JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MAHAKAMA YAMWACHIA HURU ALIYEKUWA MGOMBEA UBUNGE BUKOBA MJINI

- Chief Kalumuna amesema yeye na wenzake walikamatwa kufuatia vurugu zilizotokea baada ya Mkurugenzi kukataa kuwaapisha

- Asema Serikali iliwashtaki kwa kufanya fujo kipindi cha Uchaguzi

Soma > https://jamii.app/KalumunaHuru
#COVID19: WATAKAOINGIA TANZANIA KUTOKA NCHI ZENYE VIRUSI VIPYA KUKAA KARANTINI

- Kuanzia Mei 04, Wasafiri/Raia wanaorudi kutoka Nchi hizo watakaa Karantini ya lazima kwa gharama zao

- Wasafiri watatakiwa kuzingatia taratibu za kujikinga na maambukizi

Soma https://jamii.app/CovidTZ
BILL NA MELINDA GATES WAACHANA BAADA YA MIAKA 27

- Wanandoa hao wametangaza kutalikiana wakisema hawaamini wanaweza kukua pamoja kama wenza

- Bill Gates mwenye utajiri wa Dola Bilioni 124 na Melinda wanaendesha Bill & Melinda Gates Foundation

Soma > https://jamii.app/BillMelindaDivorce
#COVID19 INDIA: VISA VYAFIKIA MILIONI 20, UPATIKANAJI OXYGEN BADO CHANGAMOTO

- Hospitali zaomba misaada huku Jeshi likitakiwa kusaidia kukabiliana na mlipuko

- Wataalamu waonya idadi halisi za visa na vifo inaweza kuwa kubwa kuliko inavyoripotiwa

Soma https://jamii.app/20MillionIndia
MATIKO: UKAGUZI UNAOFANYIKA MAGEREZANI UNAKIUKA UTU

- Mbunge wa Viti Maalum, Esther Matiko, ameitaka Serikali kufunga mashine maalum za ukaguzi kwenye Magereza

- Asema Wafungwa kukaguliwa wakiwa Uchi wa mnyama ni kinyume na #HakiZaBinadamu

Soma - https://jamii.app/UkaguziGerezani
JOB NDUGAI: KUWEKA WATU NDANI OVYO SIO SAWA

Amesema "Tujifunze kwa Nchi zingine, Mtu anayefahamika anaitwa Kituoni na kufanyiwa mahojiano kisha kurudi nyumbani kwasababu hawezi kukimbia. Huku Askari wanaona kuweka Watu ndani ni raha"

Soma https://jamii.app/NdugaiMahabusu
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
NAIROBI, KENYA: Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewasili Nchini Kenya ambapo ameenda kwa ziara ya siku mbili kuanzia leo Mei 04, 2021 kufuatia mwaliko wa Rais Uhuru Kenyatta

#JamiiForums
NDEJEMBI: TIMU ZINAPOFUNGWA NA YANGA ZIKUBALIANE NA MATOKEO

- Akiwa Bungeni Dodoma, Naibu Waziri wa Utumishi na Utawala Bora amesema baadhi ya Viongozi wa Timu wamekuwa wakitoa kauli ya kwamba walihongwa hususan wanapofungwa na Yanga

Soma > https://jamii.app/RushwaSoka

#Sports
BURKINA FASO: TAKRIBAN WANAKIJIJI 30 WAUAWA

- Wanamgambo wanaosadikika wa kundi la Jihad wamevamia kijiji cha Kodyel na kufanya mauaji hayo

- Mashambulio yameongezeka Nchini humo katika Mikoa inayopakana na #Niger na #Mali

Soma > https://jamii.app/MauajiBurkinafaso

#HumanRightsViolations
ETHIOPIA: MZOZO WA #TIGRAY KUTENGANISHA WATOTO NA WAZAZI WAO

- Zaidi ya #Watoto 5,000 watenganishwa na wazazi wao kutokana na mapigano yanayoendelea

- Watoto hao wako ktk hatari ya kupata njaa, kunyanyasika kimwili na kingono

Soma > https://jamii.app/WatotoTigray
NDALICHAKO: SERIKALI ITAONDOA TOZO YA 6% YA KULINDA THAMANI KTK MIKOPO YA ELIMU JULAI 1

- Pia, Serikali imeiagiza Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi kuondoa tozo ya adhabu ya 10% ambayo inatozwa kwa wanaochelewa kulipa Mikopo

Soma - https://jamii.app/TozoMikopoElimu
MBUNGE: WIZARA YA ELIMU IKUBALI MFUMO UNA TATIZO

- Akiwa Bungeni, Bernadeta Mushashu amesema Wizara ifungue mjadala mpana tuangalie kitu gani kinakosekana na tuongeze nini

- Pia, ametoa wito kwa Serikali kuweka mkakati wa kuajiri Walimu

Soma > https://jamii.app/MfumoElimu