JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
LIGI YA MABINGWA ULAYA: NANI KUTINGA FAINALI, MAN CITY AU PSG?

- Mchezo wa pili wa Nusu Fainali kati ya Manchester City dhidi ya PSG kuchezwa hii leo majira ya saa 4:00 usiku

- Mchezo wa kwanza katika hatua hiyo Manchester City iliibuka na ushindi wa goli 2-1

- Ili kutinga Fainali PSG inahitaji kushinda si chini ya magoli 2-0 wakati Man City ikihitaji sare au ushindi wowote
MBUNGE: WATOTO 15 KATI YA 45 DARASANI HAWAFUNDISHIKI

- Neema Lugangira amesema suala la Lishe Shuleni linapaswa kupewa uzito, na hali ya Udumavu inachangia Watoto kutofaulu na kufundishika kwa kiasi kikubwa

Soma > https://jamii.app/WatotoLishe
SIMBACHAWENE: KITAMBULISHO CHA NIDA HAKIHALALISHI KUWA RAIA WA TANZANIA

- Waziri huyo ameeleza Uraia wa Tanzania una #Sheria na mchakato wake

- Kitambulisho ni kwa ajili ya kuwatambua Watu na hutolewa hata kwa Wakimbizi na Wahamiaji wakazi

Soma - https://jamii.app/NIDAUraia
JOSE MOURINHO ATANGAZWA KUWA KOCHA MPYA WA AS ROMA

- AS Roma ya Italia imemtangaza Mourinho (58) kuwa Kocha wake ikiwa ni wiki mbili tangu kibarua chake kiote nyasi akiwa Tottenham

- Amesaini kandarasi ya miaka mitatu na ataanza kuinoa AS Roma mwanzoni mwa msimu ujao

#JFSports
MEXICO: 23 WAFARIKI NA 70 WAJERUHIWA BAADA YA BARABARA YA JUU KUPOROMOKA

- Sehemu ya barabara ya juu iliporomoka na kusababisha treni kuanguka ktk barabara ya chini iliyokuwa na watu wengi

- Kiwango cha barabara hiyo kimewahi kulalamikiwa

Soma > https://jamii.app/AjaliMexico
UMEWAHI KUKUTANA NA MATUKIO YA KISHIRIKINA KIJIJINI KWENU?

- Mdau wa JamiiForums.com anasema kumekuwa na changamoto ya Watu kwenda Vijijini kwao wakati wa likizo kutokana na hofu ya ushirikina/kurogwa hasa pale Mtu anapokuwa amefanikiwa Kimaisha.

- Je, unakubaliana na hoja hii? Ulikutana na tukio gani la kishirikina?

Mjadala zaidi - https://jamii.app/UshirikinaVijijini
#Maisha
MBUNGE: WANANCHI WA KAGERA WANAPIMWA URAIA KWA KUIMBA WIMBO WA TAIFA

- Florent Kyombo amesema Wananchi wa Kagera ambao wanapakana na Nchi 5 wamekuwa wahanga katika kutambuliwa

- Asema, "Wananchi wanaishi kwa tabu kama vile hawapo ndani ya Nchi yao"

Soma https://jamii.app/UraiaKagera
ATCL YASITISHA SAFARI ZA NDEGE KWENDA MUMBAI, INDIA

Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) limesitisha Safari zake kwenda Mumbai nchini India kuanzia leo Mei 4 kutokana na ongezeko la maambukizi ya Virusi vya Corona

- Abiria wote walioathiriwa na uamuzi huu watarudishiwa gharama zao za Safari

#JamiiForums
Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi amefanya uteuzi wa Viongozi mbalimbali wakiwemo:

- Mshenga Haidar kuwa Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme (ZECO)

- Nassor Ameir kuwa Mkurugenzi Mwendeshaji ZSSF

- Shariff Ali kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa ZIPA

Soma > https://jamii.app/Uteuzi7Znz
TANZANIA MEASURES TOWARDS CONTROLLING #COVID19 PANDEMIC: TRAVEL ADVISORY NO. 7

#Tanzania has decided to elevate and enhance prevailing preventive measures especially those with regard to International Travel

Read more at https://jamii.app/COVID-Advisory7

#Unite2FightCorona #Corona2ndWave
UHALIFU WA CHUKI ZA KISIASA WAONGEZEKA UJERUMANI

- Uhalifu unaochochewa kisiasa uliongezeka kwa kasi ambapo 8.5% ya visa vilirekodiwa mwaka 2020 ikilinganishwa na 2019

- Ongezeko la visa vya uhalifu vilifanywa na wafuasi wenye siasa kali

Soma - https://jamii.app/PoliticalHate
MAREKANI: DEREK CHAUVIN AOMBA KESI YAKE KUSIKILIZWA UPYA

- Mwanasheria wake amesema uendeshaji wa kesi dhidi yake haukuwa wa Haki akidai kuna makosa ya kisheria

- Chauvin amekutwa na hatia katika mauaji ya Mmarekani Mweusi George Floyd

Soma > https://jamii.app/KesiChauvin
CHAUREMBO: KATA 3 ZA MBAGALA HAZINA SHULE ZA SEKONDARI

- Akiwa Bungeni, Mbunge wa Jimbo la Mbagala amezungumzia hali ya msongamano wa Wanafunzi ktk Shule mbalimbali zikiwemo Mbande, Chamazi, Mianzini, Kilamba, Nzasa, Mbagala Kuu na Kijichi

Soma > https://jamii.app/ShuleMbagala
MAREKANI: DONALD TRUMP AANZISHA TOVUTI YAKE

- Tovuti yake inakuja saa chache kabla ya Bodi ya #Facebook kutangaza ikiwa akaunti yake itafungwa moja kwa moja au la

- #Twitter imemfungia moja kwa moja Trump aliyekuwa na wafuasi Milioni 88

Soma > https://jamii.app/TrumpPlatform
NJOMBE: MJOMBA ALIYEDAIWA KUBAKA MTOTO ASHINDA KESI. WANANCHI WAIOMBA SERIKALI KUINGILIA KATI

- Mtoto huyo aliyebakwa 2018 akiwa na miaka 3 alisababishiwa maumivu na ulemavu uliopelekea kutafutiwa njia mbadala kwa ajili ya haja kubwa na ndogo

Soma https://jamii.app/MjombaBakaMtoto
MBUNGE: JITIHADA ZA KUKAMATA WAVUVI NI KUBWA KULIKO ZA KUWAWEZESHA

- Mbunge wa Nyasa amehoji, kwanini Mikopo ya Injini za Boti isitolewe kwa mtu mmoja mmoja kuliko kupitia vikundi?

- Asema jambo hilo linachelewesha ukuaji wa Sekta ya Uvuvi

Soma > https://jamii.app/BungeUvuvi
WHO: 46% YA VISA VYA CORONA WIKI ILIYOPITA VIMETOKEA INDIA

- India imerekodi 46% ya maambukizi ulimwenguni na 25% ya vifo vyote vilivyoripotiwa wiki iliyoisha

- Vifo vipya 3780 vimerekodiwa na Serikali imekosolewa kwa kutochukua hatua mapema

Soma > https://jamii.app/WHO-India
RAIS SAMIA AOMBWA KUWAACHIA HURU WANAHARAKATI, WAANDISHI NA WANASIASA

- Wanaharakati kutoka Kenya, Uganda na #Tanzania wamemuomba Rais wa Tanzania kuwaachia huru zaidi ya Wafungwa 100 ambao walifungwa kwa kukosoa Uchaguzi Mkuu wa 2020

Soma - https://jamii.app/ActivistsSamiaKE
#HumanRights