JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
SERIKALI: TANZANIA HAINA WAFUNGWA WA KISIASA

Serikali imesema hayo leo Mei 07, 2021 baada ya Chombo cha Habari kutoka Nchi jirani kuripoti Rais Samia Suluhu Hassan ametoa agizo la kuachiwa Wafungwa 23 wa Kisiasa Nchini

Soma > https://jamii.app/TZWafungwaSiasa
Baadhi ya aliyosema Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Dar mbele ya Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Mei 07, 2021 Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam
Hotuba ya Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano na Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam leo Mei 07, 2021

#JamiiForums
HUENDA FAINALI YA KLABU BINGWA ULAYA IKACHEZWA ENGLAND

- Ni baada ya England kuiongeza Uturuki ktk orodha ya nchi hatari kwenda kutokana na #COVID19

- FA inaongea na UEFA kuruhusu fainali hiyo kati ya Chelsea na Man. City itakayochezwa Mei 29, ichezewe England

#UCL #JFSports
SHINYANGA: MBARONI KWA KUMUUA MKEWE AKIDAI ANATUMIA ARV KWA SIRI

Peter Elias alimpiga Pili Luhende baada ya kubaini anatumia Dawa za Kufubaza Virusi vya UKIMWI kwa kuficha

Alipobaini amefariki alitupa mwili maeneo ya Daraja la Mwagala

Soma > https://jamii.app/MauajiShy
#COVID19: CHANJO YA CHINA YAIDHINISHWA NA SHIRIKA LA AFYA

WHO imetoa idhini ya dharura kwa Chanjo iliyotengenezwa na Kampuni ya China ya #Sinopharm

Japokuwa tayari imetolewa kwa Mamilioni ya watu, idhini ya WHO ni mwongozo kuwa ni Chanjo salama

Soma > https://jamii.app/SinopharmWHO
AYATOLLAH: ISRAEL NI NGOME YA MAGAIDI

Kiongozi wa #Iran, Ayatollah Ali Khamenei, anailaumu #Israel kuhusika katika mashambulizi mfululizo ya Majini kwenye kinu chake na kumuua Mwanasayansi mwandamizi wa Iran

Soma - https://jamii.app/IranVsIsrael
SHINYANGA: BABA AKAMATWA KWA KUOZESHA MWANAFUNZI

Masele Kuyela (52) na Kaka wa Bwana Harusi wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumwozesha Binti ambaye ni Mwanafunzi wa Kidato cha Pili kwa Mahari ya Ng’ombe sita na Shilingi Laki Mbili

Soma - https://jamii.app/MbaroniMahariMwnfz
RASMI: NEYMAR ASAINI MKATABA MPYA NA KLABU YA PSG

- Neymar amesaini mkataba huo utakaomfanya adumu #PSG hadi Juni 2026.

- Mshahara wake unakadiriwa kuwa Bilioni 83.9 za Kitanzania kwa msimu baada ya makato ya kodi.

#JFSports #JamiiForums
MCHEZO WA SIMBA NA YANGA KUCHEZWA SAA 1 JIONI BADALA YA SAA 11 LEO

> Taarifa ya TFF imesema mabadiliko hayo ni kutokana na maelezo ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

> Tayari Yanga SC na Simba SC zimejuzwa juu ya mabadiliko hayo

#JFSports #JamiiForums