JamiiForums
βœ”
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
VYAKULA VINAVYOIMARISHA UWEZO WA KUONA (MACHO)

- Karoti: Zina utajiri mkubwa wa Vitamini A na Beta Carotene ambazo huboresha uwezo wa kuona na kuyalinda Macho kutokana na Umri

- Samaki: Wana Mafuta ya Omega-3 ambayo ni muhimu kwa ajili ya kuzuia kunyauka kwa Macho, kudhoofu kwa misuli na hata Mtoto wa Jicho

- Karanga na jamii zake: Vina Asidi ya Mafuta ya Omega-3 pamoja na kiwango kikubwa cha Vitamini E

- Nyama ya Ng’ombe: Ina Madini ya Zinc ambayo huuwezesha Mwili kufyonza Vitamini A ambayo ni muhimu kwa Macho.

Soma - https://jamii.app/VyakulaMacho
#LisheChakula
MKURANGA: SERIKALI YAFUNGA KIWANDA CHA NONDO KUTOKANA NA VIFO VYA WAFANYAKAZI

- NEMC imekifunga Kiwanda cha Fujian Hexingwang kwa kukosa mazingira Salama ya kazi

- Wafanyakazi 2 wamefariki ktk mlipuko wa tanuru la kuyeyusha vyuma chakavu

Soma - https://jamii.app/NondoVifo2
Fainali ya #UCL itachezwa Mei 29 na itazikutanisha timu mbili za England - Chelsea na Man City

#uefachampionsleague
CANADA: PFIZER YAIDHINISHWA KWA WATOTO WENYE MIAKA 12-15

- Inakuwa Nchi ya kwanza kutoa idhini kwa walio na umri huo

- Mamlaka imesema Chanjo hiyo dhidi ya #COVID19 ni salama na inafanya kazi inapotumika kwa walio na umri mdogo

Soma > https://jamii.app/PfizerCanada
GWAJIMA: NCHI NI LAZIMA IWE NA MAONO YA MIAKA MINGI

- Mbunge wa Jimbo la Kawe, Askofu Josephat Gwajima, amesema kwasasa #Tanzania haina maono ya muda mrefu kwaajili ya Maendeleo ya Wananchi bali kuna Ilani za Vyama na mipango ya muda mfupi

Soma - https://jamii.app/GwajimaMaonoNchi
MBUNGE IGHONDO: MIKOPO YA ELIMU ITOLEWE NA KWENYE VYUO VYA UFUNDI

- Mbunge wa Singida Kaskazini ameiomba Serikali kuwawezesha Mwanafunzi wa Vyuo vya Ufundi kwasababu hawa wanakwenda kufanya kazi moja kwa moja badala ya kusubiri kuajiriwa

Soma - https://jamii.app/MikopoUfundi
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
RAIS SAMIA: NAKWENDA KUFUNGUA NCHI, MAENEO YA KUJENGA UCHUMI YAPO

- Akiwa Kenya amesema "Mmekuwa mkinitukana sana kwenye mitandao. Unakwenda kubomoa yaliyojengwa kwa muda mrefu"

- Asema anajiandaa kufanya mkutano na Sekta Binafsi ili kuzungumzia kero

Soma https://jamii.app/RaisWafanyabiashara
Hivi karibuni BASATA ilimtaka Mwanamuziki Nay wa Mitego kusitisha kupeleka kwenye Vyombo vya Habari na Mitandao wimbo wake wa 'Mama' kwa madai Maudhui yake yanakinzana na kanuni za BASATA

Jambo hili limezua hisia hasi miongoni mwa Wasanii pamoja na Jamii

#Sanaa #Arts #JamiiForums
MBUNGE: MATAMKO YA KISIASA YANAATHIRI ELIMU. MWENYE MADARAKA ANATAMKA BILA KUSIKILIZA WATAALAMU

- Tunza Malapo asema Mtaala ubadilishwe kwa utulivu kwa kusikiliza Wadau na Wataalamu

- Aongeza "Tuache mihemko, tuwatumie Wataalamu tuepuke Siasa”

Soma - https://jamii.app/TunzaTamkoElimu
LIGI YA EUROPA: MBIVU NA MBICHI ZA FAINALI KUJULIKANA LEO

- Michezo miwili ya nusu fainali ya Europa kurindima hii leo saa 4:00 usiku katika viwanja viwili tofauti, ambapo Roma itakuwa nyumbani kuialika Manchester United huku Arsenal ikiikaribisha Villarreal

- Ili Roma kutinga Fainali inatakiwa kushinda goli 4-0 huku Arsenal nayo katika mechi yake itahitaji ushindi wa goli 1-0 ili kutinga Fainali

#Europaleague #JFSports
RAIS SAMIA SULUHU KUKUTANA NA WAZEE WA DAR ES SALAAM MEI 7, 2021

Rais wa Tanzania anatarajiwa kufanya Mkutano na zaidi ya Wazee 900 wa Mkoa wa Dar es Salaam ktk Ukumbi wa Mlimani City kuanzia saa 8 Mchana

Soma - https://jamii.app/SamiaWazeeDar
DAR: AFISA TRA TEMEKE AKAMATWA KWA RUSHWA

Humphrey Mhagama amekamatwa kwa kuomba Tsh. 500,000 ambapo alipokea Tsh. 250,000

TAKUKURU imesema Mtuhumiwa atafunguliwa Mashtaka kwa kosa la kushawishi, kuomba na kupokea Rushwa

Soma > https://jamii.app/RushwaAfisaTRA
Hutumika kuongoza mahusiano kati ya Viongozi na Watumishi wa Umma, Bodi mbalimbali za Kitaaluma, Vyombo vya Habari, Wadau na Makundi mengine ya wananchi katika jamii

> Kwa ujumla huwataka Viongozi wa Umma kufanya kilicho sahihi ikiwa ni pamoja na kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, weledi, uwajibikaji na uwazi

#GoodGovernance
DAR: WATU 161 WAKAMATWA KWA WIZI WA MAGARI NA PIKIPIKI

Watano kati yao wamekamatiwa Zanzibar wakiwa na pikipiki 40

Vilevile, Polisi imekamata vitu mbalimbali vinavyodhaniwa kuwa vya wizi vikiwemo pikipiki 91, bajaji na vipuri vya magari

Soma > https://jamii.app/161WiziDar
HOJA: EPUKA KUFUATA MKUMBO IKIWA UNATAKA KUFANIKIWA

> Mdau anasema usishiriki kwenye mabishano yoyote ambayo hayana manufaa kwako. Usifanye jambo sababu wa Watu bali tumia akili zako kufanya kilicho sahihi.

> Kitu pekee kinachotutofautisha Binadamu na viumbe wengine ni uwezo wa kufikiri na kufanya maamuzi sahihi kulingana na hali tuliyonayo

Mjadala zaidi - https://jamii.app/MkumboMafanikio
#Maisha
UHAMISHO KWA WATUMISHI KUFANYIKA MARA 4 KWA MWAKA

- Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - TAMISEMI amewataka Makatibu Tawala kutokupitisha maombi ya wanaotaka kuhamia kwenye Majiji, Manispaa na Miji kwa kuwa maeneo hayo yana idadi kubwa ya Watumishi

Soma > https://jamii.app/UhamishoWatumishi
MTWARA: 11 WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA UHUJUMU UCHUMI

Wanadaiwa kughushi nyaraka za Serikali na kulipwa fedha za fidia isivyo halali, na kuisababishia Halmashauri ya Wilaya ya Masasi hasara ya zaidi ya Milioni 13.2

Soma > https://jamii.app/11UhujumuMtwara