JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
SERIKALI YASITISHA MATUMIZI YA KANUNI MPYA ZA BASATA KUKAGUA NYIMBO

Waziri Innocent Bashungwa amesitisha utekelezaji wa Kanuni mpya kutoka Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) zinazohusu kukagua nyimbo za Wasanii kabla hazijaenda kwa Wananchi

Soma - https://jamii.app/BanKanuniBasata
YANGA: MABADILIKO YA MUDA WA MECHI DHIDI YA SIMBA YANAKINZANA NA KANUNI

- Yanga imesikitishwa na mabadiliko ya muda wa mechi baina yao na wapinzani wa jadi, Simba na kudai mabadiliko hayo ni kinyume na Kanuni

- Waamua kupeleka timu Uwanjani saa 11
EPL: CHELSEA YAIFUNGA MAN. CITY, YAPANDA NAFASI YA 3

Klabu ya Chelsea imeibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Man City iliyokuwa nyumbani uwanja wa Etihad kwenye mchezo wa Ligi Kuu England

> Timu hizo sasa zitakutana Mei 29, 2021 katika Fainali ya Klabu Bingwa barani Ulaya (UEFA Champions League)

#JFSports #MCICHE #chelsea #mancity
#MYANMAR: JESHI LASEMA KUNDI LINALOPINGA UTAWALA WAKE NI MAGAIDI

Jeshi limesema kundi la Serikali ya Umoja wa Kitaifa ni la kigaidi na kulishutumu kwa mashambulizi ya mabomu na mauaji

Maandamano na migomo ya kupinga Utawala wa kijeshi inaendelea

Soma > https://jamii.app/MyanmarCrisis
GHASIA MJINI #JERUSALEM: WATU 200 WAJERUHIWA

Kuna urushaji Maputo ya Moto kutoka #Gaza kuelekea Israel na kushambuliwa kwa Mashamba ya Wapalestina

Polisi wa #Israel wanafyatua Maji ya kuwasha na Risasi za mipira kuwatawanya Wapalestina

Soma - https://jamii.app/JerusalemCrisis
SERIKALI YATANGAZA AJIRA MPYA 9,675

TAMISEMI imetangaza ajira za Watumishi wa Afya 2,726 kwa ajili ya Hospitali za H/shauri, Vituo vya Afya na Zahanati pia Walimu 6,949 wa S/Msingi na Sekondari watakaofanya kazi chini ya Mamlaka za Serikali za Mitaa

Soma https://jamii.app/AjiraMpya
RAIS SAMIA AMKABIDHI NYUMBA YA KUISHI RAIS MSTAAFU KIKWETE

- Amemkabidhi nyumba hiyo iliyojengwa Wilayani Kinondoni, Dar

- Pia, Rais Samia amemuagiza Waziri wa Utumishi, kuanza maandalizi ya kutimiza haki zote anazostahili Hayati Rais Magufuli

Soma https://jamii.app/SamiaNyumbaKikwete
UMESUBSCRIBE NA CHANNEL YETU YA TELEGRAM?

Habari yako! Tunakusihi kutumia Telegram ili uweze kusubscribe kwenye channel yetu na kupata taarifa. Ingia Telegram andika 'JamiiForums'

> Tukutakie kila la kheri katika majukumu yako ya wiki hii. Tunashukuru kwa kuwa nasi
KAMANDA MUROTO: WANAOPANGA KUANDAMANA WATAKIPATA WANACHOKITAFUTA

Kamanda wa Polisi Mkoani Dodoma amewaonya Wafuasi wa CHADEMA waliopanga kuandamana kutokea Geita ili kumshinikiza Spika Job Ndugai kuwafukuza Wabunge 19 wa Viti Maalum

Soma - https://jamii.app/MurotoOnyoBawacha
#JFLeo #Siasa
#COVID19: VIRUSI VYA INDIA NA UINGEREZA VYAGUNDULIKA AFRIKA KUSINI

Virusi vya Corona vinavyojulikana kama B.1.617.2 na B.1.1.7 vimethibitika Majimbo ya Guateng na KwaZulu-Natal

Waliokutwa na maambukizi ni wenye historia ya kusafiri ktk nchi hizo

Soma > https://jamii.app/VirusiSA
SOMALIA: POLISI WATANO WAUAWA KATIKA SHAMBULIO LA KUJITOA MHANGA

> Pia, raia zaidi ya sita wameuawa ktk shambulio hilo lililofanyika Mei 9, 2021, saa tatu na nusu usiku, Mjini Mogadishu

> Kati ya Polisi watano waliouawa wawili ni Makamanda

Soma https://jamii.app/SomaliaBomu
#Ugaidi
UMOJA WA ULAYA HAUJAONGEZA MKATABA WA KUPATA CHANJO YA ASTRAZENECA

Mkataba wa Umoja wa Ulaya (EU) na #AstraZeneca utaisha mwezi Juni

> Mei 8, Kamisheni ya EU iliingia makubaliano ya hadi 2023 na BioNTech/Pfizer ya ununuzi wa dozi za nyongeza

Soma https://jamii.app/AstrazenecaVsEU
WAZIRI MKUU: WIZARA ITOE TAARIFA HARAKA KUHUSU MCHEZO WA SIMBA NA YANGA

Kassim Majaliwa ameagiza Wizara ya Michezo kutoa taarifa haraka kuhusu Mechi kati ya Simba SC na Yanga SC na hatma ya waliolipa viingilio vya Mchezo ulioahirishwa

Soma - https://jamii.app/MajaliwaSimbaYanga