaliano hayo

#MUFC #ManUTD
KIBAHA: WAWILI WALIOTOKA JELA KWA MSAMAHA WAUAWA KWA TUHUMA ZA WIZI

Ramadhani Mohamed (28) na Iddi Hamisi Chuga (30) wameuawa kwa kupigwa na raia alfajiri ya Mei 8

> Walifungwa kwa makosa ya wizi na walipata msamaha wa Rais Aprili 12, 2021

Soma https://jamii.app/KibahaWaliosamehewa
UJERUMANI YAIPA TANZANIA TSH. BILIONI 56 KUSAIDIA UHIFADHI NCHI

Waziri wa Maliasili na #Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro amesema miradi inayofadhiliwa ina umuhimu mkubwa katika Uhifadhi

> Mradi utadumu kwa miaka 3, utaanza baada ya bajeti kupitishwa

Soma https://jamii.app/UhifadhiNchi
UNAPOTEZEAJE KUMPA SHIKAMOO MTU AMBAYE HUNA UHAKIKA KAMA AMEKUZIDI UMRI?

Kuna baadhi ya Watu wana mwonekano ambao ni vigumu kujua kama umri wake ni mdogo au mkubwa, hivyo kukufanya uwe njia panda kumpa Shikamoo au la

Je, ukikutana na Watu wa aina hii unatoa salamu ya aina gani?

Mjadala zaidi - https://jamii.app/SalamuUmri
#Maisha
SUA-APOPO: PANYA WANAWEZA KUTAMBUA MAAMBUKIZI YA COVID19

Watafiti wa SUA-APOPO wamesema walifanikiwa kuwafunza panya wabaini Kifua Kikuu hivyo wataweza kubaini Corona

> Wamesema kila kimelea kina harufu tofauti, ni rahisi kwa panya kuzitofautisha

Soma https://jamii.app/PanyaCOVID19
WATANZANIA MILIONI 22 WANA MINYOO NA KICHOCHO. KANDA YA ZIWA YAONGOZA

Ukubwa wa tatizo kwa Kanda ya Ziwa unasababishwa na Jiografia yake ya kuwa na Maji mengi

Watu Bilioni 2 Duniani wameathiriwa na Minyoo huku 155,000 wakifariki kila mwaka

Soma - https://jamii.app/MinyooKichochoTZ
UN: KUNAHITAJIKA UWEKEZAJI KWENYE MASUALA YA AFYA YA AKILI

Katibu Mkuu wa UN, AntΓ³nio Guterres amesema afya ya akili halijatiliwa maanani kwa muda mrefu

> Ametoa wito kuwekeza eneo hilo ili kupunguza unyanyapaa kwa wanaohitaji msaada wa kitabibu

Soma https://jamii.app/MentalHealthMonth
Pamoja na hayo, Matango yana vitamini K ambayo huisaidia kuimarisha mifupa

#JamiiForums #JamiiTalks
WADAU: SHULE ZA β€˜ENGLISH MEDIUM’ ZIMEFANYA WAZAZI KUWA WALIMU

> Wazazi ndani ya JamiiForums wanajadili kuhusu 'Homeworks' wanazopewa watoto toka shuleni. Baadhi wanaona ni vyema mzazi kushiriki kazi za mtoto ili kujua maendeleo yake huku wengine wakiona kama wanapewa kazi ya kufundisha watoto ilhali wamelipa ada

> Je, una maoni gani kuhusu hili?

Soma https://jamii.app/ShuleEnglishMedium